Aucho v FeiAucho v Fei

MABINGWA mara 30 ndani ya Ligi Kuu Bara wamebainisha kwamba kazi kubwa wataifanya msimu wa 2024/25 kufikia malengo yao katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa kutokana na uimara wa kikosi walicho nacho, benchi bora la ufundi na uzoefu.

Pamba
TIMU ya Pamba ilifungua pazi la ligi kwa kutoshana nguvu na Tanzania Prisons 2024/25 mchezo ulichezwa Agosti 16. Source: Pamba.

Tayari ligi zimerejea hivyo unaweza kubashiri na kuweka mkeka wako kupitia SportPesa ukavuna mkwanja wako haraka na bila longolongo muda huu bofya link na ucheze sasa.

Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni mabingwa watetezi wa ligi msimu wa 2024/25 baada ya kutwaa taji hilo msimu wa 2023/24. Baada ya mechi 30 walikomba pointi 80 watapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na Yanga kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Azam FC nao wanaipeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na watafungua code Uwanja wa Azam FC kwenye mchezo dhidi ya APR itakuwa ni Agosti 18 na Coastal Union ya Tanga hii ilimaliza nafasi ya nne inaingia kwenye orodha ya zitakazokomba dakika 90 kusaka ushindi kimataifa.

MABINGWA KWENYE KAZI

 

AZIZ NA MAX
MAXI Nzengeli na Aziz Ki wachezaji wa mabingwa watetezi wa ligi. Source: Yanga.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi watakuwa na kazi Agosti 17 Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Vital’O ya Burundi ambapo ni mchezo wa hatua ya awali. Kikubwa ambacho kinataufutwa ni ushindi wa jumla kwenye mechi mbili ile ya nyumbani na ugenini hivyo kazi kubwa kwa Yanga ni kusaka ushindi kwenye mechi zote mbili kama ilivyo kwa wapinzani wao.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo na tambo za wapinzani wao wamesikia hivyo wanakwenda kufanya kazi kwa vitendo uwanjani kwa kuwa ni mchezo muhimu na wanatambua umuhimu wa kupata ushindi.

Ndani ya Yanga kuna wachezaji ambao wanafuatiliwa kwa ukaribu na wapinzani wao ikiwa ni Aziz Ki, Maxi Nzengeli, Pacome, Djigui Diarra, Duke Abuya hawa wote ni chaguo la kwanza katika kikosi hicho anga la kimataifa.

Kamwe kuhusu mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika amesema: “Hatuna jambo dogo sisi na tunatambua ni mchezo muhimu kwa kila mmoja kupata ushindi lakini kwa kile ambacho wamekipanda watavuna uwanjani, tukutane Azam Complex mashabiki tuishangilie timu yetu kwenye mchezo huu mkubwa.

“Wachezaji wanatambua kwamba mashabiki furaha yao ni kuona kwamba tunashinda hilo lipo kwenye uwezo wao na burudani itatolewa uwanjani. Wachezaji wote wapo vizuri na wapo tayari kupambana kwa ajili ya kupata matokeo.”

MWALIMU WA MABINGWA NENO LAKE

 

Yanga Ngao
MABINGWA wa Ngao Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi. Source: Yanga.

Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kwamba benchi la ufundi lipo tayari na hesabu kubwa ni kupata matokeo kwenye mchezo wao kufikia malengo ya kusonga mbele kimataifa. Gamondi alikiongoza kikosi hicho kutwaa taji ya Ngao ya Jamii 2024/25.

“Kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi na hilo linawezekana kwani wachezaji wanajituma na wanastahili pongezi kwa kuwa kila mchezo ni mgumu na ushindani ni mkubwa kweli.”

RAIS WA MABINGWA HUYU HAPA

Injinia Hersi SaiId rais wa klabu ya Yanga kwenye mahojiano yake na BBC Swahili ameweka wazi kuwa Yanga wanahitaji ubingwa wa Afrika na hilo linawezekana kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uzoefu na mipango imara.

“Dhana yetu Yanga kila mashindano ambayo tunashiriki tunataka kubeba makombe hivyo kwenye ligi kuu bara na katika Ligi ya Mabingwa Afrika tukiweka mguu Jumamosi malengo yetu ni kuona kwamba tunabeba kombe la Afrika.”

AZAM FC NA CODE

FEI Azam
Kiungo wa Azam FC Feisal Salum. Source: Azam FC.

Matajiri wa Dar Azam FC wamebainisha kuwa tayari wamepata code hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi Jumapili kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR.

Mkuu wa kitengo cha Idara ya Habari na Mawasiliano Azam FC, Zakaria Thabit amebainisha kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo mkubwa na wanatambua kwamba utakuwa na ushindani mkubwa hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashangilia bila kuchoka.

Thabit amebainisha kuwa mashabiki wote wa soka Tanzania iwe ni pamoja na wale wa Simba ni muda wa kuwa bega kwa bega katika hili kwa kujitokeza kuishangilia timu hiyo Uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

COASTAL UNION KIMATAIFA

Wagosi wa Kaya, Coastal Union nao pia kutoka Tanzania jioni saa 12 watakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye Kombe la Shirikisho dhidi ya FC Bravos.

Share this: