- Simba SC mshindi wa pili Kombe la Shirikisho la CAF, yapoteza mbele ya RS Berkane.
- Yusuph Kagoma kiungo mkabaji wa Simba SC aonyeshwa kadi nyekundu kwenye fainali yake ya kwanza Afrika.
- RS Berkane watwaa ubingwa wa CAF, VAR yawapa kicheko huku Simba SC ikiwa ni kilio.
Simba SC 1-1 RS Berkane ya Morocco huku yatwaa ubingwa wa CAF Mei 25 2025 mbele ya wenyeji Simba SC kwenye ardhi ya Tanzania baada ya dakika 90 kukamilika katika msako wa taji kubwa Afrika ambalo lina thamani kubwa kutokana na ukubwa wa mashindano yenyewe na ushindani ndani ya timu zilizopo Afrika.

Simba SC kwenye mchezo wa mchezo wa leo Mei 25 walikuwa na mabadiliko kadhaa kwenye eneo la wachezaji wao ambapo ni Kibu Dennis kiungo mshambuliaji aliyeanza mchezo wa nchini Morocco alianzia benchi nafasi yake ilichukuliwa na Joshua Mutale.
Mutale alikuwa na mchezo mzuri katika dakika ambazo alicheza huku akifungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo wa fainali ya pili ambao umegotea kwa Simba SC kugotea nafasi ya pili na mabingwa ni RS Berkane ya Morocco.
Inahusiana na hii:RS Berkane 2-0 Simba SC: Magoli, takwimu, yaliyotokea ‘haijaisha mpaka iishe’
Dakika 90 zawamaliza Simba SC, RS Berkane wapeta
Dakika 90 za ugenini kwenye mchezo uliochezwa Mei 17 ziliwamaliza Simba SC kwa kuwa waliruhusu mabao ya mapema ndani ya dakika 15 za mwanzo kwenye mchezo huo wa fainali uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.
Ushindi wa RS Berkane wakiwa nyumbani uliwapa nguvu kuja kumaliza kazi katika mchezo wa fainali Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Ikumbukwe kwamba awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
RS Berkane walicheza kwa kujiamini kipindi cha kwanza na walikuwa wakishambulia kwa kasi huku Simba SC makosa makubwa yakiwa kwenye eneo la ulinzi na umaliziaji nafasi ambazo walikuwa wanazipata.
Soma na hii:Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live: H2H, uchambuzi, vikosi hivi hapa, Simba kubeba ubingwa?
Kadi nyekundu yawavurugia Simba SC
Kadi mbili za njano ambazo alipata kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma kwenye fainali ya pili kuliivuruga Simba SC ambayo ilianza kucheza ikiwa pungufu. Kagoma alikuwa imara katika ukabaji akizuia hatari nyingi kwa wakati ndani ya uwanja.
Shomari Kapombe, Fadlu Davids na Seleman Matola ambao wapo ndani ya kikosi cha Simba SC walionyeshwa kadi za njano kila mmoja dakika ya 35 kwenye mchezo huo.
Hizi hapa baadhi ya rekodi za wachezaji wa Simba SC vs RS Berkane
Mutale wa Simba SC
Mutale alipiga krosi dakika ya 8, alipiga kona dakika ya 8, alipiga pasi ndefu dakika ya 12, Goal dakika ya 15 ndani ya 18, kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 akimalizia krosi ya Mpanzu ,alicheza faulo dk 26, chezewa faulo dk 35, cheza faulo dk 39, chezewa faulo dk 41 na Ayoub onyeshwa njano dk 41, cheza faulo dk 42, piga kona dk 60, 61.

Ngoma
Fabrince Ngoma wa Simba SC aliokoa hatari dakika ya 26, 27, krosi dk 28, 42.
Steven Mukwala
Mukwala chezewa faulo dk 3, cheza faulo dk 10, krosi dk 35. Alizamisha mpira nyavuni dakika ya 73 VAR ilikataa bao hilo.
Jean Ahoua wa Simba SC
Jean Ahoua piga faulo dk 4, dribe dk 28, piga kona dk 29, 41, 70,80 .
Zimbwe Jr
Zimbwe save dk 4, cheza faulo dk 30, pasi dk 49
Mousa Camara
Camara wa Simba SC pasi dk 4, 28, save dk 36, 38 long pasi dk 45, 65.
Che Malone
Che Malone save dk 2, 8, 15 long lasi dk 57
Mpanzu
Ellie Mpanzu chezewa faulo dk 6, Lamine Camara save, long pasi dk 58, chezewa faulo dk 60, piga kona dk 80.
Yusuph Kagoma
Kagoma save dk 7, 8, cheza faulo dk 10, long pasi dk 40, cheza faulo dk 48, kadi nyekundu akiwa kapewa kadi mbili za njano
Shomari Kapombe
Kapombe rusha dk 8, of target dk 22 ndani ya 18, cheza faulo dk 35 njano dk 35, cheza faulo dk 62, chezewa faulo dk 67.
Munir wa RS Berkane
Munir Mohamed kipa wa RS Berkane aliokoa hatari dakika ya 2, 47 alikuwa ni kipa ambaye aliwazuia washambuliaji wa Simba SC kupata nafasi yakufunga.

Yassin Camara
Yassin Camara nyota wa RS Berkane alitoa pasi dakika ya 2, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 2, alichezewa faulo dakika ya 45 na alimchezea faulo Joshua Mutale dakika ya 72 alichezewa faulo.
Simba SC imepishana na ubingwa ikiwa mshindi wa pili sawa na mtani wake wa jadi Yanga SC ambaye naye alipotinga kwenye fainali Kombe la Shirikisho Afrika aligotea nafasi ya pili. Bado rekodi hazijavunjwa kwa wababe hawa wawili wakiwa na kazi nyingine kwa msimu ujao.

