HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imemalizika kwa staili ya aina yake ambapo Tanzania imekuwa Taifa pekee ambalo limefanikiwa kutoa timu mbili ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali.
Ni Simba ambao wamefuzu kutokea kundi B la mashindano hayo wakimaliza kwenye nafasi ya pili na pointi zao tisa ambazo wamekusanya katika michezo sita. Kutoka kwenye kundi lao ni wao na Asec Mimosas ya Ivory Coast ndio wamefuzu Robo Fainali.
Kwa upande wa Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya SportPesa wao wamefuzu hatua ya Robo Fainali kutokea kundi D ambapo nao wamemaliza kama ‘Runner up’ yaani wamemaliza kwenye nafasi ya pili nyuma ya bingwa mtetezio Al Ahly.
TIMU ZILIZOFUZU ROBO FAINALI

Timu 8 kutoka makundi manne ya Ligi ya Mabingwa msimu huu wa 2023/24 zimefuzub hatua ya Robo Fainali ambapo kundi A ni Mamelodi Sundowns na TP Mazembe ndio waliofikia hatua hiyo.
Kutoka kundi B ni timu za Asec Mimosas na Simba ndio ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali, kutoka kundi C ni Petro Atletico na Esperance ndio zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali, huku kund D likishuhudia bingwa mtetezi Al Ahly na Yanga zikifuzu.
DROO YA ROBO FAINALI INAPIGWA LINI?

Droo ya hatua ya Robo Fainali ya mashindano hayo inatarajiwa kupigwa siku ya Jumanneno ijayo yaani Machi 12, mwaka huu ambapo kila timu itajua ni mpinzani gani wanakwenda kukutana naye katika hatua hiyo.
Lakini huku droo hiyo ikiwa inasubiriwa kwa hamu, kutokana na namna hatua ya makundi ilivyomalizika tayari ni dhahiri kuna namna ya kuweza kubashiri timu ambazo zinaweza kukutana katika hatua hiyo.
KANUNI ZA DROO YA ROBO FAINALI
Zipo kanuni nyingi kuihusu namna ambavyo droo ya hatua hii inavyochezeshwa, lakini miongoni mwa mambo muhimu ni kuwa timu ambazo zimemaliza kwenye nafasi ya kwanza basi huwa haziwezi kukutana kwa kuwa zinakuwa kwenye ‘pot’ moja, kama ilivyo kwa zile zilizomaliza kwenye nafasi ya pili.
Hivyo imu zilizomaliza vinara wa hatua ya makundi hukutana na timu zilizomaliza nafasi ya pili, lakini pia timu ambazo zilikuwa kwenye kundi moja kwenye hatua ya makundi haziwezi kukutana kwenye hatua ya Robo Fainali.
YANGA, SIMBA KUKUTANA NA NANI?

Kwa kuzingatia kanuni tajwa hapo juu wawakilishi wa Tanzania Yanga na Simba katika hatua hiyo ya Robo Fainali wanaweza kukutana na wapinzani wafuatao;
Yanga
Wakiwa wametinga hatua hii kwa mara ya kwanza Yanga (kwa msaada mkubwa wa udhamini wa (SportPesa) wana nafasi kubwa ya kukutana na Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas au Petro Atletico
Simba SC
Wazoefu wa hatua hii wakiwa wametinga kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wao wana nafasi kubwa ya kuvaana na Mamelodi Sundowns, Al Ahly, au Petro De Luanda
EDO AZIONYA YANGA, SIMBA ROBO FAINALI
“Kama Simba na Yanga wanataka kwenda nusu fainali basi waombee bahati ya kutopangwa na Mamelodi Sundowns ambao wameongoza katika kundi A. Kila mmoja anaweza kupewa Mamelodi. Yanga wana bahati kwamba wanaweza kupewa ASEC Mimosas.
“Lakini wanaweza kupewa Petro Atletico ya Angola. Bahati nzuri kwao ni kwamba hawawezi kupewa Al Ahly ambao walikuwa nao kundi moja. Bahati mbaya kwa Simba ni kwamba anaweza kupewa Al Ahly au Mamelodi. Bahati nzuri kwao ni kama ikipewa Petro Atletico.
“Hawa kina Al Ahly na Mamelodi sio watu wazuri sana katika hatua za robo fainali. Kwao inakuwa kama vile michuano ndio imeanza. Kwa Mnyama kama itatokea nafasi ya kupewa Al Ahly au Mamelodi basi ni bora wapewe Al Ahly. Hawaonekani kuwa sawa kama walivyokuwa katika miaka ya nyuma.
“Simba anaweza kupambana na Al Ahly kama alivyofanya katika michuano ya Super League. Mamelodi ni ndoto ya kutisha. Sio Yanga wala Simba ambao wanaweza kupambana nao kwa sasa. Petro hawana historia ya kutisha katika michuano hii.
“Kwa upande wa ASEC itashangaza kama wanaweza kuwa timu ya kwanza ya Afrika Magharibi kufika nusu fainali tangu Enyimba walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2003 ambapo walikwenda moja kwa moja kuchukua taji hilo na kuwa timu ya mwisho ya Afrika Magharibi kufanya hivyo.” Amenukuliwa mchambuzi Edo Kumwembe.

