Matumaini Kibu V Al AhlyKibu V Al Ahly
  • Uongozi Simba wataja mbinu za kupata ushindi dhidi ya Al Ahly ugenini kimataifa
  • Hesabu kubwa ni kufikia malengo ya kutinga hatua ya nusu fainali 
  • Ratiba yao Aprili ni bandika bandua mwanzo mwisho

MATUMAINI ni makubwa kwa Klabu ya Simba kutinga nusu fainali licha ya kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliochezwa Uwanja wa Mkapa Machi 29 kwa kupoteza mchezo wa hatua ya robo fainali mkondo wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 baada ya dakika 90 umepania kupindua meza kibaba ugenini mchezo wa mkondo wa pili.

Chama v Al Ahly
MWAMBA wa Lusaka Clatous Chama akiwa kwenye jitihada za kutimiza majukumu yake dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo wawakilishi wa Tanzania wakiwa nyumbani jitihada za kusaka ushindi ziligonga mwamba walipofungwa bao la mapema dakika ya 5   kazi kubwa imebaki ugenini itakuwa ni Aprili 5 nchini Misri.

Katika mchezo huo Simba ilikuwa bora kwenye eneo la umiliki wa mpira na kufanya mashambulizi mengi kwa wapinzani wao lakini umakini ulikuwa mdogo kwao jambo lililosababisha wakapoteza mazima mchezo wa kwanza.

UJANJA WA AL AHLY

 Al Ahly, kutoka Misri walikuwa wajanja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa ugenini walipoanza kufanya kazi kubwa mpango kazi wao kwa kutafuta bao la mapema na walifanikiwa.

 Ambacho walifanya kwenye mchezo huo waliwaacha Simba wacheze mpira wao wakaziba njia zote zilizokuwa zinatumiwa na Simba kutafuta nafasi na mwisho wakapata ushindi wakiwa nyumbani.

Kiungo wa Simba Clatous Chama ambaye ni mtengeneza mipango namba moja ndani ya kikosi cha kwanza alikomba dakika 90 mazima alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wapinzani wao Al Ahly mwanzo mwisho kwenye mchezo huo.

MUUAJI WA SIMBA KWA MKAPA

Kouka
AHMED Kouka nyota wa Al Ahly mfungaji wa bao la ushindi dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa. Source: Al Ahly

Safu ya ulinzi ya Simba iliyokuwa chini ya Henock Inonga, Shomari Kapombe, Mohamed Hussen walikuwa na kazi kubwa kuweka ulinzi lakini walikwama katika dakika5 za mwanzo.

Presha kubwa ya ushambuliaji ilifanywa na mwisho  kosa la dakika ya 5 liliwagharimu na kumpa nafasi muuaji wa Simba Ahmed Kouka kupachika bao hilo ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Aprili 5 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa kukamilisha ngwe ya safari ya robo fainali kumpata mshindi wa jumla hatua ya nusu fainali, kazi imeongezewa ugumu kwa Simba.

USHAMBULIAJI TATIZO KWA SIMBA

Kibu V Al Ahly
Kibu Dennis kiungo mshambuliaji wa Simba akiwa kwenye majukumu yake dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba

Kwenye mchezo huo Simba ilikuwa bora kwenye mbinu na ilitengeneza nafasi nyingi lakini kwenye eneo la umaliziaji muda wote ulikosa umakini kusahihisha makosa ya safu ya ulinzi.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 0-1 Al Ahly hivyo Simba wanakibarua cha kusaka ushindi ugenini kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Rekodi zinaonyesha kuwa jumla ya mashuti 20 Simba ilipiga kuelekea lango la wapinzani wao Al Ahly lakini katika hayo ni 7 pekee yalilenga lango na kuokolewa na kipa wa Al Ahly.

BOSI WA SIMBA ATOA NENO HILI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Muhene, (Tryagain) ameweka wazi kuwa bado wana nafasi ya kufikia malengo ya kutinga hatua ya nusu fainali kutokana na maandalizi ambayo yanaendelea kufanyika.

“Kikubwa ni kuwa makini kwenye eneo la uwanja pamoja na ushirikiano kwani kwa wakati huu ni muhimu kuendelea umoja wetu ambao ni nguzo kwetu kupata ushindi katika mchezo wetu dhidi ya wapinzani wetu kimataifa.

“Ilikuwa ni kazi kubwa kutafuta ushindi lakini hatukufanikiwa kushindwa kuwa na bahati nyumbani haina maana kwamba tutakwama kuwa na bahati wakati mwingine tunafanya maandalizi kupata matokeo ugenini hilo linawezekana,”

HII RATIBA YA SIMBA APRILI

Aprili 5 Al Ahly v Simba, itakuwa ugenini, robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, walipokutana Uwanja wa Mkapa ilikuwa Simba 0-1 Al Ahly.

Aprili 9 Mashujaa v Simba mchezo wa Azam Sports Federation itakuwa ugenini, kwenye ligi Mashujaa walipoteza mechi zote mbili nje ndani, Uwanja wa Lake Tanganyika ilikuwa Mashujaa 0-1 Simba, Uwanja wa AzamComplex, Simba 2-0 Mashujaa mabao yalifungwa na Chama.

Aprili 13 Ihefu v Simba, Ligi Kuu Bara itakuwa ugenini, mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye ligi Uwanja wa Mkapa, Simba 2-1 Ihefu.

Aprili 2024 Yanga v Simba, utapangiwa tarehe pia itakuwa ugenini, mchezo wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Mkapa Simba 1-5 Yanga.

Aprili 2024 dhidi ya Namungo utapangiwa tarehe pia itakuwa ugenini, mchezo wa ligi mzunguko wa kwanza Simba 1-1 Namungo,Uwanja wa Uhuru.

 

Share this: