
Ni ‘super Sunday’ ndivyo unavyoweza kusema kwani huku ukiwa umejipumzisha kujiandaa na wiki ya kwanza ya mwezi Septemba, leo Jumapili kunatarajiwa kuwaka kwenye Uwanja wa Old Trafford kwenye EPL jijini Manchester.
Hii ni pale wenyeji Manchester United watakaposhuka uwanjani kuvaana na mahasimu wao, Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu England yaani EPL ambao unatarajiwa kupigwa kuanzia majira ya saa 12:00 jioni.
Unaweza kushinda mamilioni kwenye mchezo huu kupitia ubashiri wako ukiweka kupitia kampuni bora ya michezo ya kubashiri hapa nchini ya SportPesa kwa kubonyeza link hii www.sportpesa.co.tz
NI VITA YA WAHOLANZI

Mchezo huu unatazamwa kama vita ya Waholanzi kwani unawakutanisha makocha wawili kutoka nchini Uholanzi Erik ten Hag vs Arne Slot.
Makocha hao wamekuwa na historia kubwa ya ushindanio tangu wakiwa kwao nchini Uholanzi na alipoulizwa kuhusu hilo, alisema: “Ni jambo kubwa kwa soka letu na heshima, kupata makocha wawili kutoka taifa moja kufundisha timu hizi mbili zenye historian a heshima kubwa.”
Imekuwa ngumu kwa makocha wengi waliotokea Ligi Kuu ya Uholanzi kupata mafanikio makubwa katika ardhi ya Uingereza, lakini Ten Hag tayari amefanikiwa kuiongoza Man United kwenye michezo 117 na kufanikiwa kushinda makombe mawili katika misimu yake miwili ya kwanza japo kumekuwa na mashaka juu ya kibarua chake hasa kama atapoteza mchezo wa leo.
HAKUNA MBABE
Mpaka sasa kati ya wawili hao kunaonekana hakuna mbabe, kwani katika michezo minne ambayo walikutana kwenye vipindi tofauti ndani ya Ligi Kuu Uholanzi, kila mmoja amefanikiwa kushinda michezo miwili, hivyo swali kubwa kuelekea mchezo huu linabaki kuwa ni nani ataandika rekodi ya ubabe kati yao kwa kuibuka na ushindi?
UZOEFU WA EPL WAMBEBA TEN HAG

Licha ya muonekano wao ambao unakaribia kufanana hususani kwa mtindo wa kuondoa nywele za kichwani ‘upara’, lakini makocha hao wanaonekana kuwa na vitu vingi tofauti.
Ishu ya uzoefu wa ligi inambeba zaidi Ten Hag kulinganisha na mpinzani wake. Kwa upande wa, Slot yeye anajulikana zaidi kwa ubora wa kuzungumza na vyombo vya habari.
MTIHANI MWINGINE KWA SLOT
Ni wazi kuwa, Slot ni lazima anapaswa kuhakikisha anafanikiwa hasa kutokana na historia ya mtangulizi wake Jurgen Klopp.
Wachambuzi wengi wanaamini, Slots ataendeleza utamaduni wa timu kukaba kwa nguvu ‘pressing’ kwenye kila eneo la uwanja hasa kutokana na namna ambavyo timu alizofundisha zimekuwa zikicheza.
LIVERPOOL NA MATUMIZI YA WALINZI WA PEMBENI
Gwiji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher aliutazama mchezo wao uliopita dhidi ya Ipswich na kufichua yafuatayo: “Nadhani kuna mahali kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi na muundo wa uchezaji hasa wakati timu haina mpira.
“Nadhani atajaribu zaidi kufanya umiliki wakati watakapokuwa na mpira na kufanya mashambulizi ya kushtukiza. Huu umekuwa utaratibu wa timu nyingi za EPL na unaona hata Manchester City wamekuwa bora kwenye eneo hili.”
Slot anajulikana zaidi kwa kutumia kiungo mmoja tu, wa asili wa ukabaji ambaye anasaidiana na kiungo mmoja ‘box to box’, lakini mfumo huu una changamoto kubwa England kwani timu nyingi hulazimika kutumia viungo wawili wa ukabaji wa asili.
TEN HAG AFUNGUKA
Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Man United, Erick Ten Hag amekiri kuwa wanatarajia upinzani mkubwa kutokana na ubora wa wapinzani wake.
Kauli hizo za kumsifu, Slot zimetafsiriwa na wengi kama hofu ambayo anayo kocha huyo wa Manchester United kuelekea mchezo huu muhimu, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema huenda zikawa ni kauli ambazo zinaweza kumletea shida, Ten Hag hasa katika kipindi hiki ambacho kibarua chake kiko mashakani.
KILA MTU NA MTIHANI WAKE

Kwa Ten Hag na Manchester United yake hii inatarajiwa kuwa nafasi ya kuangalia uborekaji wa kikosi chake, hasa katika msimu huu wa tatu kwake tangu akabidhiwe majukumu ya kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.
Kwa Slot yeye atapata nafasi ya kuona ikiwa ni changamoto gani anazoweza kukutana nazo kwenye Ligi Kuu England mara baada ya kutoka Uholanzi.
