Magori kwa MkapaMagori kwa Mkapa
  • CAF waipa maswali kibao Simba SC suala la RS Berkane kutafuta hotel mapema Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa fainali ya pili.
  • Simba SC yauza tiketi zaidi ya 12,000 kwa mashabiki ambao wanatambua kwamba mchezo utachezwa Uwanja wa Mkapa.
  • Ukweli utakuwa wazi mapema kabisa wapi itachezwa fainali ya pili itakayoamua mshindi atakayetwaa taji hilo kubwa Afrika.

Sekeseke zito limeibuka kuhusu mechi ya marudiano ya Simba SC vs RS Berkane ya hatua ya fainali ya pili itakayotoa maamuzi ya mshindi wa mwisho wapi itachezwa kwa sasa Uwanja wa Mkapa, Dar ama Uwanja wa Amaan, Zanzibar kutokana na mabadiliko ambayo yametokea ghafla.

Uwanja wa Mkapa
Uwanja wa Mkapa ambao unatarajiwa kuchezwa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika. Source: Simba SC.

Simba SC inayopeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa ina kibarua cha kucheza na RS Berkane kwenye mchezo wa fainali ambapo fainali ya kwanza inatarajiwa kuchezwa Mei 17 nchini Morocco na tayari msafara wa Simba SC umeshawasili kwa maandalizi ya mwisho.

Uwanja ambao awali ulitangazwa utatumika kwa mchezo wa hatua ya fainali ya pili inayotarajiwa kuchezwa Mei 25 2025 ulikuwa ni Uwanja wa Mkapa na tayari tiketi zinaendelea kuuzwa huku kukiwa na mwitikio mkubwa kwa mashabiki kununua tiketi hizo kupata fursa kushuhudia fainali ya kihistoria.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Simba SC kucheza fainali ya CAF ilikuwa 1993 ikigotea nafasi ya pili na sasa inakwenda kucheza kwa mara nyingine fainali hiyo Mei 17 ugenini na ile ya pili itakayoamua mshindi inatarajiwa kuchezwa Mei 25 2025.

Inahusiana na hii:RS Berkane vs Simba SC 17/5/2025, Steven Mukwala aongoza jeshi la Simba kutua kwa kishindo Morocco

Sekeseke la uwanja kubadilishwa lazua gumzo

Mjumbe wa Bodi ya Klabu ya Simba, Crescentius Magori amebainisha kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram kuwa suala hili linaloendelea kuhusu Uwanja wa Mkapa halina ukweli anaamini taarifa zilizofika mezani hazina ukweli.

Mashabiki wa Simba SC
Mashabiki wa Simba SC wakiwa kwenye moja ya mchezo uwanjani. Source: Simba SC.

Magori amemwambia Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe kuwa Watanzania hawapo tayari kwa hilo linaloendelea na kuzuia kutumia Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) kati yao dhidi ya RS Berkane ya Morocco wanaamini sio sawa.

“Rais wa Caf, Mostepe, picha na video hii imechukuliwa sasa hivi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, uwanja upo katika hali nzuri, Rais Motsepe watu wako wanakudanganya kuhusu uwanja. Tunajua Berkane ni ya nani lakini sisi Simba na Watanzania hatuko tayari kwa hili.

Tiketi 12,000 tayari zimeshauzwa kwa Mkapa

“Tayari tiketi 12,000 zimeshauzwa kwa mchezo wa Simba dhidi ya Berkane unaotarajiwa kuchezwa tarehe 25 Mei 2025, je, inawezekanaje CAF kupendekeza kuhamisha eneo kwenda Zanzibar? Uwanja mpya wa Amaan Zanzibar hauwezi kubeba wahudhuriaji 15,000. Hali ya hewa, (ambayo ni kipande cha hofu) inaonyesha kwamba katika tarehe hizo hakutakuwa na mvua Dar es Salaam! CAF inapaswa kuweka eneo la Mkapa ili kuepuka machafuko.

“Hii inaanza kuwa aina ya kashfa, Berkane ilitafuta hoteli huko Zanzibar jana (14/5/25) Simba alipokea barua ya kupendekeza kubadili mahali leo asubuhi (15/5/25) Je, ni vipi Klabu Mwenyeji na Shirikisho hawakujua kuhusu uamuzi wa CAF hadi jana lakini Berkane walijua! Je, Berkane walikuwa sehemu ya mchakato wa kufanya maamuzi kwa CAF? Tukio hili haliwezi kupuuziwa mbali na taasisi huru!

Tamko la Simba SC hili hapa

Kufuatia sitofahamu hiyo kuhusu wapi mchezo wa pili hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika utachezwa, uongozi wa Simba SC umetoa taarifa rasmi kupitia ukurasa wa Instagram.

Taarifa ya Simba SC imeeleza namna hii: “Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025.”

Simba SC ndani ya Morocco

Mei 14 msafara wa Simba SC uliwasili Morocco kwa maandalizi ya kazi yao kuwakabili RS Berkane kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya kwanza ambayo inasubiriwa kwa shauku kubwa kutokana na kila timu kuwa kamili kwa mchezo huo.

Ahoua J C
Ahoua J C

Inahusiana na hii:RS Berkane vs Simba SC 17/5/2025, Steven Mukwala aongoza jeshi la Simba kutua kwa kishindo Morocco

Miongoni mwa wachezaji wa Simba SC ambao wapo nchini Morocco ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids. Awesu Awesu ambaye ni kiungo mshambuliaji, Steven Mukwala huyu ni mshambuliaji, Shomari Kapombe ambaye ni beki mwenye uzoefu mkubwa na nahodha Mohamed Hussen Zimbwe Jr.

Yusuph Kagoma, Kibu Dennis, Mavambo, Ellie Mpanzu. Ukiweka mbali Zimbwe Jr kipa namba moja Moussa Camara, Ally Salim na Hussen Abel hawa wapo kwenye eneo la makipa ambao wapo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Share this: