Mkazi wa Mbagala, Jumanne Hamisi Kape, ameshinda Tshs 8,154,788 kama bonus ya Jackpot ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.
Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, Jumanne anasema alianza kucheza na Sportpesa zaidi ya mwaka na nusu. ‘’Nilianza kucheza na Sportpesa mwaka 2022, na nimekuwa nikishinda kiasi tofauti kama laki 5, laki 2, laki 3, na pia nimeshawahi kushinda zaidi ya mara 8 kwa kupatia timu 10.

SportPesa nimeifahamu muda mrefu, lakini kuna Rafiki yangu ndio alinishawishi nianze kucheza na alinifundisha na mimi ndio nilipoanza kucheza. nilivutiwa na Sportpesa, baada ya kuona kiwango cha bonasi za Sportpesa ni kikubwa kuliko makampuni mengine na pia unaweza kucashout, nakumbuka wiki chache zilizopita niliweka mkeka wa timu 24 na nilikuwa nasubiria timu moja tu ilikuwa inacheza, niliamua kucashout na nikapata shilingi milioni 2 na laki 3.
Aliendelea kwa kusema huwa anachukua zaidi ya masaa mawili kupanga mkeka wake.
‘’Mimi napenda ktumia muda mwingi sana kuangalia kwanza timu na kuzichambua kabla sijaweka mkeka wangu, mara nyingi huwa natumia live score baada ya hapo ndio huwa naingia SportPesa na kuanza kubeti. Mara nyingi huwa naweka mikeka 50.
Akiongelea kuhusu ushindi alioupata, Jumanne alisema kama angeweza kupata timu moja iliyomkosesha,alikuwa anaenda kupata mikeka tisa ya timu 10.

Mimi nilicheza Jackpot ya mechi 13 ambayo niliona naiweza. Nilibahatika kupata mechi zote na kukosa mechi moja. Alisema Jumanne.
Jumanne anawashauri watanzania wasisite kucheza kwa wingi kwani Jackpot ya Sportpesa imeboreshwa na kukupa unafuu katika uchaguzi ucheze Jackpot yenye timu ngapi. ‘’Nawaomba muitumie fursa hii kwani ndio njia ya uhakika kulamba mkwanja kama mimi’’.
Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atawekeza kwenye biashara zake makazi yake ambayo anajenga na pia kidogo kitakachobaki ataongezea mtaji kwenye biashara yake..
Naye meneja uhusiano na Mawasiliano Sportpesa Sabrina Msuya alimpongeza Jumanne kwa ushindi wake na kuwaasa watanzania waendelee kuiamini na kucheza na Sportpesa kwani wanaweza kushinda kama Jumanne. ‘’Niwakumbushe tu watanzania kuwa tuna bidhaa zetu za Jackpot ya katikati ya wiki, Supa Jackpot na michezo ya Casino ambazo zinawapa nafasi watu kuwa mabilionea, bila kusahau tunatoa pia bonus ya hadi 1000%
