BENCHI la ufundi Simba linaloongozwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Seleman Matola ambaye ni msaidizi limeweka wazi kuwa watapambana kwa hali na mali kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kimataifa ugenini ndani ya dakika 90 nchini Misri kutokana na maandalizi ambayo yanaendelea.
Kikosi cha Simba kipo nchini Misri kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa kimataifa hatua ya robo fainali dhidi ya Al Masry mchezo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025 na robo fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa Aprili 9 2025 Uwanja wa Mkapa.

Usisahau kwamba unaweza kujishindia mamilioni ya pesa kwa kuendelea kuweka ubashiri wako wa mchezo huu na mingine mingi kupitia Kampuni bora ya kubashiri ya Sportpesa ambayo inakupa ‘odds’ kubwa na za kipekee. Tembelea sasa www.sportpesa.co.tz.
Machi 28 msafara wa Simba ulikwea pipa kuibukia Misri na mchezo wao wa mwisho kufungia Machi 2025 ilikuwa dhidi ya Big Man uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex baada ya dakika 90 Machi 27 ubao ulisoma Simba 2-1 Big Man.
Matokeo hayo yanaipa tiketi Simba kutinga hatua ya robo fainali Kombe la CRDB Federation Cup ambapo kwenye mchezo huo walikosekana mastaa wao sita ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania. Na mabao yalifungwa na Joshua Mutale dakika ya 16 na Leonel Ateba dakika ya 31 kwa mkwaju wa penati na bao pekee la Big Man likifungwa na Joseph Henock dakika ya 45.

Fadlu amesema kuwa kila mchezo ni muhimu kwao kupata matokeo na uzoefu ambao wamepata katika mechi za hatua ya makundi unawaongezea nguvu ya kufanya vizuri kutokana na wachezaji ambao walikuwa hawajacheza mechi za kimataifa kutambua namna hali inavyokuwa.
“Kwenye mechi za mwanzo unaona kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa hawana uzoefu wa kucheza mechi hizi za kimataifa lakini kwa kucheza mechi nyingi hatua ya makundi kumetupa nguvu na uzoefu kwa mechi zijazo.
“Tunatambua kwenye hatua hii ambayo tupo wapinzani wetu wanahitaji kupata ushindi kama ambavyo nasi tunahitaji hivyo kikubwa ni utayari na maandalizi mazuri, hilo tunalifanyia kazi na kwenye eneo la mazoezi imekuwa hivyo.
“Haitakuwa kazi rahisi kutafuta ushindi na tunaanzia ugenini hii itatupa muda mzuri kutafuta ushindi wa jumla kwenye mchezo wa nyumbani ambao tutacheza Uwanja wa Mkapa, tupo tayari na kinachohitajika ni matokeo mazuri.”
SEMAJI LAUNGURUMA NAMNA HII
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kugotea hatua ya robo fainali mara nyingi hawapendi kuona inatokeo kwa mara nyingine malengo ni kusonga mbele hatua inayofuata.
Ally amesema kuwa kwenye mashindano ya kimataifa wamekuwa na mwendelezo mbaya kuishia hatua ya robo fainali jambo ambalo linawaumiza kwa kuwa hawavuki mbele hivyo watapambana kuvunja rekodi hiyo.
“Tumekuwa na mwendelezo wa kuishia katika hatua ya robo fainali mara nyingi, hii hatuifurahii kwa kuwa mwisho wa kujifunza sasa inatosha, mara ya kwanza ya pili yatatu mpaka tano bado ni robo fainali sasa tunahitaji kuvuka hatua hii hadi nusu fainali.
“Kwa sasa tupo tayari kwa mapambano hasa ukizingatia kwamba kwenye ukanda wa Afrika Mashariki Simba ni timu pekee ambayo imebaki katika mashindano makubwa hivyo tunakwenda kifua mbele kupeperusha bendera kwa ukubwa.
“Ili kuonyesha ukubwa ni lazima kupata matokeo mazuri kwa kuwa wapo ambao walikuwa na kelele sasa hawapo tumebaki wenyewe katika mashindano makubwa Afrika na tunajivunia hilo kwani walipoishia hatua ile ya makundi niliwaambia tumefurahi.
“Lakini sio walipoishia hatua ya makundi, nilikutana nao hapa siku moja wakiwa wanasafiri Terminal 3 nikawaambia hii ni safari yenu ya mwisho, wakacheka hatimaye yametimia wao wameondoka sisi bado tupo na tunafurahi kwelikweli.
“Ubaya ubwela hauna suala la kurudi nyuma ni mbele kwa mbele na kazi kubwa inaendelea kufanyika chini ya benchi la ufundi tunaamini kwamba matokeo yatapatikana na Wanasimba watafurahi.”
HAWA HAPA WACHEZAJI WALIOPO MISRI
Moussa Camara, Ally Salim na Hussen Abel kwa upande wa makipa. Mabeki ni Karaboue Chamou, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Valentine Nouma, David Kameta, Kelvin Kijili. Viungo ni Yusuph Kagoma, Fabrince Ngoma, Elie Mpanzu, Deborah Fernandez, Ladack Chasambi, Kibu Dennis, Awesu Awesu, Jean Ahoua, Augustine Okejepha na Joshua Mutale.

Washambuliaji ni Leonel Ateba na Steven Mukwala. Kwa upande wa washambuliaji ni Valentino Mashaka hatakuwa kwenye kikosi hicho huku Mzamiru Yassin ambaye ni kiungo mkabaji, Che Malone ambaye ni beki na Aishi Manula ambaye ni kipah awa watakosekana kwenye mchezo kwa kuwa hawapo fiti.

