- Tottenham yatwaa ubingwa wa Europa Legue mbele ya Manchester United iliyokuwa kwenye ubora wake.
- Bruno yupo tayari kuondoka ndani ya Manchester United ikiwa mabosi watahitaji kumuuza.
- Europa League kwa Tottenham yafuta ukame wa miaka 17 bila kutwaa taji.
Fainali ya Europa League ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa mchezo wa mpira ulimwenguni imefika tamati huku kila mmoja akishuhudia mchezo wenye ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 na ubao ukasoma Tottenham 1-0 Manchester United.

Kwenye mchezo huo uliowakutanisha wababe wawili ambao wanacheza Ligi Kuu England yenye ushindani mkubwa, mbabe mmoja kaibuka shujaa kwa bao la maajabu ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo. Ni usiku wa kuamkia Alhamisi, Mei 21 2025.
Tottenham wametwaa taji la Europa League kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United ambapo bao pekee la ushindi lilipachikwa na nyota Brennan Johnson dakika ya 42 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa San Mames.
Hakika ulikuwa ni mchezo wenye kuvutia na mashabiki wengi wa Manchester United walionekana kuwa na huzuni kwa kuwa timu yao haijatwaa taji mbele ya wapinzani wao ambao walipata bao moja kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo. Rekodi zinaonyesha kuwa shuti pekee ambalo lililenga lango kwa washindi wapya wat aji hilo lilikuwa ni moja likiwapa taji.
Ushindi huo kwa Tottenham unaua ukame ambao walikuwa nao kwa muda wa miaka 17 bila kutwaa taji jambo ambalo limeongeza furaha kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Gregg Popovich.

Mara baada ya ushindi waliopata Tottenham, wachezaji walikuwa wanatembea na bango lenye picha ya kocha wao likiwa na nukuu ya kocha hiyo inayosema namna hii: “Mara nyingi nimekuwa sishindi vitu , lakini nina kawaida ya kushinda vitu hasa kwenye mwaka wangu wa pili.”
Kutwaa taji hilo kwa Tottehham ni fursa nyingine kwao kushiriki mashindano makubwa Ulaya ambapo timu hiyo sasa itacheza Champions League licha ya kutokuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya Ligi Kuu England msimu wa 2024/25.
Soma na hii:Man United 4-1 Athletic Club Europa League: Mashetani wekundu kuwavaa Spurs Fainali
Hizi hapa rekodi za mchezo wa fainali

Katika mchezo huo wa fainali, rekodi zinaonyesha kuwa shuti ambalo walipiga Spurs lango la Manchester United likalenga lango ni moja ambalo lilikuwa bao la ushindi katika mchezo huo.
Manchester United ni mashuti matatu walipiga kuelekea langoni kwa mpinzani wao na yote yaliokolewa na kipa wa Tottenham Guglielmo Vicario ambaye alianza kikosi cha kwanza kwenye fainali hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.
Umililiki wa wa mpira ilikuwa ni asilimia 35 kwa Tottenham na Manchester United walikuwa na asilimia 65 za umiliki. Hivyo Man U walikuwa bora katika eneo la umiliki wa mpira.
Faulo ilikuwa 20 kwa Tottenham na 9 ilikuwa ni kwa Manchester United. Kadi za njano mastaa wa Tottenham watatu walionyeshwa na wanne kwa upande wa Man United.
Hakukuwa na kadi nyekundu kwenye fainali na kuotea ni mara moja kwa Tottenham huku Man United wakikutwa katika mtego mara mbili. Mapigo ya kona ni nne kwa Tottenham na 5 kwa Manchester United. Shukrani kwa mlinda mlango Guglielmo Vicario ambaye aliokoa hatari nne kwa Tottenham na Andre Onana wa Manchester United akitunguliwa bao moja.
Hawa hapa 7 walionyeshwa kadi za njano
Walioonyeshwa kadi za njano kwa upande wa Tottenham ni:-Yves Bissouma dakika ya 68, Richarlison dakika ya 58 na Micky Van de Ven dakika ya 49. Manchester United ni Amad Diallo ilikuwa mapema kipindi cha kwanza dakika ya 35, Joshua Zirkzee dakika ya 84, Harry Maguire dakika ya 88 na Johnny Evans dakika ya 90.
Bruno Fernades yupo tayari kuondoka Manchester United
Bruno Fernandes amesema kwamba yupo tayari kuondoka ndani ya kikosi cha Manchester United majira haya ya kiangazi ikiwa klabu itataka kumuuza baada ya kufungwa katika fainali ya Europa League. Na inatajwa kuwa Al-Hilal ya Saudia, wapo tayari kumnunua mchezaji huyo na wapo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza na kumlipa Fernandes karibu pauni milioni 200 kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mazungumzo na wawakilishi wake.
United baada ya kukwama kupata ushindi mbele ya Tottenham katika fainali iliyopigwa huko Bilbao usiku wa Alhamisi kumekuwa na taarifa zinaeleza kuwa wapo wachezaji ambao wataondoka. Licha ya kwamba inaonekana kuwa haiwezekani kumuuza kapteni wao, Fernandes atahama ikiwa biashara hiyo iko katika maslahi ya klabu.

“Nimesema daima nitakuwapo hadi klabu itakaposema ni wakati wa kuondoka. Niko tayari kufanya zaidi kwa ajili ya klabu kwa siku kubwa. Siku ambayo klabu itafikiria kuwa mimi ni mzito sana au ni wakati wa kutengana, soka ni hivi, hujui kamwe. Lakini kila wakati nimesema hivyo na ninaweka neno langu kwa njia ileile.”
Ruben Amorim ambaye ni Kocha Mkuu wa Manchester United amekuwa na msimu mbaya zaidi ndani ya timu hiyo kwenye Premier League ikiingia kwenye historia ya klabu ambapo imekosa kabisa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Source: Tottenham/ Manchester United/ Mail Online

