AzizAziz
  • Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga SC huenda akatangazwa kupata timu mpya muda wowote kuanzia sasa baada ya dili lake kukamilika.
  • Simba SC imetajwa kuwa kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiungo huyo wa Yanga SC anayevaa jezi namba 10.
  • Maxi Nzengeli mfungaji wa bao la kwanza Yanga SC kwenye ligi msimu wa 2024/25 naye kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa.

Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kuna uwezekano mkubwa akaondoka ndani ya kikosi hicho kwenda kupata changamoto mpya ndani ya Wydad Athletic Club baada ya taarifa kueleza kuwa dili la nyota huyo kuibukia kwenye timu hiyo limefikia hatua nzuri.

DUBEEEEEEEEEEEEE ️ (-)
Aziz Ki na Prince Dube kwenye moja ya mchezo wa ushindani. Source: Yanga SC.

Licha ya Aziz Ki kutajwa kuwa katika hesabu za Wydad ilikuwa inatajwa kuwa mabosi wa Simba SC walikuwa wanahitaji saini yake pia ila walisitisha mpango huo baada ya kupata mchezaji mwingine katika eneo la kiungo mshambuliaji.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo ambaye Pyramids walikuwa wanamuhitaji pia kwa sasa ni suala la muda kwa kiungo huyo anayevaa jezi namba 10 akiwa uwanjani kutimiza majukumu yake Aziz Ki kutangazwa kwenye timu mpya ambayo imeinasa saini yake ili akaanze changamoto mpya.

Rekodi za Aziz Ki ndani ya Yanga SC

Aziz Ki alihusika kwenye mabao 29 kati ya 71 yaliyofungwa na Yanga iliyotwaa ubingwa msimu wa 2023/24. Kiungo huyo alichukua tuzo ya mfungaji bora wa mabao alipofunga mabao 21, alikuwa mchezaji bora wa msimu na jina lake lilitajwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Inahusiana na hii:Baada ya Mayele, Pyramids wanamtaka Aziz Ki 2024

Fainali ya CRDB Federation Cup

Kwa msimu wa 2024/25 anaingia kwenye orodha ya mastaa ambao walianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup dhidi ya JKT Tanzania mchezo uliochezwa Mei 18 2025.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania mabao ya Prince Dube dakika ya 41 na Mudathir Yahya dakika ya 89 ambayo yanaipa Yanga SC tiketi kutinga hatua ya fainali.

Yanga SC imetwaa taji la CRDB Federation Cup mara nne mfululizo ikiwa ni rekodi kubwa kuandikwa na timu hiyo ambayo kwa sasa inamsubiri mshindi kati ya mchezo wa Simba SC vs Singida Black Stars, Mei 31 Tanzanite Kwaraa.

Wengine hawa hapa tetesi zao

Mbali na Aziz Ki kutajwa dili lake kukamilika wapo wachezaji wengine ambao wanatajwa kuwa kwenye rada ya timu mbalimbali namna hii:-

Feisal Salum wa Azam FC anatajwa Simba SC na Yanga SC

Kiungo Feisal Salumwa Azam FC ambaye mguu wake wenye nguvu zaidi ni ule wa kulia ndani ya uwanja anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC, Yanga na Kaizer Chiefs.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Feisal yeye alifunga jumla ya mabao 19 alikuwa ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi. Msimu wa 2024/25 katupia mabao manne.

Clement Mzize anatajwa Wydad

Kwenye eneo la ushambuliaji huyu anafanya kazi kubwa akiwa katupia mabao 13 anaitwa Clement Mzize  anatajwa kuwa kwenye hesabu za Wydad Casablanca ya Morocco ili akapate changamoto mpya.

Ellie Mpanzu- Yanga SC

Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye dirisha dogo, Ellie Mpanzu anatajwa kuwa kwenye rada za watani wa jadi wa Simba SC, ambao ni Yanga SC inayohitaji saini ya winga huyo mwenye spidi akiwa uwanjani na uwezo wa kutumia mguu wake wa kulia.

Mpanzu v JKT Tanzania
Mpanzu nyota wa Simba SC anayetajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Source: Simba SC.

Hivi karibuni, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally aliweka wazi kuwa wanatambua vurugu ambazo zipo na kwa timu ambayo inahitaji saini ya Mpanzu inapaswa ifuate utaratibu kumpata.

“Ikiwa kuna timu inamuhitaji mchezaji wetu Mpanzu inapaswa ifuate utaratibu kwa kuwa ana mkataba wa miaka miwili na tupo naye kwa sasa.”

Jonathan Sowah- Yanga SC na Simba SC

Yupo ndani ya kikosi cha Singida Black Stars Jonathan Sowah akiwa katuma jumla ya mabao 11 msimu wa 2024/25. Kwenye mabao ambayo amefunga Sowah hayo 11 alimfunga pia kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Singida Black Stars, pointi tatu zilibaki kwa Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi. Anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC na Simba SC.

Maxi Nzengeli- Simba SC

Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli

Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba SC ambao wanahitaji saini yake kwa ajili ya kuwa naye katika kikosi hicho ambacho kimetinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Nyota huyo mkataba wake na Yanga SC unatarajiwa kugota mwisho msimu utakapoisha taarifa zinaeleza kuwa ameitwa mezani na mabosi wa Yanga SC kumuongezea mkataba mwingine ambapo ni miaka miwili atasaini.

Bado hakuna ambacho kimekamilika kwa sasa zaidi ya tetesi ambapo taarifa zikikamilika kila kitu kitakuwa wazi kama mchezaji husika ataondoka kwenye timu yake ya sasa ama atakwenda kupata changamoto mpya.

Share this: