Wawakilishi wa Tanzania kimataifa Yanga leo Jumamosi wataisimamisha nchi pale watakaposhuka uwanjani kuvaana na MC Alger ya Algeria katika mchezo mkubwa ambao umebeba tiketi ya timu mojawapo kati ya hizo kutinga Robo Fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Ikumbukwe Yanga ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia katika mashindano hayo makubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika. Huku wawakilishi wengine wa Tanzania kimataifa wakiwa ni Simba ambao wanashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo wao watashuka uwanjani kesho Jumapili kuvaana na CS Constantine.
Kumbuka unaweza kujishindia pesa nyingi na kupata utajiri leo kwa kubashiri matokeo ya mchezo huu na mingine mingi kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa yenye odds kubwa kwa kutembelea http://www.sportpesa.co.tz
YANGA KULIPA KISASI KWA WAARABU?

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga leo watashuka uwanjani kuvaana na MC Alger ambapo Yanga wanahitaji sana matokeo ya ushindi wowote katika mchezo wa leo ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya Robo Fainali katika mchezo ambao unatafsiriwa kuwa ni mchezo mgumu na wa kisasi kwani Yanga walikubali kipigo katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Algeria ambapo ubao ulisoma 2-0.
Yanga inayodhaminiwa na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwenye mchezo wake uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika ilivuna pointi tatu ikiwa ugenini baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vinara wa kundi lao Al Hilal ambao tayari wamefuzu kucheza nusu fainali.
Ikumbukwe kwamba kwenye kundi A mpaka sasa Yanga ipo nafasi ya tatu wakiwa wamevuna pointi saba katika michezo yao mitano waliyocheza na wanakwenda kukutana na MC Alger ambao wanakamatia nafasi ya pili na pointi zao nane katika idadi hiyo ya michezo mitano waliyocheza.
YANGA WANASEMAJE?

Kocha mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya MC Alger utakuwa mgumu, lakini wapo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu kutokana na umuhimu wa mchezo huo kwa Yanga.
“Tunauendea mchezo huu tukiwa na imani kwamba tutapata pointi tatu muhimu, tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi lakini tupo tayari na wachezaji wanajua kwamba huu ni mchezo muhimu kwetu kutafuta pointi tatu, kikubwa ni utayari na mchezo, ipo wazi kwamba walipata ushindi kwenye mchezo wetu uliopita, tutapambana kupata matokeo mazuri.
“Tunajua umuhimu wa mchezo unaokuja, sio kwetu tu tunajua hata wapinzani wetu wanajua wanahitaji nini, nina matumaini makubwa kutokana na namna wachezaji wangu wanajitoa na kuelewa mfumo wangu, tunakwenda kujitoa kwa kila iwezekanavyo. Tunakwenda kulipuka kama moto kuhakikisha tunaweka utawala katika mchezo huo.
“Hatujawahi kwenda kucheza mchezo kwa ajili ya droo sisi lengo letu namba moja ni ushindi, sina haja ya kuongelea kuhusu matokeo mengine zaidi ya ushindi, nina wachezaji ambao wanaweza kubadilika kutokana na mbinu zangu au kutokana na mfumo wa wapinzani, sina mashaka na mbinu zangu kwenye kupata matokeo ya ushindi hapo kesho.
“Maxi ni mchezaji wa maajabu, lakini bado hajawa sawa kucheza, Chama amerejea pia sina haraka nae kwa sababu tayari nina wachezaji 24 ambao wanaweza kutupatia matokeo, sina sababu ya kulazimisha wachezaji ambao bado hawapo fiti kucheza. Tutaangalia mwenendo wa kila mchezaji kimwili na kiakili kabla ya kufanya maamuzi
“Naomba niweke wazi, utakuwa ni mchezo mgumu sana, utakuwa mchezo ambao utakuwa na matumizi makubwa ya nguvu, ni mchezo wenye presha kubwa lakini naamini vijana wangu wanaweza kuhimili mikikimikiki hiyo. tunakwenda kuwasha moto kutoka dakika ya kwanza mpaka filimbi ya mwisho,” Sead Ramovic
Ali Kamwe

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa maandalizi yapo vizuri kuelekea mchezo huo: “Maandalizi yetu ni mazuri na kuna wachezaji ambao huenda hawatakuwa sehemu ya kikosi kama kocha alivyosema kwa kuwa bado hawajawa fiti, lakini pia wapo ambao wamerejea na tunaweza kuwatumia, tunakwenda kwa kujiamini kuwa tuna nafasi na inawezekana.”
SPORTPESA INAWATAKIA KILA LA KHERI YANGA

