Bacca VibeBacca Vibe

NDANI ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC kuna timu tano ambazo zimekuwa na ukuta imara kwenye eneo la ulinzi hivyo kupenya katika ngome zao ni lazima ujipange kinomanoma. Ipo wazi kwamba kwa sasa burudani ambayo ilikuwa imesimama kwa muda inarejea ndani ya msimu wa 2024/25 hivyo kutakuwa na dakika 90 za kazi kwa wababe ndani ya ligi.

Dube
Prince Dube, Aziz, Mudathir nyota wa Yanga 2024/25. Source:Yanga

Ikumbukwe kwamba Februari Mosi mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga inayodhaminiwa na SportPesa itakuwa uwanjani kusaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa KMC, Complex na Yanga imekuwa na rekodi nzuri kwenye mechi za KMC ikishinda mabao zaidi ya manne.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mechi nne ambazo Yanga imecheza Uwanja wa KMC, Complex tatu zikiwa ni za ligi na moja ya CRDB Federation Cup zote ilishinda kwa mabao zaidi ya mawili, ni mabao 16 imefunga ikiruhusu mabao mawili pekee yakufungwa.

HAWA KUWAFUNGA UJIPANGE

Kwenye mzunguko wa kwanza katika ligi namba nne kwa ubora rekodi zinaonyesha kuwa timu ambayo iliruhusu mabao mengi ya kufungwa ni Fountain Gate ambayo inaonesha kuwa ukuta wake ni nyanya ikiwa imeruhusu mabao 32 baada ya kucheza mechi 16.

Hapa tunakuletea timu tano ambazo zimefungwa mabao machache zaidi hivyo kwa wapinzani ni lazima wajipange kupenya ngome zao namna hii:-

SIMBA

Aziz KI V Chemalone
Aziz KI akipambana kupenya ngome ya Simba dhidi ya Che Malone mchezo wa Kariakoo Dabi. Source: Yanga.

Vinara wa ligi wakiwa na pointi 40 ukuta wao umekuwa imara ni namba moja kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ambayo ni matano baada ya kucheza mechi 15. Licha ya makosa ambayo safu ya ulinzi imekuwa ikifanya yale yanayojirudia bado kazi kubwa ilifanyika kwa mlinda mlango Moussa Camara ambaye alikaa langoni kwenye mechi 15 akikusanya hati safi 12 alifungwa kwenye mechi tatu.

Dhidi ya Yanga mchezo pekee ambao Simba ilipoteza katika mzunguko wa kwanza jitihada za beki Shomari Kapombe kuokoa krosi ya Maxi Nzengeli ziligonga mguu wa Kelvin Kijili ambaye alijifunga kwenye mchezo huo.

Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, mabao yote Camara alitunguliwa nje ya 18 baada ya wachezaji wa Coastal Union kusoma madhaifu yake na namna safu ya ulinzi ilivyokuwa ikifanya makosa kwenye kukaba hasa mpira ukiwa nje ya 18.

YANGA

Ramovic Sead
Ramovic Sead, Kocha Mkuu wa Yanga, 2024/25. Source: Yanga.

Kwenye msimamo wa ligi Yanga ni namba mbili chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic ni mabao sita ukuta wat imu hiyo uliruhusu na mchezo ambao walifungwa mabao mengi ilikuwa Yanga 1-3 Tabora United. Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex langoni alianza kipa namba moja Djigui Diarra ambapo Yanga ilipoteza pointi tatu mazima baada ya dakika 90.

Mchezo wa pili Yanga kutunguliwa mabao mengi ilikuwa Yanga 3-2 Mashujaa, mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex wakati Yanga ikisepa na pointi tatu mazima huku rekodi ya hat trick ikiandikwa ndani ya msimu wa 2024/25 mtupiaji alikuwa ni Prince Dube, ilikuwa ni Desemba 19 2024.

AZAM FC

Mustapha
Mustapha kipa namba moja wa Azam FC 2024/25. Source: Azam FC.

Matajiri wa Dar, Azam FC kwenye msimamo wa ligi wamekusanya pointi zao 36 nafasi ya tatu na pia kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ndani ya ligi ni namba tatu ikiwa imeruhusu mabao 8 pekee kwenye mechi 16.

Azam FC kipa wao namba moja ni Mohamed Mustapha yeye alikaa langoni kwenye mechi 12 katunguliwa mabao yote 8 huku miongoni mwa hay oni lile alilofungwa na Said Ndemla katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18.

Ni dakika 990 kakomba Mustapha akiwa na hati safi tano kwenye mechi za mzunguko wa kwanza mabao mengi ilikuwa ni makosa yake binafsi kwenye ukoaji hivyo ana kazi kubwa kufanyia kazi makosa yake ndani ya mzunguko wa pili.

SINGIDA BLACK STARS

Kipa namba moja wa Singida Black Stars ni Metacha Mnata ambaye amekaa langoni kwenye mechi 16 akikomba jumla ya dakika 1,417 akiwa miongoni mwa wachezaji waliokomba dakika nyingi uwanjani.

Singida Black Stars ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 33 baada ya kucheza mechi 16 ni mabao 11 safu ya ulinzi imefungwa ambapo mech izote langoni alikaa Mnata.

JKT TANZANIA

Jean Ahoua
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba alifunga dhidi ya JKT Tanzania. Source: Simba.

Wajeda hawa ndani ya ligi wameonyesha ushindani mkubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja. Itakumbukwa mechi yao ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba, Uwanja wa KMC Complex walikaza na dakika za jioni Simba ikapata penalti na mtupiaji alikuwa Jean Ahoua dakika ya 90.

JKT Tanzania ni mabao 12 imefungwa ikiwa namba tano kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache kwenye msimamo ipo nafasi ya   8 ikiwa na pointi zake 19 ndani ya msimu wa 2024/25.

Share this: