Fadlu MastaFadlu Masta
  • VAR yaipunguzia kasi Stellenbosch FC, kicheko kwa Simba SC dakika 180.
  • Ellie Mpanzu hana huruma akiwa uwanjani anawatesa wapinzani anavyotaka.
  • Bao la Jean Ahoua na maajabu yake kwenye anga la kimataifa.

Stellenbosch FC na Simba SC dakika 180 zimekamilika kwenye hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika huku Simba SC ikitinga hatua ya fainali.

Hatuishii Hapa- #TunaitakaFainali #WenyeNchi #NguvuMoja
Mukwala na Camara nyota wa Simba SC baada ya kutinga fainali kimataifa. Source: Simba SC.

Ngoma ilikuwa nzito kwa wababe hawa kusaka tiketi kutinga hatua ya fainali kutokana na kila timu kuchanga karata zake kwa umakini.

Aprili 20 2025 kwenye nusu fainali ya kwanza Uwanja wa Amaan baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Stellenbosch FC. Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Jean Ahoua dakika ya 44.

Kwenye nusu fainali ya pili nchini Afrika Kusini kukamilisha dakika 180, Stellenbosch FC wakiwa nyumbani walikwama kupata matokeo chanya na bao moja likaipeleka Simba SC fainali.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza kiungo Ahoua licha yakufunga bao moja kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 alikosa nafasi ya wazi kufunga bao dakika ya 90 kwa pasi ya Ellie Mpanzu.

Jean Ahoua (-)
Jean Ahoua nyota wa Simba SC aliyefunga bao la ushindi kimataifa. Source: Simba SC.

Hapa tunakuletea rekodi za nusu fainali ya pili kwa wachezaji wa timu zote mbili walichokifanya katika dakika 90 za msako wa ushindi:-

MASULUKE

Kipa wa Stellenbosch FC, Oscar Masuluke alikomba dakika 90 mazima na aliokoa hatari dakika ya 73 iliyopigwa na Mpanzu.

NDULI

Nyota Nduli wa Stellenbosch FC alipiga shuti ambalo lilikwenda nje ya lango dakika ya 38. Nyota huyu hakukomba dakika 90 aligotea dakika ya 82 nafasi yake ikichukuliwa na Philander.

PALACE

Palace ambaye aliingia kipindi cha pili dakika ya 63 akichukua nafasi ya Busaka alipiga shuti ambalo lilikwenda kwenye nyavu za Simba ilikuwa dakika ya 77 baada ya wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Mohamed Hussen kuomba mwambuzi aangali VAR bao hilo lilifungwa kwa kuwa kuna mchezaji alikuwa ameotea.

TOURE

Toure wa Stellenbosch FC alipiga mashuti mawili ambayo yalikwenda nje ya lango ilikuwa dakika ya 39 kwa pigo la kichwa na alipiga shuti ambalo lililenga lago dakika ya 45.

BASADIEN

Basadien wa Stellenbosch FC alipewa majukumu ya  kurusha dakika ya 44, 45. Khiba naye alirusha dakika ya 72.

MAPIGO YA KONA

Dakika 45 za mwanzo Stellenbosch FC walipata kona zaidi ya mbili ambazo ilikuwa ni dakika ya 38, 39, 44, 45.

SIMBA SC UGENINI

Simba v Stelle
Kibu Dennis kiungo wa Simba SC akiwa chini ya ulinzi mkali. Source: Simba SC.

Kipa wa Simba Moussa Camara aliokoa hatari dakika ya 36, 45, 45 na kukamilisha dakika za mwanzo lango likiwa salama. Kipindi cha pili Camara aliokoa hatari dakika ya 47, 69,70, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86 kwa kosa ambalo mwamuzi alitafsiri kuwa alikuwa anapoteza muda.

MUKWALA

Mshambuliaji Steven Mukwala alianza kikosi cha kwanza cha Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids na alicheza faulo dakika ya 53 aligotea dakika ya 53 nafasi yake ilichukuliwa na Leonel Ateba.

YUSUPH KAGOMA

Kwa kiungo mkabaji Yusuph Kagoma kwenye harikari za kuokoa alicheza faulo dakika ya 36. Kagoma kipindi cha pili alicheza faulo dakika ya 51 alimchezea Titus.

SHOMARI KAPOMBE

Shomari Kapombe alipewa majukumu ya kurusha ilikuwa dakika ya 41, 43. Kapombe aliokoa hatari dakika ya 86. Kapombe rusha dakika 48 alicheza faulo dakika 59, alipiga kona dk 73.

KIBU D

Kibu Dennis alichezewa faulo dakika ya 14 iliamuliwa penati na mwamuzi ikafutwa baada ya kutazama VAR. Kibu alicheza faulo dakika ya 81 na aliokoa hatari dakika ya 88.

MPANZU

Ellie Mpanzu alichezewa faulo dakika ya 45 na Traore. Mpanzu kipindi cha pili alichezewa faulo dakika ya 67, 80. Che Malone aliingia dakika ya 86 kuchukua nafasi ya Mpanzu.

JEAN AHOUA

Jean Ahoua alipewa jukumu la  kupiga faulo dakika ya 45 alipiga kona dakika ya 45. Alichezewa faulo nyingine dakika  45 na Kezy. Kipindi cha pili alichezewa faulo dakika ya 48, 55 na Moloisane. Hakukomba dakika 90 aligotea dakika ya 64 ni Mavambo ambaye mpira wake wa kwanza kupiga ilikuwa dakika ya 65 ulikwenda nje.

HAMZA JR

Hamza Jr aliokoa hatari dakika ya 43, Chamou aliokoa hatari dakika ya 45. Kipindi cha pili Hamza aliokoa hatari dakika ya 67, 68.

ZIMBWE JR

Nahodha Zimbwe Jr alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 49, 62, 64, 69. Beki huyu hakokomba dakika zote 90 aligotea dakika ya 86 Nouma aliingia.

CHAMOU

Nyota wa Simba SC Chamou alionekana  kucheza faulo dakika ya 54 ambayo iliamuliwa kuwa penati ndani ya 18, VAR ilikataa tukio hilo.

DAKIKA 13 ZILIONGEZWA

Kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Stellenbosch FC dhidi ya Simba SC ya Tanzania ni dakika 13 ziliongezwa kusaka mshindi wa jumla.

Kipindi cha kwanza ziliongezwa dakika 5 na kipindi cha pili ziliongezwa dakika 8 nakufanya jumla dakika 13 ziongezwe kwenye mchezo huo.

Simba SC inatinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa faida ya bao 1-0 ililofunga katika nusu fainali ya kwanza mtupiaji akiwa ni Jean Ahou anayenolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Share this: