
Staa mpya wa Real Madrid, Kylian Mbappe kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha yake mapya ndani ya Real Madrid baada ya kufdanikiwa kuiongoza timu hiyo kushinda ubingwa wa UEFA Super Cup dhidi ya Atalanta.
Akicheza mchezo wake wa kwanza ndani ya jezi ya Real Madrid aliyojiunga nayo msimu huu akitokea klabu ya PSG ya Ufaransa, ilimchukua dakika 68 tu, kufungua akaunti yake ya mabao baada ya kutumia vizuri asisti ya kiungo, Jude Bellinham.
Mbappe kwa sasa amekabidhiwa jezi namba 9 aliyokuwa akiivaa, Mfaransa mwenzake aliyekuwa nahodha wa Real Madrid, Karim Benzema.
Staa huyo amejiunga na Madrid kama mchezaji huru baada ya kumaliza makataba wake na kuachana na PSG ambayo aliitumikia kwa kipindi cha miaka saba.
Bao hilo la Mbappe lililuwa bao la pili katika mchezo huo baada ya bao la kwanza ambalo lilifungwa na kiungo, Federico Valverde’s aliyetumia asisti nzuri ya Mbrazil, Vinicious Jr huku mchezo huo ukiisha kwa ushindi wa mabao 2-0. Ikumbukwe Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa iliweka odds za maana watu kupiga pesa kwenye mchezo huu.
Katika mchezo hulo staa huyo alianza kjatika kikosi cha kwanza cha Real Madrid chini ya kocha, Carlo Ancelotti baada ya kuwa na wakati mzuri katika program za mazoezi.
URAFIKI NA BELLINHAM
Tangu ajiunge na Madrid Mfaransa huyo ameonekana kuwa na wakati mzuri na mahusiano mazuri na kiungo wa kimataifa wa England, Jude Bellinham ambaye ndiye alimpasia asisti ya bao hilo.
Kwa muda mchache tangu ajiunge na kikosi cha timu hiyo, Mbappe ameonekana kuwa kipenzi cha mashabiki ambao pia walijitokeza kuujaza uwanja wakati akitambulishwa rasmi kuwa staa wa Madrid.
REAL MADRID WAANDIKA REKODI MPYA

Kwa kutwaa ubingwa huo, Madrid imeandika historia mpya ya kuwa timu ya kwanza kuweza kushinda ubingwa wa mashindano ya UEFA Super Cup mara sita.
MBAPPE AWAONYA WAPINZANI KUWA ATAFUNGA SANA
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Mfaransa huyo aliweka wazi kuwa hajaweka malengo yoyote juu ya mabao mangapi ambayo atafunga msimu huu, lakini akaweka wazi kuwa atafunga bila kikomo.
“Unapokuwa sehemu ya Real Madrid ni lazima ufahamu kuwa hapa hakuna ukomo, kuhusu naweza kufunga mabao mangapi msimu huu naweza kusema hakuna ukomo.”
Alipoulizwa ikiwa anaweza kufunga mabao 50 alijibu: “Kama naweza kufunga mabao 50 ni 50 lakini jambo la msingi ni kushinda na kuendelea kuboresha kama timu. Umekuwa usiku bora kwangu, naweza kusema nilikuwa nikisubiri wasaa huu kwa kipindi kirefu.
“Kucheza ndani ya jezi ya timu hii, kuwakilisha nembo ya Madrid mbele ya mashabiki wake ni jambo kubwa sana kwangu. Kushinda makombe ndio jambo muhimu zaidi kwetu na kufunga goli katika mchezo wangu wa kwanza ni hisia ambazo siwezi kuzielezea.”
KOCHA CARLO ANCELOTTI ATOA NENO

“Ni mchezaji ambaye ana ubora mkubwa wa kufunga mabao mengi lakini tunajua kuwa tuna kazi kubwa ya kufanya ya kuhakikisha tunatafuta na kutunza uwiano wa kikosi chetu.
“Kwenye mchezo dhidi ya Atalanta tulionyesha hilo, kipindi cha kwanza hatukuwa bora sana kama tulivyotarajia, lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa bora sana licha ya kwamba Atalanta ‘walitupress’ sana.
“Kipindi cha pili tuliwafungua zaidi na kutengeneza nafasi mbele na ni wazi tukiwa na nafasi tuna, Rodrygo, Vinicius na Mbappe ambao ni hatari sana wakiwa na nafasi.
FERDINAND AKUBALI BALAA LA BELLINGHAM

Mchambuzi wa soka na mlinzi wa zamani wa Manchester United na England, Rio Ferdinand ameonyesha kuvutiwa zaidi na ubora wa Jude Bellingham.
Bellingham alionyesha kiwango bora katika mchezo huo na kufanikiwa kutajwa kuwa mchezaji bora wa mchezo akihusika moja kwa moja na bao la pili kwa kupika bao hilo.
Akizungumza na kituo cha michezo cha TNT, Ferdinand amesema: “Jude Bellingham ni mchezaji wa tofauti sana, alikuwa kwenye kiwango bora sana kwenye mchezo huu, na uhusika muhimu wa matokeo ya ushindi.
“Aliweza kyuandikisha asilimia 90 ya pasi zote ambazo alipiga na kufika kwa walengwa na kushinda uporaji ‘tackling’ wote wa mipira kwa asilimia 100.”

