Mutale -Mutale -

KITAUMANA Uwanja wa Mkapa kwenye Kariakoo Dabi mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kuchezwa Agosti 8 2024 ikiwa ni ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Bofya link hii hapa ubashiri mechi zote za Ngao ya Jamii, Agosti 8 2024 https://sportpesa.co.tz/

Ni wazi msimu wa 2023/24 Ngao ya Jamii ilikuwa mikononi mwa Simba ilipata kwa ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kazi inaanza kwa mara nyingine kuelekea msimu mpya.

 

Gamondi
Gamondi Miguel Kocha Mkuu wa Yanga kuelekea Kariakoo Dabi, Agosti 8 2024. Source: Yanga.

 

Makocha wa pande zote mbili na wachezaji wamebainisha kwamba wapo tayari kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na kila timu kuwa na sura mpya baada ya kufanya usajili kukamilika.

KITAUMANA KWA MAKOCHA WA DABI

Kocha Mkuu wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa yaliyopita msimu wa 2023/24 wanasahau hivyo wanakwenda kuwakabili wapinzani wao upya kutokana na mabadiliko ambayo yapo kwenye timu husika.

“Hakuna siri kwenye mpira kila kitu lazima kiwe hadharani, kesho ni siku muhimu sana kwani ni mechi ya mtoano, hatupaswi kufanya makosa tunapaswa kuwa makini kwenye kila idara ili kupata matokeo mazuri, naamini mashabiki wetu watajitokeza kwa wingi kwa lengo la kutupa hamasa.

“Yaliyopita yamepita, sipendelei kufuatilia sana yaliyopita, huu ni msimu mpya hata wapinzani wetu pia wamebadilika kila kitu kimebadilika, wacha tuone kesho kitatokea nini.

“Tupo imara kiakili na kimwili, tumejianda vya kutosha hakuna tunachohofia, sijapata wasaa mzuri wa kuwatazama wapinzani kwani mechi zake nyingi hazikuoneshwa, lakini hiyo sio changamoto kubwa kwani naandaa timu yangu kwa asilimia 75, asilimia 25 ndio natumia kumchunguza mpinzani.

“Naheshimu sana wapinzani wote ninaokutana nao, kesho ni mchezo wa derby hakuna underdog kwenye mchezo huo kwani ni mchezo maalumu sana, najua mpinzani wetu ana timu mpya, wachezaji wapya, wote kwa pamoja watachukua fursa hii kuonesha ubora wao.” Gamondi.

Fadlu
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids. Source: Simba.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa wamekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi jambo ambalo linawafanya waingie uwanjani kwa tahadhari kupata matokeo mazuri uwanjani.

“Tulikuwa na maandalizi mazuri kuelekea kwenye msimu mpya ambao tunaamini kwamba utakuwa mzuri kikubwa ni utayari na wachezaji wapo tayari kuelekea kwenye mchezo wetu wa Kariakoo Dabi.

“Tunaichukulia mechi hii ya Kariakoo dabi dhidi ya wapinzani wetu kama mechi nyingine ambazo tunacheza kikubwa ambacho tunahitaji ni kupata ushindi na kuanza kwa kutwaa kombe hilo litatuongezea nguvu kuelekea kuanza kwa msimu mpya.

“Nina uzoefu na michezo mikubwa ya dabi, ukiangalia timu yetu ni mpya tutakuwa na mbinu tofauti kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu ambao tunaamini kuwa utakuwa na ushindani mkubwa.” Fadlu.

WACHEZAJI WA KARIAKOO DABI HAWA HAPA

Komein
Komein kipa wa Yanga akizungumza kuelekea Kariakoo Dabi, Agosti 8 2024, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Kwa upande wa wachezaji wa timu hizombili zenye maskani yake Kariakoo wameweka wazi kuwa wapo tayari kuelekea mchezo huo kikubwa mashabiki wajitokeze kupata burudani.

Khomein Abubakar kipa wa Yanga ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho amesema :“Tumejiandaa vizuri sana na tuko tayari, wachezaji wana ari na wote tunawahakikishia kuwa wachezaji tunakwenda kupambana, naamini kesho tutafanya vizuri

Mohamed Hussein, Zimbwe Jr nahodha wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo kutokana na maandalizi ambayo walifanya hivyo watapambana kupata matokeo chanya.

“Tumefanya maandalizi mazuri kuelekea kwenye mchezo wetu wa Ngao ya Jamii, tunaamini tutashirikiana na kufuata maelekezo ya mwalimu kupata ushindi dhidi ya wapinzani wetu.”

ZANZIBAR KAZIKAZI

Fei Toto
Fei Toto kiungo wa Azam FC 2024/25. Source: Azam.

Kwenye Uwanja wa New Amaan Complex kuna nusu fainali nyingine itachezwa ya Ngao ya Jamii kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union ya Tanga ikiwa ni kazi kwenye kusaka mshindi ambaye atatinga hatua ya fainali.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 11 na mshindi wa tatu pia atasakwa siku hiyohiyo na ligi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 16 2024 na mabingwa watetezi ni Yanga chini ya Gamondi.

Hasheem Ibwe Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union na wanawaheshimu wapinzani kwa kuwa sio timu ya kuibeza.

“Tunatambua huu ni mchezo muhimu kwetu tutaingia uwanjani kwa tahadhari kuwakabili wapinzani wetu kikubwa ni kuwapa burudani mashabiki na kupatata matokeo mazuri uwanjani.”

MAPILATO WA MECHI HAWA HAPA

Pilato wa Kariakoo Dabi ametangazwa kuwa Elly Sassi na ile ya Azam FC v Coastal Union ametangazwa kuwa Ahmed Arajiga hawa ni waamuzi wa kati.

Share this: