
MABINGWA wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 ni Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya SportPesa baada ya kufikisha pointi ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya Ligi Kuu Bara wanabalaa kwa kupindua meza kibabe mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar na kufanikisha malengo yao.
Ipo wazi kwamba Yanga walikuwa ni mabingwa watetezi na nia yao tangu awali ilikuwa ni kuona kwamba wanatwaa taji hilo kubwa na washindani wake walikuwa ni Azam FC na Simba ndani ya tatu bora.
Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibw Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Mei 13 2024 Uwanja wa Manungu umewapa taji hilo la 30 wakitwaa mara tatu mfululizo taji hilo ambalo thamani yake inazidi kupanda kila iitwapo leo.
MCHEZO ULIVYOKUWA

Katika mchezo wa 27 wa Yanga walishuhudia wakikomba dakika 45 za mwanzo wakiwa nyuma kwa bao la mepama lililofungwa na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Charles Ilanfya dakika ya 32.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya kweli kwa kuanza kupata bao dakika ya 62 kupitia kwa Kennedy Musonda na dakika ya 66 katika harakati za kuokoa Mtibwa Sugar walijifunga kupitia kwa Nasry Kombo na kamba ya tatu ilifungwa na Clement Mzize.
Mzize alipachika bao hilo la kukamilisha pointi tatu ilikuwa dakika ya 81 akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya beki wa kazi ambaye ni nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto.
Mtibwa Sugar wanabakiwa na pointi 20 wakipambana kupata matokeo katika mechi zinazofuata ambazo ni tatu ili wasishuke daraja kuelekea kwenye Championship.
VITA HII BADO MBICHI

Wakati vita ya ubingwa ikiwa imegota mwisho msimu wa 2023/24 kuna vita nyingine tatu ambazo bado ni mbichi ndani ya ligi mpaka pale itakapokamilika.
Vita ya kiatu cha ufugaji bora kwa sasa ni viungo wawili wametupia mabao 15 kwa kila mmoja huku mechi zikiwa zimesalia tatu kwa upande wao.
Aziz Ki wa Yanga inayoongoza ligi na mabingwa wa ligi ni pointi 71 wanazo huku yeye akiwa katupia mabao 15 kibindoni.
Feisal Salum wa Azam FC ni mabao 15 pia katupia ndani ya ligi akiwa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 60 zote zimecheza mechi 27.
Vita nyingine ni nafasi ya pili hapa Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi 57 ikiwa imecheza mechi 26 inapambania na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 60 baada ya kucheza mechi 27.
Vita ya tatu ni kushuka daraja ambapo timu mbili zitakazomaliza nafasi ya 16 na 15 hizo zitashuka daraja na timu mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 hizo zitacheza hatua ya mtoano kutambua nani atabaki kwenye ligi.
MAKOCHA WALIOTWAA MATAJI YA LIGI KARIBUNI
2023/24
Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imetwaa ubingwa baada ya ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar. Mei 13 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Manungu ulisoma Mtibwa Sugar 1-3 Yanga.
Ni pointi 71 Yanga inafikisha baada ya kucheza mechi 27 ina mechi tatu mkononi za kukamilisha ratiba kwa msimu wa 2023/24 ambapo pointi hizo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi kuu bara.
2022/23
Ubingwa ulitwaliwa na Yanga kwa pointi 78 zama hizo ilikuwa chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ushirikianao na Cedrick Kaze kwenye benchi la ufundi.
Nabi alitwaa ubingwa mara mbili mfululizo akiwa kwenye benchi la Yanga kwa kuwa alianza kufanya hivyo msimu wa 2021/22 alipotwaa taji la ligi kwa jumla ya pointi 74.
2020/21
Didier Gomes alikuwa Kocha Mkuu wa Simba alikiongoza kikosi hicho kikwataa ubingwa wa ligi msimu huo kwa pointi 83 kibindoni.
2019/20
Svend Vandenbroeck jeshi la mtu mmoja, kocha anayetajwa kuwa na misimamo yake mwanzo mwisho alikuwa kwenye benchi la ufundi wakati Simba ikitwaa ubingwa kwa kufikisha jumla ya pointi 88.
2018/19
Ni Patrick Aussems walikuwa wanapenda kumuita Uchebe fundi kabisa alikuwa kwenye benchi la ufundi akiwapa mbinu akina Clatous Chama, Hassan Dilunga, Said Ndemla kwenye zama zake na walitwaa ubingwa wakiwa na pointi 93.
2017/18
Kutoka Ufaransa mwamba kabisa Pierre Le Chantre alikuwa kwenye benchi la ufundi akiwapa mbinu mastaa wa Simba zama za Emmanuel Okwi kwenye ubora wake, John Bocco akiwa katika mwendo mkali.
Pointi 69 walikomba na kutwaa wa Ligi Kuu Bara chini ya kocha huyo ambapo Simba ilikuwa inadhaminiwa na Kampuni ya SportPesa.

