JobeJobe

 

NTIBANZOKIZA
MTIKISIKO umepita na mwamba Ntibanzokiza mwenye mabao 11 ndani ya ligi msimu wa 2023/24. Source: Simba.

MTIKISIKO mkubwa Simba kwa sasa unaendelea kutokana na maboresho ya kikosi hicho. Tayari mastaa wameanza kuagwa kwenye timu hiyo ambayo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024/25 ambapo itakuwa ni kivumbi kwenye mechi dakika 90.

Ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi ni uhakika kupeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Pointi 80 walikomba Yanga na kutwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa itakuwa kwenye anga moja na Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo baada ya kugotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa sawa pointi na Simba tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.

Tayari nyota zaidi ya wawili wamethibitishwa kuwa hawatakuwa kwenye kikosi cha Simba ikiwa ni mtikisiko mkubwa kutokana na ubora walionao wachezaji hao pamoja na nafasi muhimu walizokuwa wakicheza.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa wanatambua umuhimu wa wachezaji wote waliopo ndani ya Simba lakini maboresho lazima yafanyike kwa baadhi ya wachezaji kuondoka na wengine wapya kuingia katika kikosi.

“Tunafanya maboresho ya kikosi kwa ajili ya kurejea kwenye ushindani. Kwa sasa tunaanza na wale ambao tunawaaga kisha tutaanza kuwatambulisha wachezaji wengine wapya hilo lipo wazi na tunafanya yote kwa umakini mkubwa kwa ajili ya kikosi kipya cha msimu ujao.

“Wachezaji ambao hatutakuwa nao ni pamoja na nahodha wetu bora ambaye ni mshambuliaji John Bocco tunatambua mchango wake, kazi yake kubwa ndani ya Simba lakini hakuna namna imekuwa hivyo. Yupo Saido Ntibanzokiza tunatambua namna alivyofanya kazi kubwa kwenye kikosi alikuwa anaipenda kazi yake kweli lakini hatutakuwa naye wakati ujao.

“Kinachofanyika kwa wakati huu ni maboresho, mashabiki ni muhimu kuwa na subira na kuendelea kuwa pamoja kwa ajili ya kuona kwamba tunafikia malengo yetu na kupata furaha ambayo tuliikosa kwa muda mrefu, inawezekana na muda unakuja.”

MKALI WA KAZI KAKUTANA NACHO

Luis
KIUNGO wa Simba Luis jezi namba 11 hatakuwa ndani ya Simba msimu wa 2024/25. Source: Simba.

Mkali wa kazi ambaye ana uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kushoto amekutana nacho kwa kupewa mkono wa asante ndani ya kikosi cha Simba. Hivyo nyota huyo hatakuwa ndani ya Simba msimu wa 2024/25.

Anaitwa Luis Miquissone raia Juni 19 2024 aliunganishwa kwenye orodha ya wale ambao wamekutana na Thank You mazima. Taarifa kutoka Simba ilieleza kwamba ni mkataba wake wa mwaka mmoja ulikuwa umeisha hivyo hawajamuongezea mwingine.

Kiungo huyo alirejea mitaa ya Msimbazi msimu wa 2023/24 alikuwa ndani ya Al Ahly ya Misri huko alivunja mkataba wake kwa kuwa hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza. Kwenye mechi za ligi ni 19 kakomba dakika 410 na kutoa pasi tatu zilizoleta mabao.

Miquissone amefunga bao moja katika mechi mbili alizocheza akiwa na jumla ya dakika 82 kwenye CRDB Federation Cup. Taji hilo pia lipo mikononi mwa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa.

NAHODHA BOCCO

JOHN Bocco
JOHN Bocco nahodha wa Simba ambaye alifunga mabao 2 hatakuwa katika kikosi hicho msimu wa 2024/25. Source: Simba.

Huyu ni nyota wa kwanza kukutana na Thank You ndani ya Simba hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi msimu wa 2024/25. Nyota huyo ni mechi tano alicheza na kutupia jumla ya mabao mawili kati ya 59 yaliyofungwa kwenye ligi.

Ipo wazi kwamba Yanga ni namba moja kwa timu ambazo zilifunga mabao mengi ambayo ni 71 baada ya kucheza mechi 30 kinara akiwa ni Aziz Ki aliyefunga jumla ya mabao 21 ilikuwa ni Juni 17.

NTIBANZOKIZA

Kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza alifuata kupewa Thank You ndani ya kikosi cha Simba. Ilikuwa Juni 18 ambapo nyota huyo aliagwa rasmi kwa kutoongezewa mkataba wake mpya.

Ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Simba alitupia jumla ya mabao 11 akiwa kafunga mabao 7 kwa mikwaju ya penalti ambapo alikuwa namba moja kwenye upande wa wakali wa mapigo huru ndani ya ligi kiujumla.

CHILUNDA

Shaban Chilunda kiungo mshambuliaji aliyesaini dili la mwaka mmoja ndani ya Simba hajaongezewa mkataba kwenye timu hiyo. Nyota huyo ni ingizo jipya alisaini dili hilo akiwa huru baada ya kutoongeza mkataba ndani ya Azam FC.

Juni 19 aliungana na Luis ambaye naye hakuongezewa mkataba. Ikumbukwe kwamba alikuwa akicheza kwa mkopo ndani ya KMC. Hivyo hatakuwa ndani ya Simba ndani ya unyamani.

 

Share this: