- Washindi watatu kila wiki wa AFKON,Ushindi ni SportPesa wanaondoka na Simu Janja.
- Washindi 100 kila siku wanaondoka na TZS 5000.
Jumla ya washindi wanne,Issa Ali (Dodoma), Elia Massawe (Moshi), Lawi Dennis Mkwawa( Dar es Salaam) na Imaya Ramadhani (Dar es Salaam) wameibuka na simu janja, leo asubuhi katika droo ya Tatu ya AFKON, Ushindi ni SportPesa.
Droo hii ni sehemu ya promosheni ya AFKON, Ushindi ni SportPesa iliyoandaliwa na SportPesa katika msimu huu wa AFKON, na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zinatolewa kila siku kwa washindi 100 ambao hujishindia kiasi cha TZS 5,000.
Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa Makao Makuu ya SportPesa, Jijini Dar-Es-Salaam, Afisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Lydia Solomon anasema leo ni droo yetu ya tatu ya AFKON, Ushindi ni SportPesa ambapo wateja wa SportPesa wamejishindia Simu Janja.

‘’Kama mnavyofahamu leo imechezeshwa droo yetu ya tatu ya AFKON,Ushindi ni SportPesa ambapo wateja wanne kutoka Moshi, Dodoma na Dar es Salaam, wameshinda simu janja, baada ya kubashiri na na kuibuka washindi wa AFKON, Ushindi ni SportPesa, Tunaendelea kuwahimiza wateja wetu kuendelea kucheza na SportPesa ili waweze kujishindia zawadi hizi kwenye msimu huu wa AFKON.
Kampeni hii inalenga kuwazawadia wateja wote wa SportPesa kupitia mitandao yote ya Airtel, Vodacom,Halotel na Tigo. Na hadi kufikia leo tumewazawadia wateja zaidi ya 2500 fedha taslimu na 10 wamejishindia simu janja, wiki ijayo tunaenda kuchezesha droo yetu ya mwisho ambapo washindi 5 wataondoka na simu janja.
Ili kuweza kushiriki mteja anatakiwa kuweka TZS 500 kwenye akaunti yake ya SportPesa na kisa kuweka ubashiri wake, kwa kufanya hivyo atakuwa ameingia kwenye droo ya kuweza kujishindia fedha taslimu Pamoja na simu janja”.
Ili kuweka bashiri yako,wateja wanaweza kupiga *150*87#, kutembelea tovuti yetu ya www.sportpesa.co.tz au kudownload APP yetu ya SportPesa.
