Mukwala Vs Singida BSMukwala Vs Singida BS
  • Simba SC 1-0 Singida Black Stars 28 Mei 2025, ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulioangaziwa na mamilioni ya mashabiki wa Simba na wadau wa soka kuelekea kufunga msimu wa 2024/25 .
  • Bao pekee la straika, Steven Mukwala ndilo liliwapa Simba pointi tatu muhimu katika vita ya ubingwa.
  • Ushindi huo umeifanya Simba SC kufikisha pointi 72 wakiwa kwenye nafasi ya pili dhidi ya Yanga wanaoshikilia usukani na pointio zao 73. 
  • Simba wamezoa pointi zote za Singida BS msimu huu.

Simba SC wapo nafasi ya pili ilihali Singida Black Stars wako nafasi ya nne. Wamecheza jana na Simba kuwafunga bao moja Singinda black stars. Ni wengi walio dhamiria Simba SC kupoteza lakini wamefeli. Soma zaidi kuhusu mchezo wa Simba SC 1-0 Singida Black Stars 28 Mei 2025.

Mchezo Simba SC 1-0 Singida Black Stars 28 Mei 2025 ilikuwaje?

Bao pekee lililofungwa na straika wa Simba raia wa Uganda, Steven Mukwala limetosha kuipa Simba pointi tatu muhimu mbele ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Simba ilianza mchezo huo kwa kasi huku wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini hata hivyo walikosa umakini wakuzitumia. Baada ya majaribio kadhaa langoni mwa Singida BS, Mukwala aliipatia bao hilo pekee dakika ya 42 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ahoua.

Mukwala alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Singida na mlinda mlango wao na kufunga bao hilo kutokea upande wa kulia wa uwanja.

Dakika 15 za mwanzo za kipindi cha pili Singida walifika mara kadhaa langoni mwa Simba, lakini safu ya ulinzi ya Simba ilikuwa imara kuondoa hatari zote.

SOMA HII PIA: Simba SC vs Singida Black Stars mchezo wa Ligi Kuu Bara Mei 28 2025, rekodi, matokeo

Simba sasa yafikisha pointi 72, pointi moja nyuma ya Yanga kuelekea Dabi

Ushindi wa leo umewafanya Simba kufikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 27, ambapo wanaendelea kusalia nafasi ya pili alama moja nyuma ya vinara Yanga huku mchezo wa dabi ukiwa mbele yao.

Kikosi cha Simba kilichoanza mchezo huo

Historia ya Simba itawakumbuka milele- #WenyeNchi #NguvuMoja
Kikosi cha Simba

Kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davis hakubadilisha kikosi chake cha ushindi ambacho Jumapili kilimaliza washindi wa pili kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi cha Simba kilichoanza leo ni: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Chamou, Che Malone, Kagoma, Mutale (Kibu 67′) Ngoma, Mukwala (Ateba 83′), Ahoua (Fernandez 82′), Mpanzu (Hamza 60′), huku Camara akionyeshwa kadi ya njano dakika ya 82 ya mchezo.
Kikosi cha Singida Black Stars kilichoanza leo ni pamoja na : Obasogie, Koffi (Rupia 81′), Imoro (Kennedy 81′), Tra Bi, Assinki, Nashon (Damaro 45′), Chukwu, Bada, Adebayor (Keyekeh 67′), Tchakei (Pokou 45′), Sowah, huku kwa upande wa waliionyeshwa kadi: Nashon 29′ Damaro 73′ Sowah 90+4′

Simba watoa tamko zito ubingwa wa Ligi Kuu Bara

Simba imelazimika kurejea kwenye Ligi Kuu Bara mara baada ya kumalizika rasmi kwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambayo  Simba walicheza fainali siku ya Jumapili na sasa wamerejea Ligi Kuu ya NBC .

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa kwa sasa umeelekeza nguvu zao kwenye michuano hii, na lengo lao ni kuhakikisha wanapambana muda wote ili kupata matokeo chanya.

“Tulifahamu kuwa utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Singida kutokana na ubora walionao, lakini tumerejea kwa ajili ya kukusanya pointi tatu kwenye kila mchezo ambao upo mbele yetu.

“Singida Black Stars ni timu bora na ina kikosi imara na hizi ni mechi za mwisho za kuamua ubingwa tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda ubingwa,” amesema Matola.

SOMA HII PIA: Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live: H2H, uchambuzi, vikosi hivi hapa, Simba kubeba ubingwa?

Mukwala ‘mchezaji bora wa mechi’, anautaka ubingwa

Straika na mfungaji wa goli pekee la mchezo huo, Mukwala ameshukuru sapoti anayoendelea kupewa kutoka kwa mashabiki na viongozi wa timu hiyo na kuahidi mazuri zaidi yanakuja ikiwemo kushinda ubingwa msimu huu.

kizungumza kwa niaba ya wachezaji amesema pamoja na ubora waliokuwa nao Singida, lakini kikosi chao kilijiandaa kuzoa [pointi zote tatu za ushindi.

“Sisi kama wachezaji tumejiandaa kuhakikisha tunashinda nakuchukua alama tatu kwenye kila mchezo ulio mbele yetu.

Simba SC yazoa pointi sita za Singida Black Stars

Tukafurahi leo- #WenyeNchi #NguvuMoja
Simba wakishangilia bao Singida

Ikumbukwe kabla ya mchezo wa leo, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Liti Simba SC waliibuka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Fabrice Ngoma.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.