Ikiwa ni wiki nyingine tena, ambapo SportPesa na Tigo pesa kupitia kampeni yao ya Maokoto Deilee wameendelea kutoa washindi wa simu janja na milioni 1.
Washindi hao walipatikana katika droo ya nne iliyofanyika makao makuu ya ofisi za SportPesa jijini Dar es salaam, Ally Mbwana na Ibrahim Athumani walifanikiwa kujishindia simu janja, wakati Oden Jaston (Dodoma) alijishindia kiasi cha shilingi 1,000,000.

Droo hii ni muendelezo wa promosheni ya Maokoto Deilee ya SportPesa na Tigo pesa ambayo inawapa fursa wateja wa Tigo pesa na SportPesa kujishindia zawadi mbalimbali.
Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa makao makuu ya ofisi za SportPesa jijini Dar es salaam, Lydia Solomon kutoka kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano SportPesa amesema leo imechezeshwa droo ya nne, na zimebaki takribani wiki 2 kumalizika kwa droo ya Maokoto Deilee. Ambapo wateja wa SportPesa na Tigo pesa wameendele kujishindia simu janja na kitita cha shilingi milioni moja.
“Tunasisitiza kwa wateja wetu kuendelea kubashiri na Sportpesa kupitia mtandao wa Tigo (Tigopesa), wakiweka fedha zao kupitia mtandao wa Tigo wanao uwezo wa kubashiri michezo mbalimbali kupitia Sportpesa,” amesema Solomon.
Mwakilishi wa Mtandao wa Tigo, Afisa Biashara, Fabian Felician amewahimiza wateja mbalimbali kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia tigopesa huku akisisiza kuwa wataendelea kutoa zawadi za fedha na simu janja kushirikiana na Sportpesa.
Promosheni ya Maokoto Deilee kila siku inatoa kiasi cha shilingi Elfu Ishirini (Tsh. 20,000/-) kwa wateja wanaobashiri na Sportpesa kupitia Tigopesa, kila wiki inatoka Simu janja (smartphone) na shilingi Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) na kubwa kuliko ni Tsh. 15,000,000/-.
