- Clement Mzize wa Yanga SC ni mzawa anayetamba kwenye eneo la ushambuliaji ndani ya ligi akitunishiana misuli na wachezaji wakigeni.
- Jean Ahoua wa Simba SC anaongoza chati ya ufungaji ndani ya ligi akiwa mkali kwenye kutumia mguu wa kulia kwenye kupeleka maumivu kwa wapinzani wao uwanjani.
- Jonathan Sowah wa Singida Black Stars ni mwiba mkali akiwa ni ingizo jipya katika kikosi cha walima alizeti, hacheki na mtu akiwa ndani ya 18.
Vinara kwa ufungaji kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika vita yao inazidi kuwa kali katika kuwania kiatu cha ufungaji bora mwisho wa msimu. Eneo la ushambuliaji linaonekana kuchangamka zaidi katika kukamilisha mzunguko wa pili huku wachezaji wakigeni wakiwaacha mbali wazawa kwenye kufunga mabao mengi.
Wachezaji wakigeni katika eneo la ufungaji wanaonekana kuwa na kasi kubwa huku wazawa wakiwa kwenye kasi ya kinyonga. Clement Mzize ambaye anacheza kikosi cha Yanga SC anaongoza kwenye orodha ya wafungaji ndani ya uwanja.
Hapa tunakuletea orodha ya wafungaji vinara katika kucheka na nyavu namna hii:-
Jean Ahoua wa Simba SC mabao 15

Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC, raia wa Ivory Coast anaongoza kwenye orodha akiwa na mabao 15. Ni mechi 23 kacheza akitumia dakika 1,689 uwanjani akikosekana kwenye mechi mbili kati ya 25 ambazo Simba SC imecheza.
Kwenye mabao 15 ambayo kafunga, katumia mguu wa kulia kufunga mabao 14 na pigo la kichwa ni bao moja alifunga dhidi ya Pamba Jiji, Uwanja wa KMC Complex.
Clement Mzize wa Yanga SC, mabao 13
Clement Mzize wa Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni namba mbili kwenye orodha ya vinara katika ufungaji. Mzize kafunga mabao 13. Yanga SC baada ya mechi 26 imetupia mabao 68 ndani ya ligi ni timu namba moja yenye mabao mengi kibindoni msimu wa 2024/25.
Prince Dube wa Yanga mabao 12
Prince Dube mshambuliaji wa Yanga kafunga mabao 12 yeye ni raia wa Zimbabwe. Ukurasa wa mabao wa Dube ulifunguliwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Ni mabao matatu alifunga akiwa nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi.
Mbali na kufunga Dube katengeneza pasi 8 za mabao akihusika kwenye mabao 20 kati ya 68 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 70.
Leonel Ateba wa Simba SC mabao 12

Mshambuliaji wa Simba SC inayofundishwa na Fadlu Davids, Ateba rai awa Cameroon amefunga jumla ya mabao 12. Kwenye mabao hayo Ateba alipachika mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Mei 8 2025.
Jonathan Sowah wa Singida Black Stars mabao 11
Mshambuliaji wa Singida Black Stars ni ingizo jipya ndani ya timu hiyo kwenye dirisha dogo akiwa katupia jumla ya mabao 11. Huyu ni raia wa Ghana timu ya Singida Black Stars ikiwa nafasi ya nne na pointi 53 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 40.
Elvis Rupia wa Singida Black Stars mabao 10
Mshambuliaji wa Singida Black Stars Elvis Rupia kwenye chati ya ufungaji ni mabao 10 kafunga ndani ya ligi. Huyu ni raia wa Kenya ambaye ana zali la kucheka na nyavu. Singida Black Stars imefunga mabao 40 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Steven Mukwala wa Simba SC mabao 9
Mshambuliaji wa Simba SC, Steven Mukwala yeye amefunga jumla ya mabao 9 ni raia wa Uganda. Mukwala ni dakika 791 katumia uwanjani akicheza mechi 21. Kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania alitoa pasi ya bao ikiwa ni ya tatu kwake alimpa Fabrince Ngoma dakika ya 45.
Simba SC baada ya kucheza mechi 25 ilipata ushindi kwenye mechi 21, sare tatu na kuambulia kichapo katika mchezo mmoja dhidi ya Yanga SC. Kwenye upande wa safu ya ushambuliaji ni mabao 60 timu hiyo imefunga huku Mukwala akihusika kwenye mabao 12.
Pacome Zouzoua wa Yanga SC mabao 9

Kiungo mshambuliaji wa Pacome Zouzoua kafunga jumla ya mabao 9 ndani ya kikosi cha Yanga SC. Mbali na kufunga, Pacome ni mkali kwenye kutengeneza pasi za mwisho akiwa katengeneza pasi 9 za mabao msimu wa 2024/25.
Kwenye msimamo Yanga SC ni namba moja ikiwa na pointi 70, inaongoza kuwa timu namba moja yenye mabao mengi ambayo ni 68. Katika mabao hayo 68, Pacome kahusika kwenye jumla ya mabao 18 kwa kuwa kafunga mabao 9 na kutoa pasi 9 za mabao. Katika mabao hayo 9 ya Pacome ambayo alifunga alipachika bao moja kwa mkwaju wa penati ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Vita hii bado ni mbichi kwa kuwa Yanga SC ina mechi nne mkononi kukamilisha mzunguko wa pili, Singida Black Stars ina mechi tatu na Simba SC ni mechi tano zimesalia hivyo mchezaji atakayetwaa tuzo hiyo ambayo kwa msimu wa 2023/24 alitwaa Aziz Ki wa Yanga SC alipofunga mabao 21 atafahamika.

