Nzengeli YangaNzengeli Yanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga wamefungua pazia la ligi kwa kuanza na ushindi mbele ya wapinzani wao Kagera Sugar huku benchi la ufundi likibainisha kuwa kuna tatizo la kumalizia nafasi ambalo litafanyia kwazi kwenye mechi zijazo za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni mara 36 sawa na dakika 3,240 imekutana na Kagera Sugar ikipata ushindi mara 27 ikipeta ndani ya dakika 2,430, sare ilikuwa mara 3 ikipoteza kwenye mechi 6. Upande wa safu ya ushambuliaji ni mabao 61 ilifunga na kufungwa mabao 28 kwenye mechi za ushindani.

Ki na Nzengeli
Aziz Ki na Maxi Nzengeli wachezaji wa Yanga kwenye moja ya mchezo wa ushindani. Source: Yanga.

Kete ya kwanza ndani ya msimu wa 2024/25 ilikuwa Uwanja wa Kaitaba, Agosti 29 2024 ubao uliposoma Kagera Sugar 0-2 Yanga kwa kazi ya Maxi Nzengeli aliyepachika bao la kuongoza dakika ya 25, Clement Mzize dakika ya 88 likiwa ni bao la jioni kwenye mchezo huo.

Una nafasi ya kuweka mikeka kwenye mechi zinazochezwa kwa kutembelea SportPesa.

HUYU HAPA KOCHA MIGUEL GAMONDI

Gamondi
Gamondi Miguel, Kocha Mkuu wa Yanga. Source: Yanga.

Kocha Mkuu Gamondi amebainisha kuwa walipata nafasi nyingi ndani ya uwanja lakini hazikutumika hivyo tatizo hilo wanakwenda kulifanyia kazi kuwa imara kwenye mechi zijazo ikiwa ni pamoja na mchezo wa  Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya  CBE ya Ethiopia.

“Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa dhidi ya wapinzani wetu na tuliona kwamba kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi zaidi ya sita lakini tukapata bao moja na ilikuwa hivyo kipindi cha pili tulitengeneza nafasi tatu tukatumia moja

“Kwa kilichotokea sio mbaya kwa hili lililotokea kikubwa ni pointi tatu na makosa haya tunakwenda kufanyia kazi eneo la mazoezi. Kikubwa tumepata pointi tatu muhimu tutafanyia kazi makosa yetu kuwa imara.

“Kuna mchezo wa Ligi ya Mabingwa utakuwa mgumu kwetu hasa ukizingatia kwamba kuna wachezaji ambao watakuwa kwenye timu ya taifa na watarejea muda mfupi, kuna kazi kubwa ambayo tunakwenda kufanya nina amini tutafanya maandalizi mazuri kwa muda ambao tutaupata.”

FOUNTAIN GATE YAPETA UGENINI

 

Fountain Gate v Simba
Mchezo wa kwanza kwa Fountain Gate ilikuwa dhidi ya Simba, Uwanja wa KMC,Mwenge. Source: Simba.

Fountain Gate inayodhaminiwa na SportPesa imepeta ugenini kwa kupata ushindi mchezo wake wa kwanza ikiwa ilitoka kupoteza mbele ya Simba inayofundishwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Agosti 29 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-2 Fountain Gate huku Namungo wakikosa penalti dakika ya 25 kwenye mchezo huo ambayo waliipata kutokana na beki wa Fountain Gate kudaiwa kucheza faulo ndani ya 18.

Ni Edger William wa Fountain Gate alifungua pazi la kufunga ndani ya kikosi hicho ilikuwa dakika ya 30 na bao la pili lilifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 45 hivyo kazi iligotea hapo kwa mabao hayo kudumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ikumbukwe kwamba Fountain Gate mchezo wa kwanza msimu wa 2024/25 ilikuwa Simba 4-0 Fountain  Gate ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

SEMAJI LA FOUNTAIN GATE HILI HAPA

Liponda
Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate. Source: Fountain Gate.

Issa Liponda, Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema kuwa wamejitafuta na kujipata hivyo hawana tatizo na timu yoyote ile wakiomba kurudiana na timu iliyowafunga ya Ubaya Ubwela ambayo ni Simba.

“Tumejitafuta na sasa tumejipata, tunaomba kurudiana na ile timu ya ubaya ubwela, hakika tunawakada nyingi hatuna mashaka tuna wachezaji weye uwezo na wanajituma.”

Namungo inayofundishwa na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ni mchezo wake wa pili mfululizo inapoteza ikiwa nyumbani kwa kuwa mchezo wa kwanza ilipoteza mbele ya Tabora United kwa kufungwa mabao 2-1 ikiwa Uwanja wa Majaliwa.

Zahera ameweka wazi kuwa kuna makosa ambayo yanatokea hayo yatafanyiwa kazi ili timu kupata matokeo kwenye mechi za ushindani ambazo wanacheza.

KMC COMPLEX NGOMA NZITO

Wamiliki wa Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, KMC mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi ndani ya Ligi Kuu Bara 2024/25 ngoma ilikuwa ni nzito kwa kutoshana nguvu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa baada ya dakika 90 ubao ulisoma KMC 1-1 Coastal Union hivyo waligawana pointi mojamoja wababe hao wawili.

Bao la KMC lilipachikwa na Ibrahim Elias dakika ya 32 na bao la kuweka usawa kwa Coastal Union ambayo ilikuwa inapaperusha bendera ya Tanzania kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho na kugotea hatua ya awali lilifungwa na Maabad Maulid dakika ya 85 kwa mkwaju wa penalti.

 

 

 

Share this: