BURUDANI INAREJEA, RATIBA YA LIGI HII HAPA AGOSTI 16 2024 KITAWAKA

ByLunyamadizo Mlyuka

August 15, 2024
Kibabage v RedKibabage v RedKibabage v Red

BURUDANI inarejea upya baada ya maandalizi kwa msimu wa 2024/25 kufanyika ikiwa ni usajili na utambulisho kwa wachezaji wapya, uzi mpya ndani ya timu Bongo ligi ilipogota mwisho msimu wa 2023/24.

Usisahau kwamba mechi zote za ufunguzi ikiwa ni Pamba dhidi ya Tanzania Prisons ukibasiri kupitia SportPesa unakunja mkwaja wako mapema kabisa na ni rahisi sana.

Pamba
BURUDANI ndani ya ligi itafunguliwa Mwanza kwa Pamba kuwakaribisha Prisons. Source: Pamba.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ilitwaa taji la ligi na ilimaliza ikiwa na pointi 80 kibindoni baada ya kucheza jumla ya mechi 30. Kazi inakwenda kuanza upya msimu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Kwenye Wiki ya Mwananchi Yanga ilicheza dhidi ya Red Arrows huku Simba ikicheza na APR Simba Day wababe hawa wote wawili walitumia Uwanja wa Mkapa.

HAPA RATIBA YA BURUDANI ZA LIGI

Pamba Jiji iliyopanda daraja itafungua pazia kwa mchezo utakaochezwa Agosti 16 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Agosti 17 itakuwa Mashujaa v Dodoma Jiji Uwanja wa Lake Tanganyika na Namungo wataikaribisha Fountain Gate Uwanja wa Majaliwa.

Simba itatumia Uwanja wa KMC itamenyana na Tabora United, Ken Gold itakuwa uwanjani kusaka ushindi dhidi ya Sigida Black Stars, Uwanja wa Sokoine Mbeya zote hizi zinatarajiwa kuchezwa Agosti 18 2024.

MABINGWA KAZINI

MABINGWA
Mabingwa wa ligi na Ngao ya Jamii Yanga burudani yao wataanza kimataifa ugenini. Source: Yanga.

Mabingwa mara 30 Yanga watakuwa kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Agosti 17 watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Vital O ya Burundi. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Yanga iligotea hatua ya robo fainali katika ligi ya mabingwa Afrika na msimu wa 2024/25 hesabu kubwa ni kuanza kutinga hatua ya makundi kisha kutinga robo fainali kwa mara nyingine tena.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe aliweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kupanda hatua kwa hatua kwenye mechi ambazo watacheza hatua ya kimataifa kufikia malengo ambayo yapo kwenye timu hiyo.

“Tunaanza hatua kwa hatua kama ambavyo msimu uliopita tulitinga hatua ya robo fainali haikuwa ghafla, kwa kuwa tupo hatua ya awali tunakwenda kuanza kutafuta ushindi kutinga kwenye hatua ya makundi kisha hatua nyingine itafuata kila kitu nina amini kitakuwa sawa.”

Katika Ligi Kuu Bara, Yanga itaanza ugenini na mchezo wa kwanza Miguel Gamondi anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kukabiliana na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba Agosti 29 2024.

SIMBA KUANZA NYUMBANI KUTOA BURUDANI

Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kete ya kwanza kwenye ligi watakuwa nyumbani dhidi ya Tabora United katika kutoa burudani ndani ya dakika 90. Mchezo wa mzunguko wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu.

Ipo wazi kwamba msimu wa 2023/24 Simba mchezo wa kwanza ilikuwa ugenini ambapo ilicheza dhidi ya Mtibwa Sugar. Baada ya dakika 90 mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Manungu ubao ulisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba.

Katika mchezo huo mlinda mlango alikuwa ni Ally Salim kwa upande wa Simba alitunguliwa mabao mawili ndani ya dakika mbili kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa licha ya Simba kukomba pointi tatu ugenini.

Ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu pointi 69 baada ya kucheza mechi 30 inakutana na Tabora United ambayo ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake zilikuwa 27 kibindoni.

SEMAJI LATOA NENO HILI

 

SEMAJI Med
MASHINE ya kuongea Ahmed Ally wa Simba. Source: Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuwapa furaha Wanasimba na kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo watacheza uwanjani kitaifa na kimataifa.

“Tuna kikosi kizuri chenye wachezaji bora na uzoefu mkubwa, matokeo yaliyopita hayakuwa mazuri na sasa ni muda wetu kwenda kufanyia kazi makosa na kuwa imara kwenye mechi zetu ambazo tutacheza kwani usajili mzuri tumefanya.

“Unaona kwenye kila idara kuna wachezaji wenye uimara tulipoteza mchezo wetu wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zetu wa jadi, mashabiki hawakukasirika walikuwa na furaha kutokana na kiwango bora cha wachezaji hili ni kubwa linatupa hali ya kujiamini sasa tunakwenda kufanya kazi kubwa kwenye mashindano yanayofuata.”

SINGIDA FOUNTAIN GATE MKWARA MZITO

 

Issa
ISSA Liponda, Ofisa Habari wa Fountain Gate itakayokuwa inatoa burudani dhidi ya Namungo Uwanja wa Majaliwa. Source: Fountain Gate.

Singida Fountain Gate yenye ngome yake Manyara wao wamebainisha kuwa kwenye mechi tano za mwanzo kuna pointi 7 wanazitafuta ikishindikana watagotea kwenye pointi sita kwa kuwa wapo tayari kwa mapambano.

Singida Fountain Gate inadhaminiwa na SportPesa itaanza kutupa kete yake ugenini dhidi ya Namungo mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa itakuwa ni Julai 17 itakuwa uwanjani kusaka pointi tatu.

Kete ya pili itakuwa Uwanja wa KMC hapa dhidi ya Simba mchezo unaotarajiwa kuchezwa Agosti 25. Ni dakika 180 za moto ugenini kwa timu hiyo iliyomaliza ligi msimu wa 2023/24 ikiwa nafasi ya 11 na pointi 33.

Issa Liponda Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate amebainisha kwamba wanakwenda kufanya kazi kubwa kutafuta pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza iwe ugenini ama nyumbani.

“Kwenye mechi zetu tano za mwanzo ambazo ni pointi 15 hapa tunakwenda kwa hesabu kubwa kusaka ushindi kila mchezo na pointi ambazo tunaamini kwamba tutavuna ni 7 hamnahamna inaweza kugotea pointi 6 msije kusema sikuwaambia.”

Share this: