----------------------------------------------n----------------------------------------------n
EURO
Lamine Yamal

KINDA wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona, Lamine Yamal amekuwa gumzo kubwa duniani kufuatia kufunga bao kali kutokea nje ya 18 na kuisaidia timu ya Taifa ya Uhispania kuiondosha Ufaransa na kutinga fainali ya mashindano ya Euro 2024.

Unaweza kubashiri mechi mbalimbali za EURO kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza www.sportpesa.co.tz

Lamine ambaye hivi karibuni picha yake akiogeshwa na staa wa Argentina katika moja ya matukio ya hisani ya klabu ya Barcelona imekuwa gumzo alifunga hilo dakika ya 21 ya mchezo akiisawazishia Uhispania waliokuwa wametanguliwa na bao la mapema la Kolo Muani.

Kiwango bora ambacho kimeonyeshwa na Lamine katika michuano kimewafanya, Barcelona kuingia hofu ya kumpoteza staa huyo kiasi cha kuweka kifungu cha kuhitaji kiasi cha Euro 868 milion kwa timu yoyote itakayomtaka staa huyo, wakati huu akitazamiwa kurithi mikoba ya Lionel Messi.

Yamal alizaliwa nchini Uhispania mwaka 2007 ambapo wazazi wake ni wenye asili ya Afrika, baba akiwa na asili ya Morocco huku mama yake akiwa na asili ya Equatorial Guinea.

Familia ya staa huyo ambao walikuwepo uwanjani walionekana kububujikwa na machozi kufuatia kushuhudia bao alilofunga. Lamine kwa mara ya kwanza aligunduliwa na mgundua vipaji wa Barcelona akiwa na miaka saba na kujiunga kituo cha Lamasia ambapo alicheza mchezo wake wa kwanza Barcelona akiwa na miaka 15 na siku 290.

YAMAL AMFUNGA MDOMO RABIOT

Licha ya kufunga bao hilo Yamal pia alionekana kuwa kwenye kiwango bora katika mchezo huo akishambulia kutoka winga ya kulia akifanikiwa kufunga bao moja lakini pia mpaka sasa akikimbiza chati ya nyota waliotoa asisti nyingi zaidi.

Kiwango hicho bora cha Lamine kilikuwa kama majibu kwa staa wa Ufaransa, Adrien Rabiot ambaye kabla ya mchezo huo alinukuliwa akisema, Lamine anapaswa kufanya makubwa zaidi ya yale anayoyafanya ili kucheza fainali.

ALICHOSEMA KOCHA WA UHISPANIA

Mara baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Uhispania, alinukuliwa akisema: “Tumeona miongoni mwa wachezaji bora zaidi ambao sote tunapaswa kumlinda kwa ajili ya manufaa ya baadae. Binafsi natamani kumuona akifanya makubwa zaidi na kuendelea kujifunza.

“Anacheza kama nyota ambaye ni mzoefu na mkongwe, hivyo tunatarajia makubwa na kumuona akifanya vizuri kwa miaka mingi ijayo. Ni ngumu kuona mchezaji mwenye umri mdogo kama yeye akacheza kwa kujiamini kiasi kile.

MBAPPE AKIRI AMEFELI EURO 2024

EUEO
Kylian Mbappe

Kufuatia kipigo hicho cha mabao 2-1 kutoka kwa Uhispania na kuondolewa kwenye mashindano ya EURO 2024, Nahodha wa Ufaransa, Kylian Mbappe amekiri kuwa mashindano hayo kwa upande wake yana tafsiri kuwa ni KUFELI.

Akizungumza baada ya kuondoshwa kwenye mashindano hayo, Mbappe amesema: “Nilitamani kuwa bingwa wa mashindano haya, kwa sasa natazamia kwenda mapumziko nadhani hiyo itanisaidia kurudi kwenye hali yangu ya kawaida na kuwa tayari kwa ajili ya maandalizi ya maisha mapya kwa kuwa kuna mengi napaswa kufanya.”

MBAPPE AKIRI ‘MASK’ ILIMVURUGA

Staa wa Ufaransa, Mbappe ambaye kwenye EURO 2024 alilazimika kuvaa kinyago maalum ‘Mask’ ya kukinga pua yake baada ya kupata jeraha la kuvunjika pua kwenye mchezo wao wa ufunguzi hatua ya makundi dhidi ya Austria huku akikiri ni miongoni mwa sababu ziliathiri kiwango chake.

Akizungumzia hilo kocha mkuu wa Ufaransa, Didier Deschamps amesema : “Ni kweli Mbappe hakuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo wetu wa hatua ya Robo fainali dhidi ya Ureno na hii kwa kiasi kikubwa ilisaabishwa na changamoto ya kulazimika kuvaaji mask kufuatia majeraha aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Austria.

“Lakini tulijitahidi kuhakikisha anakuwa huru zaidi na kucheza bila mask katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uhispania lakini kwa bahati mbaya hatukufanikiwa kwenda fainali.”

NI UHISPANIA Vs ENGLAND/UHOLANZI FAINALI EURO 2024

Baada ya kutinga fainali ya mashindano hayo, Uhispania sasa wanasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya England na Uholanzi ambayo inatarajiwa kupigwa leo usiku.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.