Jumla ya washindi watatu, Muhamedi Watege (Kigoma), Fidelis Komba (Dar es salaam), wameibuka na simu janja, wakati Salmin Ahmad (Mtwara) amejishindia shilingi 1,000,000, leo asubuhi katika droo ya kwanza ya wiki ya Maokoto Deilee kutoka Tigo pesa na SportPesa.
Droo hii ni sehemu ya promosheni ya Maokoto Deilee iliyoandaliwa na SportPesa kwa kushirikiana na Tigo Pesa, na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zinatolewa kila siku kwa washindi 10 ambao hujishindia kiasi cha TZS 20,000.
Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa kwenye viwanja vya karume, Jijini Dar-Es-Salaam, Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya anasema leo imechezeshwa droo ya kwanza katika wiki ya kwanza ya Maokoto Deilee ambapo wateja wa Tigo pesa na SportPesa wamejishindia simu janja na shilingi milioni 1.

‘’Kama mnavyofahamu leo imechezeshwa droo yetu ya kwanza ya wiki ya kwanza ya Maokoto Deilee, ambapo wateja watatu kutoka Kigoma, Mtwara na Dar es salaam, wameshinda simu janja na shilingi milioni moja kwa mmoja, baada ya kubashiri na na kuibuka washindi wa Maokoto Deilee ya Sportpesa na Tigo pesa.
Akiongea kwa niaba ya Tigo, Meneja Biashara wa Tigo pesa, Fabian Felician alisema wachezaji wa SportPesa ambao wanatumia laini za simu za Tigo hawana budi kuiga mfano wawenzao ambao wameshinda kwa kucheza na kuingia kwenye droo ili na wao washinde.

‘’Ninapenda kuwahamasisha watanzania wenzangu hususani wateja wetu wa Tigo pesa kuchangamkia fursa hii. Mmoja wa washindi wa leo Salmin Ahmad ameshinda milioni moja hivyo basi iwe chachu kwa wengine kushiriki kadiri wawezavyo.
Ili kuweka bashiri yako kupitia TigoPesa, wateja wanaweza kupiga *150*87#, kuchagua namba 4, na kuweka kiasi anachotaka, kisha kuweka PIN yako ya Tigopesa ili kukamilisha muamala.
