Abuya DukeAbuya Duke

MWENDELEZO wa kucheza mechi bila kufungwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa Singida Black Stars ya Singida uligota mwisho Oktoba 30 2024 baada ya Yanga kutibua rekodi hiyo ndani ya uwanja. Timu ya Singida Black Stars ni mechi 8 ambazo ni dakika 720 ilicheza bila kupoteza.

Kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho huku dakika 45 mwamuzi Ally Mnyupe akionyesha jumla ya kadi 8 za njano, Yanga ilisepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo huo.

Pacome v Singida
Pacome kiungo wa Yanga kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Singida Black Stars Oktoba 30 2024. Sourc: Yanga.

Ni bao la Pacome liliipa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa pointi tatu ikitibua rekodi ya Singida Black Stars iliyocheza mechi 8 bila kupoteza huku Yanga ikifikisha mchezo wa 8 na pointi 24 bila kupoteza ndani ya ligi.

Hapa tunakuletea baadhi ya rekodi walizoandika wachezaji wa timu zote mbili ndani ya uwanja wa New Amaan namna hii:-

METACHA MNATA

Alianza kikosi cha kwanza akikomba dakika 90 alifungwa bao moja dakika ya 67 na Pacome, aliokoa hatari dakika ya 18, 34, 36, 37, 43, 61, 64, 66 alipiga pasi fupi dakika ya 19, pasi ndefu ilikuwa dakika ya 44, 45, 46, 55.

ANDE KOFFI

Alicheza faulo dakika ya 3 kwa Boka, 22, 51, aliokoa hatari dakika ya 45, 64 alichezewa faulo dakika ya 48.

IBRAHIM IMORO

Mwamba huyu hapa alianza kikosi cha kwanza alicheza faulo dakika ya 17, dakika ya 22 alionyeshwa kadi ya njano.

KENNEDY JUMA

Juma Kened
Kenedy Juma beki wa Singida Black Stars. Source: Singida Black Stars.

Nahodha wa Singida Black Stars alianza kikosi cha kwanza na aliokoa hatari ikiwa ni dakika ya 28, 55.

ANTHONY URBAN

Alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 12, 13, 13, 19 alicheza faulo dakika ya 49.

IDD HABIB

Mwamba huyu aliokoa hatari dakika ya 16, 43, alichezewa faulo dakika ya 59.

ISRAEL MWENDA

Beki wa kupanda na kushuka Israel Mwenda alianza kikosi cha kwanza na aliokoa hatari dakika ya 16, alichezewa faulo dakika ya 34, 56.

MAROUF TCHAKEI

Jezi namba 10 mgongoni ni dakika ya 30 alicheza faulo 37, 75 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 37.

ELVIS RUPIA

Alicheza faulo dakika ya 41, 44, 45 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 42.

 

HAWA HAPA YANGA

DJIGUI DIARRA

Alipiga pasi ndefu dakika ya 13, 36, 45, 64, 88 alipewa majukumu ya kupiga faulo dakika ya 22, 87 alipiga pasi fupi dakika ya 30, 40, 62, 83, 90 aliokoa hatari dakika ya 78, 90, 90.

DENNIS NKANE

Alikuwa kwenye upande wa kushoto nyota huyu ambaye alipenya kikosi cha kwanza, alichezewa faulo dakika ya 18, 41.

BOKA

Alikomba dakika 10 baada ya kupata maumivu kwenye mchezo huo nafasi yake ni Nikson Kibabage aliingia ambaye huyu alipga shuti lililolenga lango dakika ya 34, alicheza faulo dakika ya 78 alikwama kusepa na dakika zote alipata maumivu na dakika ya 84 alitoka nafasi yake ni Bacca aliingia.

NONDO

Bakari Nondo nahodha wa Yanga alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 45, 89 alicheza faulo dakika ya 48.

JOB

Job v Singida
Job beki wa Yanga kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars, Oktoba 30 2024. Source: Yanga.

Dick Job beki wa kazi alikomba dakika 90 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 39, alicheza faulo dakika ya 45 aliokoa hatari dakika ya 15, 26, 28, 37, 43, 57, 89.

KHALID AUCHO

Aucho Khalid ni dakika ya 12 alichezewa faulo, dakika ya 21, 26 alicheza faulo na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 26.

AZIZ KI

Aziz Ki
Kiungo wa Yanga Aziz Ki akiwa kwenye majukumu ndani ya uwanja. Source: Yanga.

Aziz Ki alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 31, 53 shuti ambalo lililenga lango ilikuwa dakika ya 61, alicheza faulo dakika ya 47, alichezewa faulo dakika ya 15, 24, 49, 50.

DUKE ABUYA

Duke Abuya alicheza faulo dakika ya 14, 29 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 43.

PRINCE DUBE

Prince Dube alianza kikosi cha kwanza ambapo alicheza faulo dakika ya 22, 59, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 22, alichezewa faulo dakika ya 10, 56 jaribio lake la dakika ya 13 lilikutana na kizingiti cha mabeki ndani ya 18 alikomba dakika 68 nafasi yake ni Clement Mzize aliingia.

CHAMA

Clatous Chama alipiga faulo dakika ya 18,52, alipewa jukumu la kupiga kona dakika ya 61, 64, 66, 84 kwa Yanga.

PACOME

Pacome kiungo wa kazi alifunga bao la ushindi kwa Yanga dakika ya 67 akiwa nje ya 18, alichezewa faulo dakika ya 22, 34, 75 alicheza faulo dakika ya 58.

Share this: