Mwenda Israel (-)Mwenda Israel (-)
  • Yanga wakusanya silaha zote za maangamizi kwa kazi Muungano Cup 2025.
  • Singida Black Stars, Coastal Union ya Tanga majanga dakika 90 huko.
  • Mkali wa kudaka mpaka mishale Djigui Diarra kamili gado kwa kazi.

KVZ FC vs Yanga mchezo wa hatua ya robo fainali Muungano Cup 2025 unatarajiwa kuchezwa Aprili 26 2025 kwa wababe hao kuvuja jasho dakika 90 kusaka tiketi kutinga nusu fainali.

Diara
Diara kipa namba moja wa Yanga 2024/25. Source: Yanga.

Mashindano haya yanafanyika visiwani Zanzibar ambapo mchezo wa ufunguzi ulikuwa na ushindani mkubwa mwisho ubao ukasoma JKU SC 2-2 Singida Black Stars. Mshindi alipatika kwa penati alikuwa ni JKU SC alishinda 6-5.

YANGA JESHI ZIMA NDANI YA ZANZIBAR

Aziz
Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga 2024/25. Source: Yanga.

Yanga haina jambo dogo ambapo kikosi kizima kimeibukia Zanzibar kwa ajili ya kupambania taji la Muungano ambapo Aprili 26 2025 watakuwa na kazi yakusaka ushindi

Wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Yanga ni Jonas Mkude, Aziz Ki, Djigui Diarra, Dickson Job, Aboutwalib Mshery, Bakari Nondo ambaye ni nahodha, Maxi Nzengeli huyu anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga bao ndani ya ligi kwa Yanga.

Maxi alipachika bao hilo kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba baada ya dakika 90 ubao ukasoma Kagera Sugar 0-2 Yanga bao la pili lilifungwa na nyota Clement Mzize ambaye alifunga akaunti ya mabao ugenini.

Boka, Israel Mwenda, Kennedy Musonda, Kibwana Shomari, Mudathir Yahya, Farid Mussa ni miongoni mwa wachezaji waliopo Pemba.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kwenye ligi katika mechi 26 ilipata ushindi kwenye mechi 23 ikipoteza mechi mbili pekee.

Mechi ambazo Yanga ilipoteza ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC na Yanga 1-3 Tabora United, sare ni JKT Tanzania 0-0 Yanga. Safu ya ushambuliaji ni namba moja kwenye kutupia ikiwa na mabao 68.

Ikumbukwe kwamba katika mechi za mzunguko wa pili Yanga walipokutana na wapinzani hao walisepa na pointi tatu mazima kwa kulipa kisasi mbele yao ndani ya dakika 90.

Dhidi ya Tabora United mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa walishuhudia ubao ukisoma Tabora United 0-3 Yanga na ule dhidi ya Azam FC baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-2 Yanga.

Mabao kwenye mchezo dhidi ya Azam FC yalifungwa na Pacome ambaye alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo huo baada ya kupata maumivu na bao la ushindi lilifungwa na Prince Dube lilidumu mpaka dakika 90 ya mchezo.

Ipo wazi kwamba Dube aliibuka ndani ya kikosi cha Yanga akitokea Azam FC hivyo aliwatungua mabosi wake wa zamani na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kwenye Dar Dabi.

HATARI YA YANGA KUCHEKA NA NYAVU

Wakiwa ni vinara wa ligi Yanga wamekomba  dakika 2,340 uwanjani baada ya kucheza jumla ya mechi 26 za ligi ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Yanga ina wastani wa kuwa na hatari kwenye kufuga bao moja kila baada ya dakika 34 kwenye mechi ambazo wamecheza wakiwa wametupia jumla ya mabao 68

WAKALI WAKUCHEKA NA NYAVU

Ndani ya Yanga wakali kwenye kucheka na nyavu wametulia wakiongozwa na mzawa Clement Mzize ambaye katupia jumla ya mabao 13 akiwa namba moja kwa wakali wakucheka na nyavu ndani ya ligi.

Mzize kwenye mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Fountain Gate ambayo nit imu namba moja kufungwa mabao mengi kwenye ligi ambayo ni 51 alifunga mabao mawili na alichaguliwa kuwa mchezaji bora ilikuwa ni Aprili 21.

DUBE YUMO

Prince Dube ni namba mbili kwa wakali wakucheka na nyavu kwenye ligi akiwa katupia mabao 12 na katengeneza pasi 8 za mabao akiwa kahusika kwenye mabao 20 msimu wa 2024/25.

Huyu ni namba moja kwa wakali waliohusika kwenye mabao mengi ndani ya uwanja anafuatiwa na Jean Ahoua wa Simba aliyefunga mabao 12 na kutoa pasi 7 za mabao hivyo kahusika kwenye mabao 19 kati ya 52 yaliyofungwa na Simba iliyo nafasi ya pili.

UKUTA WAO HAUVUJI HOVYO

Job D
Job Dickson beki wa Yanga inayoshiriki Muungano Cup 2025.Source: Yanga.

 Ukuta wa Yanga ni namba mbili kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ambayo ni 10 ni wastani wakuokota bao moja nyavuni kila baada ya dakika 234. Kipa namba moja ni Djigui Diarra ambaye ana hati safi 14 kwenye mechi za ligi.

Yanga ni vinara kwenye ligi wakiwa na jumla ya pointi 70 timu inayoshika namba 16 ni Ken Gold baada ya kucheza jumla ya mechi 27 kibindoni ina pointi 16.

MUUNGANO CUP BALAA

Muungano Cup imepamba moto 2025 ambapo timu mbili kutoka bara zimefungashiwa virago kwa kugotea hatua ya robo fainali, Aprili 24 2025 Singida Black Stars ilimaliza mwendo na Aprili 25 2025, Coastal Union ilikuwa timu ya pili kwa kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto SC.

Share this: