AZAM FC gari limewaka kwa kukusanya jumla ya pointi 54 kibindoni ndani ya ligi huku ikiwaacha kwa jumlaya pointi 8 wapinzani wao Simba wenye pointi 46 timu hizi mbili zipo Zanzibar kwa ajili ya kupambania Kombe la Muungano 2024 na timu nne zitashiriki ikiwa ni baada ya kupita miaka 20 kwa kombe hilo kufanyika.

AZAM FC NAFASI YAKE

Fei na Lyanga
Fei na Lyanga nyota wa Azam FC wakishangilia moja ya bao walilofunga kwenye mchezo wa ushindani. Source: Azam FC

Msimu wa 2023/24 ambao unaushindani mkubwa kila idara kwenye upande wa nafasi ipo nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 24 ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Pointi zake kibindoni ni 54 ilipata ushindi kwenye mechi 16 huku ikipoteza katika mechi mbili na kuambulia sare kwenye mechi sita uwanjani kwenye msako wa pointi tatu.

Kwenye mechi ambazo walipata ushindi walikuwa wababe mbele ya Yanga mzunguko wa pili kwa ushindi wa mabao 2-1 na kwenye mechi mbili ilizopoteza ilikuwa dhidi ya Yanga na Namungo.

Mbele ya Simba kwenye mchezo wa ligi walitoshana nguvu baada ya dakika 90 ubao kusoma Simba 1-1 Azam FC bado hawajakutana mzunguko wa pili mchezo unaosubiriwa kwa shuku kubwa na wababe hao wawili.

MKALI WAO KUCHEKA NA NYAVU

Fei Toto
Fei Toto kiungo mshambuliaji wa Azam FC ambaye ni kinara wa utupiaji mabao ndani ya timu hiyo. Source: Azam FC

Mwamba Feisal Salum yeye anacheka tu na nyavu akiwa ni namba moja kwenye utupiaji wa mabao kwenye kikosi hicho akiwa ametupia mabao 14 ambapo bao lake la 14 ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-0 Ihefu huku bao hilo likifungwa dakika ya 13 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Kiungo huyo amesema: “Kikubwa ni ushirikiano ambao upo na tunatambua kwamba kila timu inafanya kazi kubwa kusaka ushindi tutaendelea kufanya vizuri na kushirikiana,”.

WAPO NDANI YA CRDB FEDERATION CUP

Lyanga na Dabo
Lyanga jezi namba saba Nado wakisikiliza maelekezo kutoka kwa kochaYusuph Dabo. Source: Azam FC

Timu hiyo imetinga hatua ya robo fanali CRDB Federation Cup baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa 16 bora Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ulichezwa Aprili 7 2024 na mabao ya Azam FC yalifungwa na Fei Toto, Ayoub Lyanga na Sopu ikiwa ni safari nyingine kuwania taji hilo lililo mikononi mwa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa.

Ipo wazi kwamba fainali ya 2023 katika taji hilo ilikuwa ni Yanga dhidi ya Azam FC na Yanga waliibuka wababe Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa ushindi wa bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Kennedy Musonda.

Heshem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wanahitaji kuwa na mwendelezo mzuri na kupata mataji ikiwa ni pamoja na CRDB Federation Cup.

“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi ambazo tunacheza kikubwa ni kupata mataji hilo linawezekana na tunatambua umuhimu wa taji hili la CRDB Federation Cup tutaendelea kupambana,”.

 

JEMBE JIPYA NDANI

Yoro
Yoro jembe jipya ndani ya kikosi cha Azam FC. Source: Azam FC

Aprili 19 2024 matajiri wa Dar walitoa taarifa rasmi kuwa wamefikia makubaliano na akademi ya Yeleen Olympique ya Mali kwa ajili ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Yoro Mamadou Diaby.

Nyota huyo ni mlinzi wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye Klabu ya Stade Malien de Bamako, atajiunga rasmi na Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi.

Akiwa klabuni Stade Malien de Bamako, Yoro alikuwa miongoni mwa nyota waliotimiza majukumu yao ndani ya klabu hiyo ambayo ilifika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho, aliifungia timu yake mabao katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Dreams FC ya Ghana.

Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23. Pia alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria. Hivyo anaungana na matajiri hao kwa ajili ya kupata changamoto mpya

Mbali na nyota huyo ambaye ni ingizo jipya kuna mastaa walioongezewa mikataba ikiwa ni pamoja na mwamba Lusajo Mwaikenda ambaye yeye bado ataendelea kuwa na uzi wa Azam FC mpaka 2027.

Beki Pascla Msindo ambaye alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba naye ameongezewa mkataba hivyo bado yupo ndani ya timu hiyo inayoshiriki Muungano 2024 ikiwa nafasi ya pili kwenye ligi.

Nyota huyo wa kupanda na kushuka dili lake ni mpaka 2027 ndani ya Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za nyumbani.

Share this: