Tarimba na Sabrina Msuya wakiwakilisha Sportpesa wakati John Kadutu na Tabitha Kidawawa wakiwakilisha Singida Fountain Gate.SP-Fountain-Gate-Dummy-Cheque

Kampuni ya burudani na michezo ya ubashiri SportPesa, leo asubuhi imekabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 50, kwa timu ya Singida Fountain Gate FC, baada ya kushika nafasi ya nne katika ligi kuu bara NBC premier League, msimu wa 2022/2023.

Waliohudhuria kutoka SportPesa ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Sabrina Msuya. Kutoka Singida Fountain Gate FC alikuwepo Makamu wa Rais utawala na fedha John Kadutu na Mkurugenzi wa Masoko Tabitha Kidawadawa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Singida Fountain Gate FC kwa hatua waliopiga katika msimu huu uliokwisha kwa kuonyesha ni kwa jinsi gani walidhamiria kupata mafanikio au kufika mbali kisoka.

“Napenda kuwapongeza viongozi na wachezaji wa Singida Fountain Gate FC kwa mafanikio ambayo mmeyapata, kwani mmewapa heshima kubwa wana Singida kwa ujumla wao popote pale walipo.

Kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi wadhamini wenu wakuu kwa namna mlivyoweza kupigania chapa yetu kwa namna ambavyo mlijipambanua uwanjani, kama washindani wa kweli na si washiriki.

Singida Fountain Gate“Nafasi hii ya nne mliyoishika ni fursa kwa timu yenu kucheza vizuri zaidi kwenye msimu mpya unaokuja, na pia ni ishara nzuri kwani mnaweza kupambana na kupanda nafasi mbili za juu na pengine hata kuchukua ubingwa”.

Nachukua pia fursa hii, kuwapongeza kwa kufanikiwa kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa, ya kombe la Shirikisho barani Afrika, msimu unaoanzia 2023/2024.

Akiongea kwa upande wa Singida Fountain Gate FC, Makamu mwenyekiti John Kadutu alianza kwa kuwashukuru kwa kufuata matakwa ya kimkataba walioingia na kusema kitendo cha kukabidhi bonasi ya Milioni 50 tena kwa wakati ni chachu ya wao kujituma msimu ujao

“Nichukue nafasi hii kuipongeza SportPesa kwa kufuata kila kipengele cha makubaliano yaliyopo kwenye mkataba huu kwa kutoa bonus ya Sh. 50,000,000 kama timu itaingia tano bora katika ligi ya msimu husika, kwa kipindi cha miaka 4 toka msimu wa mwaka 2022/2023.

Jambo hili limekuwa na tija hivyo kuamsha morali ya wachezaji na watendaji katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuipigania klabu kufanya vizuri.

Nichukue nafasi hii kwa mara nyingine kuwashukuru SportPesa kwa kutujali na kuwa karibu na timu yetu pale ambapo tunahitaji msaada wenu’’. Alisema John.

Akimalizia Kadutu aliahidi timu ya Singida Fountain Gate itajitahidi kupanda ngazi msimu ujao na kufika japo nafasi tatu za juu.

Timu ya Singida Fountain Gate zamani singida Big stars imemaliza msimu wa ligi ya NBC premier League 2022/2023 kwa kishindo baada ya kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara.

Timu hii ilifanikiwa kumaliza ikiwa na jumla ya pointi 55, pointi 33 nyuma ya bingwa Yanga ambaye wamemaliza msimu na pointi 78, wakifuatiwa na Simba ambaye ameshika nafasi ya pili akiwa na jumla ya pointi 73. Nafasi ya tatu imekwenda kwa Azam FC ambao wao wamemaliza ligi wakiwa  na junla ya pointi 59, alama nne kutoka alama za Singida Fountain Gate.

Singida Fountain Gate and SportPesaKwa ufupi takwimu za Singida Fountain Gate kwa msimu ulioisha zinaonyesha, ukiachia pointi 55, Wachezaji Bruno Gomez amemaliza msimu akiwa na magoli 10, wakati mshambuliaji Meddie Kagere amemaliza msimu akiwa na magoli nane.

Kwa idadi hiyo ya magoli Gomeza ni sawa amemaliza msimu vizuri kwani amekuwa wa 3 kitakwimu za jumla sawa na mchezaji wa Simba Moses Phiri, lakini akiwa chini ya Prince Dube mwenye magoli 12.

Kwa upande wa SportPesa, hii ni kampuni ya ubashiri inayoongoza katika eneo la kutoa washindi wakubwa na wadogo katika tasnia ya ubashiri kupitia bonus za Jackpot ya katikati ya wiki pamoja na bonus za Supa Jackpot, Multibet bonus, bet spinner na michezo ya kasino kama Aviator, Buffalo King megaways, Cash Patrol na Spaceman .

SportPesa  ndio kampuni pekee Tanzania inayodhamini timu tatu za ligi kuu Tanzania bara. Timu ni pamoja na Singida Fountain Gate, Namungo FC na Yanga SC.

 

Share this: