------------------------------------------------n------------------------------------------------n
CHAMA
Clatous Chama akisaini Yanga

RASMI mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga leo Jumatatu wamemtangaza kiungo wa kimataifa wa Zambia, Clatous Chota Chama kuwa mchezaji wao kuelekea msimu ujao.

Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesa kupitia akaunti zao rasmi za mtandao wa kijamii leo asubuhi waliweka machapisho ya utambulisho wa Chama ambayo yalisindikizwa na maneno: “, Clatous Chama ni Karibu sana Jangwani ?”

CHAMA ATAMBULISHWA KWA MAANDAMANO

CHAMA
Ali Kamwe akiongoza maandamano

Kama haitoshi kufanya utambulisho wa mtandaoni, Yanga kupitia kwa Ofisa habari wa timu hiyo, Ali Kamwe aliyeambatana na kundi la baadhi ya mashabiki na Wanachama wa timu hiyo waliratibu tukio la maandamano ‘Parade’ ya utambulisho wa Chama ambalo lilianzia Tandale Dar es Salaam hadi makao makuu ya timu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

ALI KAMWE AAHIDI KUWAFUNGA WATU 10

Ofisa habari wa Yanga akizungumzia usajili huo amesema: “Kama mlikuwa mnadhani kuwa tunatania basi jueni tu, kwamba hapa ndio tumeanza. Wiki hii nzima tunafurahia usajili wa Chama kwa matukio tofautitofauti.

“Huu ni uthibitisho kuwa Yanga inakwenda kutengeneza timu ya kubeba ubingwa wa Afrika, mfano kila ukijaribu kupanga kikosi chetu cha msimu ujao wewe mwenyewe unachanganyikiwa. Yaani msimu ujao tutampiga mtu 10.”

WACHAMBUZI WAFUNGUKA MAZITO

Kufuatia usajili huo, wachambuzi mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti kama ifuatavyo;

Jemedari Said

Kwa upande wake amesema haya ni maamuzi bora zaidi ambayo Simba wameyafanya kwa ajili ya Taasisi katika kipindi cha misimu kadhaa iliyopita.

Farhan Jr

CHAMA 10
Mchambuzi, Farhan Jr

“Ni taarifa ambayo nilikuwa naifahamu, lakini moyo tu ulikuwa unagoma kukubaliana na ukweli, ni kitu ambacho nilijidanganya kuwa hiyo siku wakimpost sitoumia ila sio kweli, nimeumia sana na huu usajili, niliamini nimeshazoea ndani ya mwezi mzima niliishi nikifahamu ila nilipoona post leo nilishika ganzi.

“Hutokea pale Mchezaji bora kuwahi kutokea kwenye historia ya huu mpira wa Tanzania, Rafiki yako na umeishi kuyaona matukio yake bora uwanjani anaondoka klabuni, iliwahi kunitokea hii kwa Eden Hazard, Emmanuel Okwi na leo imejirudia, ndio football ni sehemu ya furaha na maumivu makali sana.

“Suala wala sio kwenda Yanga bali hii picha inajirudia kichwani mwangu kuwa wana CHAMA Technician, wana AZIZ Technician, wana PACOME Ball Dancer, wana Maxi Nzengeli Engine ya Scania na Wana AUCHO The Tank kwenye kiduara, halafu mbele una DUBE The Baby Face Assasin, hii ni simulizi ya kutisha sana.

“Hii imeuma sana hii, BORN RED MAESTRO Ndio umezaliwa kuwa Mwekundu, BORN READY, yes umezaliwa kuwa tayari, na upo tayari kwa hii changamoto mpya, all the best Baller! BORN RED, BORN READY. HII IMENIUMA VIBAYA MNO.

“SHABIKI WA SIMBA nisikilize tu kidogo, mpira wa miguu ni burudani lakini kwa upande mwingine ni biashara, anayeipenda klabu ni SHABIKI na anayefanya kazi ya mpira ni MCHEZAJI, mmoja anaburudika na mmoja kati ya hao wawili yupo kibaruani, hata wewe ambaye ni Shabiki una ajira yako pengine sehemu huwa unahama kufuata maslahi mazuri, ndio kama ilivyo kwenye soka.

“CHAMA tayari ameondoka klabuni, ni sehemu ya football ila SIMBA imesalia na itaendelea kuwepo, hata kama asingeondoka basi kuna siku angestaafu na maisha yangeendelea, ni sahihi kuumia ila ni sahihi zaidi kutopanic na kutupiana lawama yoyote kwa Viongozi au Mchezaji kwakuwa hii ni biashara kuna kukubaliana na kutokubaliana.

“SHABIKI wewe ipende hii logo ya Simba, fahamu ni wewe pekee hutohama ila wengine woote wanakuja na kuondoka haswa Wafanyakazi wakiwemo Wachezaji, Messi Lionel ameondoka Barcelona, pale Liverpool walimtengeneza Michael Owen ila akasepa zake, Chelsea tulimpika Hazard akasepa zake, Man United walimtengeneza Beckham ila akaondoka, ni kawaida sana kwenye dunia ya mpira.

“SIMBA aliwahi kuondoka, Juma Kaseja kwenye ubora wake, Emmanuel Okwi kwenye ubora na wengine wengi tu ila klabu iliendelea na wachezaji wengine akiwemo CHAMA ambaye alijenga Ufalme wake, leo umetamatika hivyo klabu itapaswa kuanza maisha mpya na zama mpya, tukubaliane kwa pamoja kuwa nothing is there forever.

“Sisi kama klabu tuna mengi ya kufanya haswa wakati huu ‘focus’ yetu ni kupaza sauti kuwahimiza wasajili Wachezaji wa maana, tushauri, tukae chini kama klabu ili tufike sehemu kubwa na nzuri, huu sio wakati wa kunyoosheana vidole wala kupishana bali kuanza mwanzo mpya ambao sote tunautaka, anayehisi hajapenda ahame tu klabu, wala sio suala ila football ni kawaida sana hivi vitu.

“Tukae nyuma ya timu, tusupport Wachezaji wote ambao watasajiliwa na tukubali kuwa TRIPLE C ameshaondoka, ila timu haiwezi kufa, maisha yataendelea na tumtakie heri kwenye changamoto mpya.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.