SupaJackpot bonus winnerHamisi

Unaweza ukasema bahati haina mwenyewe. Hivi ndivyo usemi huu ulivyotimia kwa Hamisi Kassimu Ndingo, mkazi wa Kijichi, Wilaya ya Temeke, Dar-Es-Salaam. Mshindi huyu ni mmoja wa wachezaji wengi wa kitanzania wa bonasi ya Supa Jackpot ya SportPesa, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 15 kati ya 17, akijishindia Tsh 5,908, 578.

Akizungumza katika ofisi za Sportpesa Hamisi anasema alianza kucheza na SportPesa miaka mitatu iliyopita, baada ya kuwa anawaona washikaji zake wanacheza na kushinda vitita vya multibet na Jackpot za SportPesa.

‘’Mimi nilianza kucheza na SportPesa kuanzia mwaka 2020 wakati ule nikiwa bado hapo maeneo ya Mtoni Kijichi. Nilikuwa nawaona washikaji zangu wanacheza na kushinda na SportPesa.

Sana sana nilikuwa nawaona siku za wikiendi nawakuta vijana wako bize na simu zao wakibashiri na SportPesa.

Sasa mimi nikawaomba wanifundishe na walikubali na kunifundisha. Nilianza mdogo mdogo nikicheza timu mbili tatu hadi nilipoweza kucheza kuanzia timu nane mpaka timu kumi.

Hamisi anaendelea kuelezea tangu amejifunza na kujua kucheza na SportPesa, amewahi kushinda mara moja, kabla ya ushindi huu wa sasa wa Supa Jackpot bonus.

‘’Kwa bahati nzuri toka nimeanza na kujua kucheza nilibahatika kushinda Tsh 18,000 mara moja katika multibet. Ushindi huu ulinipa moyo sana na kunifanya kuendelea kucheza hata kama baadae nilikuwa sikushinda chochote.

Sikuruhusu kukata tamaa, kwani niliamini kama watu wengine walikuwa wanashinda basin a mimi ninanafasi saw ana wao ya kushinda hivyo niliendelea. Safari hii nilianza kucheza zaidi Jackpot za SportPesa.

Unajua katika kucheza michezo hii kuna maneno mengi. Mengine ya kutia moyo na mengine ya kukatisha tamaa. Unaweza kutana na watu na wakijua unabashiri, basi wataanza kukwambia maneno ambayo yatakukatisha tamaa. Mimi sikukata tamaa niliendelea kucheza na matokeo yake ndio haya nimeshinda Supa Jackpot bonus.

Kuhusu mkeka wake wa bonus alioshinda Hamisi Kassimu ndingo anasema yeye huwa na kawaida ya kucheza Jackpot zote mbili za SportPesa, akimaanisha Mid-Week na Supa Jackpot. Kila mwanzo wa wiki huwa naangalia mechi za Jackpot kupitia simu yangu janja, ila wakati wa kucheza nacheza kwa kutumia simu ya tochi au kiswaswadu.

‘’Mimi huwa na kawaiada kila Jumatatu na Ijumaa kuingia mtandaoni na kutizama kama mechi za Jackpot zimetoka au la. Ikiwa zimetoka basi hujitahidi ifikapo usiku wakati nimemaliza shughuli zangu, napitia mechi moja moja kisha naweka mkeka wangu wa Jackpot’’.

Hamisi akiangalia sms yake ya ushindi wa Supa jackpotAnaelezea kwamba aliweka mkeka huu ulioshinda siku ya Jumamosi ya wiki ile iliyokwisha kabla ya saa kumi na moja jioni.  Aliweka jumla ya mikeka miwili, mmoja ukiwa wa multibet na mwingine ndio huu wa Supa Jackpot ulioshinda’’.

Anaendelea kusema kwamba baada ya mechi za Jackpot kuanza alipata mechi moja na kukosa mechi moja. Baada ya hapo alipata ya 3 na ya 4 na kukosa ya 5. Nilipata mech izote zilizofuatia katika Supa jackpot.

Anasema kabla ya ushindi anachokumbuka yeye ni kuangalia matokeo ya mechi namba 16 kati ya mechi 17 za Supa Jackpot. Hii ndiyo ilikuwa mechi ya mwisho kwa mimi kuipatia matokeo yake, hivyo kupelekea kushinda jumla ya mechi 15 kati ya 17 za Supa jackpot.

‘’Sikuwa na muda wa kufuatilia sana matokeo kutokana na ubize katika eneo langu la kazi, kwa kuwa kulikuwa na wateja wengi siku hiyo ya Jumamosi. Kuna sms iliingia mida ya saa saba kama na dakika 20 za usiku.

Baada ya kumaliza kazi za usafi nikiwa nafunga kazi niliamua kutizama simu na kukutana na habari njema ya ushindi kupitia sms kutoka SportPesa.

Kwa muda ule nilifurahi sana na kuduwaa kidogo. Si unajua pesa hii kwa sisi wa uswahilini ni nyingi kidogo. Nilijaribu kutoa pesa nikashindwa hivyo nililala mpaka asubuhi na kuwasiliana na watoa huduma kwa wateja wa SportPesa ambao walinielekeza nahitaji kuja ofisi za SportPesa kwa ajili ya uhakiki na kukabidhiwa mfano wa hundi.

Nashukuru mtoa huduma kwa wateja alinielekeza vizuri, hivyo kupelekea mimi kuja hapa ofisi za SportPesa kwa ajili ya uhakiki na taratibu za ki utawala.

Akimpongeza mshindi Hamisi Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimtaka Hamisi kuendelea kucheza na SportPesa bila kukata tamaa kwani anaweza katika siku za mbeleni akawa mshindi wa Jackpot yenyewe au akaendelea kushinda bonasi kama hii aliyoshinda.

‘’Kwanza nimpongeze Hamisi kwa kufanikiwa kushinda bonasi ya Supa Jackpot, vile vile nitoe rai kwake aendelee kucheza hizi Jackpot bila kukosa kwani kila mchezaji ana nafasi sawa katika kushinda zawadi zetu, iwe kiwangu kikubwa au kiwango cha kawaida.

Cha mwisho ni kuwakumbusha watanzania kuendelea kucheza na SportPesa kwani mkwanja upo wa kutosha na bidhaa za kukupa mikwanja zipo. Unaweza cheza Jackpot zote mbili, unaweza cheza michezo ya Kasino kama Aviator na Virtual Football Pro au multibet ambayo ina bonasi ya mpaka asilimia 1000 ya ushindi ambao utaupata.

Supa Jackpot yetu wiki hii imesimamia TZS 1,131,423,064.

 

 

 

Share this: