MudaMuda

YANGA licha ya kukwama kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya MC Alger Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 rekodi zinaonyesha kuwa umiliki asilimia kubwa ulikuwa upande wao kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kwenye mchezo wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya MC Alger walikuwa wanatakiwa kupata ushindi kuwa nafasi ya pili jambo ambalo limekwama baada ya ubao kusoma Yanga 0-0 MC Alger wakigawana pointi mojamoja.

REKODI ZA MCHEZO KWA MKAPA

Boka
Boka kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Jumla ya mashuti 18 Yanga walipiga kuelekea langoni mwa wapinzani wao MC Alger huku matatu yakilenga lango katika mchezo wa leo ambao wapinzani wao walikuja kwa mpango kazi wa kujilinda zaidi.

MC Alger rekodi zinaonyesha kuwa ni mashuti matatu pekee walipiga kuelekea langoni huku shuti moja pekee likilenga lango kwenye mchezo huo.

Yanga ilipata jumla ya kona 14 kwenye mchezo na MC Alger ni kona moja pekee walipata ikiwa inamaanisha kwamba Yanga walikuwa wakishambulia zaidi kwenye lango la wapinzani katika msako wa ushindi.

Nyota watatu wa MC Alger walionyeshwa kadi za njano huku Yanga wakiwa salama ndani ya dakika 90 na hakuna kadi nyekundu iliyoonyeshwa kwenye mchezo.

AL HILAL WAPOTEZA KIMATAIFA

TP Mazembe 4-0 Al Hilal ambapo mabao ya TP Mazembe yamefungwa na Diof dakika ya 22, Keita dakika ya 29, Vundi dakika 58 na Shaiu dakika ya 89 kwa mkwaju wa penalti.

HUU HAPA MSIMAMO KUNDI A

Aziz Stephan
Aziz Stephan kwenye anga la kimataifa ni mabao mawili amefunga hatua ya makundi 2024/25. Source: Yanga.

Al Hilal nafasi ya kwanza na pointi zao ni 10

MC Alger nafasi ya pili pointi 9. Timu hizi mbili zimefuzu hatua yar obo fainali, Al Hilal na MC Alger huku Yanga na TP Mazembe zikikwama.

Yanga kutoka Tanzania nafasi ya tatu na pointi 8

TP Mazembe nafasi ya nne pointi zao ni 5

KIKOSI CHA YANGA KILICHOANZA

Dube
Dube Prince, mshambuliaji wa Yanga kwenye mchezo wa kimataifa.Source: Yanga.

Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Ladack Boka, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Clement Mzize, Mudathir Yahya, Prince Dube, Aziz Ki, Kennedy Musonda.

Wachezaji wa akiba ni Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Bakari Nondo, Duke Abuya, Sure Boy, Farid Mussa, Shekhan, Clatous Chama na Pacome.

Katika dakika 45 za mwanzo kwa Yanga walikuwa wakipambana kusaka ushindi wakimtumia Clement Mzize ambaye alikuwa akishirikiana na Prince Dube kwenye eneo la ushambuliaji.

Nyota wa Yanga Pacome aliingia kipindi cha pili dakika ya 45 akichukua nafasi ya Kennedy Musonda ambaye alikuwa kwenye eneo la ushambuliaji katika kusaka ushindi ndani ya Uwanja wa Mkapa.

Kiungo Clatous Chama aliingia kipindi cha pili dakika ya 67 akichukua nafasi ya Mudathir Yahya ambapo Chama alifanya jaribio dakika ya 74 lilikwenda nje ya lango kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Kipa wa MC Alger alionyeshwa kadi ya njano kipindi cha pili kutokana na mwamuzi kutafsiri kuwa alikuwa anapoteza mud ani dakika ya 75 Ramdane alionyeshwa kadi ya njano katika mchezo huo uliokuwa ukifuatiliwa na mashabiki wengi duniani.

Dube
PRINCE Dube akiwa kwenye majukumu yake kimataifa, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Kwenye mchezo wa leo kipindi cha pili ziliongezwa dakika 7 kusaka mshindi ndani ya uwanja kutokana na wapinzani wa Yanga, MC Alger kuwa kwenye upotevu wa muda mara kwa mara ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili.

Yanga walikuwa wakipiga konakupitia kwa viungo wao wawili amba oni Pacome na Aziz Ki hawa walikuwa na kazi kwenye kupiga mapigo ya kona katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

TP MAZEMBE WALIWAKA NYUMBANI

TP Mazembe wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi waliwaka dhidi ya Al Hilal ambao ni vinara wa kundi A na mchezo wao uliopita Al Hilal walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Bao la Aziz Ki ugenini lilifungwa dakika ya 7 wakiibuka na ushindi mbele ya Al Hilal ikiwa timu ya kwanza kupata ushindi dhidi ya Al Hilal ambao dakika 45 kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe baada ya dakika 90 imekuwa TP Mazembe 4-0 Al Hilal kikiwa ni kipigo kikubwa kwa Al Hilal kupata ugenini katika hatua ya makundi.

Kwenye mchezo huo mabao ya TP Mazembe yamefungwa na Diof dakika ya 22, Keita dakika ya 29, Vundi dakika 58 na Shaiu dakika ya 89 kwa mkwaju wa penalti.

Share this: