Mfano-wa-hundiMfano-wa-hundi

Kampuni ya burudani na michezo ya kubashiri SportPesa leo jijini Dar-Es-Salaam imekabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 405 kwa timu ya Yanga, ikiwa ni bonasi baada ya kutawazwa kuwa mabingwa kwenye mashindano mbalimbali ya msimu wa mwaka 2022/2023.

Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa na wawakilishi kutoka klabu ya Yanga, wadhamini wa kuu wa klabu hiyo SportPesa, wadau mbalimbali wa michezo pamoja na waandishi wa habari.

Akiwakaribisha waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya aliwapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa na kwa mafanikio waliyoyapata msimu huu, ambapo wameweza kushinda taji la ligi kuu bara NBC premier League, Kombe la Shirikisho ASFC na Ngao ya Jamii.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano SportPesa, Sabrina Msuya‘’Nianze kwa kuwashukuru ndugu waandishi kwa kufika, lakini kipekee niwapongeze timu ya Yanga kwa kuweza kufanya vizuri katika msimu huu wa ligi. Nafikiri kila mmoja wetu anajua kile ambacho mmefanya na kwa heshima na taadhima niwape hongera viongozi, wachezaji pamoja na benchi la ufundi”.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza uongozi wa Yanga kwa kuhakikisha wanawaongoza vyema wale walio nyuma yao ili kuhakiksha wanapata mafanikio mengi zaidi kwa misimu mingine ijayo.

“Klabu ya Yanga safari hii imepata viongozi bora na kwa mafanikio haya kila mtu anajionea maana ni mwendo wa makombe tu kila msimu, kwa misimu miwili mfululizo, ni matumaini yangu ushindi huu utakuwa endelevu”,

Mh Tarimba aligusia pia kwamba anaona safari ya mafanikio kwa Yanga ndio imeanza kwa kuwa sasa wana uongozi imara wenye maono na malengo mazuri yanayotekelezeka na yatakayoipeleka mbali klabu hiyo kimaendeleo.

Álisifu kwa namna ambavyo Yanga inaendeshwa kwa kisasa zaidi, akisema yeye mwenyewe kama mjumbe wa bodi amesafiri na timu kwenye mechi kadhaa kuanzia ile ya DRC kati ya TP Mazembe na Yanga, kisha akaenda na ile mechi waliyocheza fainali na USM Alger.

Mkurugen wa Sportpesa Tarimba Abbas.Anaendelea kusema kama sio uhuni ambao mashabiki wa USM Alger walikuwa wamefanya katika mechi ile, basi Yanga leo angekuwa ni bingwa wa Africa katika kombe la Shirikisho”.

Akimalizia Tarimba aliahidi SportPesa itaendelea kutoa ushirikiano kama ambavyo matakwa ya kimkataba yanavyotaka na pia aliwatakia kheri katika msimu unaokuja akitarajia makubwa zaidi.

“Ni Faraja yetu sisi kama wadhamini wakuu kuona mnaitendea haki nembo ya SportPesa kwa miaka 6 mfululizo. Leo tunatimiza jukumu la kimkataba kwa kuwapa bonasi ya shilingi Mil. 405 kutokana na kujituma kwenu ili iwe kama motisha kwa mashindano yajayo kuelekea msimu wa mwaka 2023/24.”

Akiongea kwa upande wa Yanga, Raisi wa klabu Hersi Saidi alianza kwa kuwashukuru SportPesa kwa namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na klabu kama mdhamini mkuu katika kutekeleza mipango na majukumu ya kila siku.

“Nichukue nafasi hii kuishukuru SportPesa kwa kutekeleza kwa wakati makubaliano yaliyopo kwenye mkataba na kwa kutoa bonasi ya Sh. 405,000,000 baada ya klabu yetu kupata mafanikio makubwa msimu huu

Aliendelea kwa kusema pesa za kimkataba wanazopata Yanga kutoka SportPesa zimegawanyika katika makundi mawili. Moja ni pesa ya ufadhili  ambayo ina kiwango kisichobadilika ambacho Yanga anapokea kila mwezi.

Pesa ya pili ambayo Yanga inapokea kutoka kwa mdhamini ni pesa inayotokana na mafanikio ya timu katika msimu husika. Sasa hii ndio sababu ya leo tuko hapa kupokea mfano wa hundi wa hela hii. Hizi 405,000,000 ni bonus kutokana na namna tulivyofanya vizuri katika msimu huu.

“SportPesa imekuwa ikitoa bonasi kila tunapofanya vizuri, kwa moyo mmoja, na niseme tu wao ndio chachu ya mafanikio yetu na tunajivunia sana tunavyoona tunatendea haki nembo yao kwa kuwapa ushindi mfululizo

Eng Hersi alichukua nafasi hiyo kutupilia mbali minongóno kwamba Yanga na SportPesa hawana uhusiano mzuri  na kwamba inawezekana hawashirikiani katika shughuli ama matukio mbali mbali ambzo Yanga anafanya.

Rais wa Yanga Eng. Hersi”Naomba niwathibitishie kwamba SportPesa bado ni mdhamini mkuu na kwamba tunaendelea na ushirikiano wetu kama ilivyokuwa awali. Ni kweli kulitokea kutoelewana kuhusiana na ushiriki wetu wa CAF katika hatua ya makundi, lakini tulishakaa tukaongea yakaisha”.

Eng Hersi alimalizia kwa kusema anashukuru anapokea cheki hii siku ya leo ikiwa ni mwaka mmoja kamili tangu alipoingia rasmi Yanga kama Raisi wa klabu.

Niwashukuru nyote kwa ushiriki wenu katika tukio la leo na pia napenda kusema ni faraja kwangu kuwa napokea cheki hii ikiwa nimetimiza mwaka mmoja kamili katika Tarehe na siku kama ya leo.

 

 

 

Share this: