
MSAFARA wa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga umetua rasmi nchini Afrika Kusini leo Jumanne kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Yanga ambao wanadhaminiwa na kampuni ya michezo ya SportPesa Ijumaa hii wanatarajiwa kuwa wageni wa Mamelodi Sundowns katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kupigwa jijini Pretoria nchini Afrika Kusini.
Mchezo huo unakuja mara baada ya matokeo ya suluhu katika mchezo wa mkondo wa pili ambao ulipigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mshindi wa matokeo ya jumla anatarajiwa kukata tikei ya moja kwa moja ya kutinga nusu fainali yua mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu.
JESHI LA WACHEZAJI 26 LAONDOKA DAR, ALFAJIRI

Kuelekea mchezo huo benchi la ufundi la Yanga limepitisha majina ya wachezaji 26 ambao leo Jumanne alfajiri waliondoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Mamemodi Sundowns utakaopigwa siku ya Ijumaa.
WATUA SAUZI MCHANA
Baada ya safari ya muda mrefu hatimaye kupitia akaunti zao rasmi za mitandao ya kijamii, Yanga majira ya saa nane mchana waliutangazia Umma wa mashabiki wa timu hiyo na wadau mbalimbali wa michezo kuwa wamewasili salama jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
PACOME, YAO, AUCHO WAONGEZA MZUKA

Yanga wakipewa jeuri ya Pesa kutoka Kampuni ya michezo ya SportPesa wanaingia katika mchezo huu wakiwa na mzuka kufuatia kuunganishwa kwenye msafara kwa mastaa wao watatu ambao walikosa mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam, ambao ni Khalid Aucho, Yao Kouassi Attohoula na Zouzoua Pacome.
ALICHOSEMA KOCHA GAMONDI

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi akizungumzia mchezo huo alisema: “Kwanza kabisa kama kiongozi nimefarijika sana na najivunia upambanaji wa wachezaji wangu ambao waliouonyesha kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao tumecheza nyumbani Tanzania.
“Licha ya kukabiliwa na tishio kubwa la majeruhi na kuwakosa baadhi ya wachezaji wetu muhimu, lakini vijana wangu walipambana kuhakikisha tunapata matokeo tena dhidi ya miongoni mwa timu bora zaidi Afrika kwa sasa.
“Kwa nafasi ya pekee pia nawapongeza sana mashabiki wetu ambao walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutuongezea morali kupitia sapoti yao, kuona mashabiki wamejaa katika mchezo ambao ulipanga kuchezwa muda wa usiku sio jambo dogo.
“Tunajua tunakabiliwa na mchezo mgumu wa ugenini lakini sisi ni watu ambao tunaamini sana katika ubora wetu hivyo tunakwenda kupambana kwenye dakika 90 nyingine tukiwa na malengo ya kufuzu nusu fainali.”
ARAFAT AAHIDI USHINDI YANGA

Makamu Rais wa Yanga, Arafat na uongozi wake ambao unadhaminiwa na SportPesa amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa kikosi chao kinakwenda kufanya kila jitihada kuhakikisha wanapata matokeo na kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo.
Arafat alisema kama uongozi unajivunia kiwango ambacho kimeonyeshwa na timu yao katika mchezo wa mkondo wa kwanza na wanaamini kuwa wana nafasi ya kufanya makubwa Afrika Kusini.
“Tunashukuru sana kwa namna ambavyo mashabiki wetu wamekuwa wakishirikiana na viongozi katika kuisapoti timu yetu, jambo ambalo linaongeza Mshikamano kati yetu ambao ni nguzo muhimu ya mafanikio ya timu yetu.
“Wapo mashabiki wa Yanga ambao wanaendelea na safari ya kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuwapa sapoti na kuishangilia timu.
“Kama uongozi tunapenda kuwaahidi mashabiki wetu kuwa kama uongozi tumefanya kila jitihada za kuiandaa timu yetu kwa ajili ya mchezo huo wa Ijumaa na tuna matarajio makubwa kwamba tutafanya vizuri na kupata matokeo yatakayotupeleka nusu fainali.
“Hivyo kwa mashabiki wetu ambao wamesafiri na basi ni matumaini yangu kuwa safari ya klurudi itakuwa fupi sana kutokana na furaha ambayo tutakuwa nayo baada ya kuwatoa Mamelodi Sundowns.
KIKOSI YANGA KINACHOWAFUATA MAMELODI HIKI HAPA
;
Djigui Diarra
Aboutwalib Mshery
Metacha Mnata
;
Bakari Mwamnyeto
Ibrahim Bacca
Dickson Job
Yao Attohoula Kouasi
Nickson Kibabage
Joyce Lomalisa
Gift Fred
Kibwana Shomari
;
Khalid Aucho
Zawadi Mauya
Salum Abubakar
Jonas Mkude
Mudathir Yahya
Maxi Nzengeli
Pacome Peodoh Zouzoua
Stephane Aziz Ki
Augustine Okrah
Mahlatse Skudu Makudubela
Farid Mussa
Denis Nkane
;
Clement Mzize
Joseph Guede
Kennedy Musonda
