KUMEPAMBAZUKA ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inadhaminiwa na NBC inarejea kwa mara nyingine tena baada ya muda kidogo kusimama kutokana na ratiba ya Mapinduzi Cup na Fainali za Mataifa ya Afrika, kwa wachezaji wa Ndani, (CHAN) ambapo Tanzania ni wenyeji.
Ikumbukwe kwamba kwa sasa ni ligi namba nne kwa ubora Afrika na mabingwa watetezi wa taji la ligi ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa.

Muda wa kubutua mkwanja mrefu na SportPesa kwa kubashiri mechi zote na sio ligi ya Bongo mpaka zile za Ulaya ni wakati wako kutengeneza mkeka kisha baada ya dakika 90 unakuwa na shangwe mbili, ile ya ushindi na nyingine akaunti yako inavimba kwa mkwanja bila chenga.
Ipo wazi kwamba awali ligi ilitarajiwa kuwa ingerejea Machi Mosi na mechi za mwisho ilikuwa ni Desemba 29 2024 kuchezwa taarifa hiyo awali ilitolewa Desemba 31 2024 na TPLB.
Baada ya Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), kusogeza mbele fainali za CHAN kutoka Februari Mosi hadi Agosti 2025 imetoa nafasi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea na michezo ya NBC ambayo ilisimama kupisha fainali hizo.
Januari 15 2025 taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) ilitoa taarifa hiyo hivyo ile burudani ya msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja kwa mastaa kupambania pointi tatu inarejea.
RATIBA HII HAPA

Februari Mosi 2025 Yanga iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo itashuka KMC Complex kuwakaribisha Kagera Sugar iliyo nafasi ya 15 kwenye msimamo na pointi 11 baada ya kucheza mechi 15 ikiwa na wastani wa kukusanya pointi moja kwenye kila mchezo.
Inakutana na Yanga iliyo na pointi 39 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Kaitaba ubao ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga, mabao ya Maxi Nzengeli na Clement Mzize.
Februari 2 2025, Simba atashuka Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kumenyana na Tabora United. Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 40 kibindoni inakutana na Tabora United iliyo nafasi ya 5 na pointi 25.
Tabora United ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga na ilishinda mbele ya Azam FC kwa mabao 2-1 hivyo imekuwa na rekodi nzuri kwenye mechi zao dhidi ya vigogo ambao wapo ndani ya tatu bora licha ya mchezo wa mzunguko wa kwanza mbele ya Simba kupoteza Uwanja wa KMC, Complex.

Februari 5, Tabora United v Namungo, Baada ya kumalizana na Simba Tabora United itabaki hapohapo nyumbani kumalizana na Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda. Namungo ni nafasi ya 12 ikiwa na pointi 17.
Yanga v Ken Gold, Uwanja wa KMC, Complex. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Yanga ilikuwa ugenini Uwanja wa Sokoine, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Ken Gold 0-1 Yanga kwa bao la beki Bacca.
Dodoma Jiji v Pamba, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Dodoma Jiji ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 19 inakutana na Pamba iliyo nafasi ya 14 na pointi 12.
JANUARI ILIKUWA MWENDO WA 5 G

Januari haikuenda kinyonge kwa kuwa kuna mechi ambazo zilichezwa katika CRDB Federation Cup huku 5 G zikitembezwa ndani ya Uwanja wa KMC Complex.
Januari 25 2025 baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga 5-0 Copco ambapo kwenye mchezo huo beki Israel Mwenda aliandika rekodi ya kutoa pasi mbili za mabao kwenye mchezo huo ile ya kwanza alimpa Prince Dube ambaye alifunga bao lake la kwanza katika mashindano hayo akiwa na uzi wa Yanga.
Pasi ya pili alimpa kiungo wa kazi Mudathir Yahya ambaye alifunga bao la tano kukamilisha 5 G kwenye mchezo huo chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic na Yanga ni mabingwa watetezi wat aji.
Simba walifuata Januari 26 ilikuwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ukasoma Simba 6-0 Kilimanjaro Warriors ambapo beki David Kameta ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ushindani akiwa na uzi wa Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids alitoa pasi mbili za mabao.

