Chama alitambulishwa Yanga Julai Mosi -----Chama alitambulishwa Yanga Julai Mosi -----
Chama
HUOGOPI kicheko cha Chama na Pacome kuelekea 2024/25. Source: Yanga.

HAUOGOPI kuleta timu yako uwanjani kutokana na mitambo ya kazi yenye shauku kusaka ushindi ndani ya dakika 90? Hizo ni tambo za mashabiki wa Yanga kwenye mitandao ya kijamii baada ya utambulisho waClatous Chama kutikisa Bongo.

Chama amejiunga na Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kwa ajili ya kuendeleza majukumu yake kuekea msimu wa 2024/25 akitokea kikosi cha Simba baada ya mkataba wake kugota mwisho.

Ni wazi  kwamba ni Yanga  walitwaa ubingwa wa ligi. Wapo waliokuwa wakichana mikeka na wapo ambao walikula kirahisi hata wewe unaweza jisajili ukawa na nafasi ya kushinda kwa kutabiri na kuweka mkeka wako na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz 

Yanga inatajwa kuwa timu yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao jambo ambalo liongeza upana wa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

CHAMA KIBABE ZAIDI

Mwamba Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga. Julai Mosi 2024 nyota huyo alitambulishwa Yanga waliandika ujumbe mfupi kuwa : “Mwamba Clatous Chama ni Mwananchi, karibu Jangwani. Nyie hamuogopi?

Tayari Chama amejiunga na wachezaji wengine kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Chama alikutanishwa na kiungo wa kazi Pacome ambaye hucheza huku akitoa maelekezo.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 alikuwa ndani ya Simba na walipokutana kwenye Kariakoo Dabi ndani ya dakika 180, Simba ilipoteza pointi sita mazima na kufungwa jumla ya mabao saba huku wao wakifunga mabao mawili.

DUBE NDANI YA NYUMBA

Prince Dube
PRINCE Dube muuaji anayetabasamu akiwa na uzi wa Yanga ingizo jipya kuelekea 2024/25. Source: Yanga,

Ukiweka kando uwepo wa Pacome ndani ya Yanga ambaye ni kiungo wa kazi yupo mshambuliaji Prince Dube aliyekuwa anacheza ndani ya Azam FC.

Pacome alikuwa na kikosi cha Yanga 2023/24 hivyo ni mwenyeji kwa nyota hawa wawili.

Dube yeye ni mshambuliaji anatambua namna ushindani ulivyo kwa kuwa amecheza ndani ya Azam FC mpaka alipofikia hatua ya kuvunja mkataba na timu hiyo.

Kazi inatarajiwa kuwa kubwa kwa miamba hao wote ndani ya Yanga kupambania majukumu ya timu hiyo. Inatajwa kuwa mwamba Aziz Ki yupo kwenye hatua nzuri kusaini dili jipya hivyo kazi itazidi kuwa ngumu kwa wapinzani wao.

ISHU YA AZIZ KUIBUKIA SIMBA

AZIZ KI
AZIZ Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga msimu wa 2023/24. Source: Yanga.

Jina la mfungaji bora ndani ya ligi msimu wa 2023/24 Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga limekuwa likitajwa kuwa kwenye hesabu za watani zao wa jadi Simba, bosi wa Yanga amefungukia ishu hiyo.

Rekodi zinaonyesha kuwa ni mabao 21 Ki alifunga akitoa pasi 8 za mabao na alihusika kwenye mabao 29 ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi raia wa Argentina.

Gamondi kaongezewa kandarasi ya mwaka mmoja huku Aziz Ki ambaye alikuwa ni chaguo la kwanza kwa kocha huyo bado hajaongeza mkataba mpya kuendelea na majukumu yake kwa msimu mpya kwa sasa ni mchezaji huru.

Inaelezwa kuwa kuna timu zaidi ya mbili ambazo zinahitaji saini yake ikiwa ni Simba ya Tanzania, Mamelod Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini.

Kamwe amesema: “Kuna timu nyingi ambazo zinahitaji saini ya Aziz Ki tunalitambua ila kuhusu yeye kwenda kwa watani zetu wa jadi, (Simba) labda atakuwa ni Aziz mweingine ila sio huyu ambaye furaha yake ni ndani ya Yanga.

“Mazungumzo yanaendelea kuhusu mkataba wake mpya kwa kuwa kinachohitajika kinajulikana hivyo mashabiki wasiwe na presha, maisha ya mpira yana mengi hivyo taarifa zikikamilika tutaweka bayana kila kitu.”

BALAA LA AZIZ KI

Ni mabao 21 alifunga kiungo huyo ndani ya Yanga Aziz Ki mkali wa kutumia mguu wa kushoto ambapo alitumia mguu huo kufunga jumla ya mabao 17. Sio mguu wa kushoto pekee wenye balaa hata ule wa kulia una hatari pia. Aziz Ki alitupia mabao matatu akitumia mguu wa kulia.

Aziz Ki alifunga jumla ya mabao 15 akiwa ndani ya 18. Ni mabao sita alifunga akiwa nje ya 18. Kwenye eneo lolote anaweza kufunga mwamba huyu. Miongoni mwa timu aliyofunga akiwa nje ya 18 ilikuwa ni Tabora United alipofunga bao lake la 10 ndani ya ligi ilikuwa kwa pigo huru akitumia mguu wake wa kushoto.

Ki alitengeneza jumla ya pasi 8 za mabao ndani ya ligi. Pasi yake ya kwanza aliitoa dakika ya 64 kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex akiwa nje ya 18.

Aziz Ki kahusika kwenye mabao 29 kati ya 71 yaliyofungwa na Yanga ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24. Ipo wazi kwamba Yanga ni namba moja kwa timu ambazo zimefunga mabao mengi na safu yao ya ushambuliaji kuruhusu mabao machache ambayo ni 14  msimu wa 2023/24.

 

Share this: