Leo, Tarehe 24 Aprili 2023, katika dimba la Gewiss, maarufu kama Bergamo, kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka, kati ya wenyeji Atalanta, ambao watakipiga dhidi ya AS Roma, ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu ya Italia.
Atalanta maarufu kama La Gea ni moja ya klabu sumbufu sana kwa takribani misimu mitatu iliyopita na ilitishia nafasi ya wakubwa katika Serie A wakichagizwa na nyota wake kama Duvan Zapatta,Luis Muriel,Mario Pasalic,Marten de Room,Hanse Hateboer na wengine waliunda kikosi cha dhahabu kilichotikisa nchini Italia na hata kwenye Ligi ya mabingwa Ulaya.
Wanakutana na AS Roma inayonolewa na Kocha machachari,Jose Mario Dos Santos Mourinho ambaye tangu ujio wake amejaribu kuirejesha heshima yao iliyopotea kwa muda kidogo ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu na kuiwakilisha Italia katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya kama ambavyo ilizoeleka misimi mingi iliyopita.
Hakuna asiyekumbuka mabalaa ya mastaa kama Francesco Totti,Gabriel Batistuta,Danielle De Rossi,Edin Dzeko,Phillipe Mexes,Milarem Pjanic,Cristian Pannuci,Mirko Vucinic,Kostas Manolas,Allison Becker ,Mohamed Sala na wengine wengi walipita kwenye Klabu hiyo na waliifanya kuwa shindani Ulaya lakini nyakati zinasogea utawala wa Juventus ,Inter Milan,AC Milan na sasa Napoli walitishia nafasi ya AS Roma.
Ujio wa Mourinho umeamsha kitu kipya kuanzia kwa timu na wachezaji na sasa wanakaribia kurejea kwenye Klabu bingwa iwapo watazichanga nyema karata zao kwa mechi 8 zilizosalia wakianzia kwenye mchezo wao dhidi ya Atalanta Bergamo April 24 ,2023.
Kiwango bora msimu huu umeshuhudia viwango bora kwa wachezaji kama Andrea Belloti,Stephane El Shaarawy,Leonardo Spinazzola ,Nemanja Matic na wenzake wakichagiza matokeo mazuri ya sasa ndani ya kikosi hicho.
Kumbukumbu za mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Stadio Olimpico,AS Roma ilitandikwa na Atalanta kwa bao 1-0 hivyo mchezo huu wa marudiano ni wa kisasi lakini pia ni wa muhimu zaidi kukusanya alama ili waendelee kujizatiti kwenye nafasi nne za juu kwani hivi sasa wapo nafasi ya 3 katika msimamo wakiwa na alama 56 .
Ushindi kwao utawafanya waisogelee Lazio yenye alama 61 lakini pia utawafanya waikimbie AC Milan yenye alama 53 na Inter Milan walio katika nafasi ya 5 wakiwa na alama 51 wakati Atalanta watahitaji alama 3 ili wafikishe alama 52 ambazo zitawashusha Inter Milan lakini wataendeleza kufufua matumaini ya kumaliza kwenye nafasi 4 za juu na kurejea kwenye Ligi ya mabingwa msimu ujao.
Takwimu zinaongea kwenye mchezo wa mpira wa miguu na ndizo zinazotupa uhalisia wa hali ya timu ilivyo tukianza na Atalanta wao wamecheza michezo 30 ya Serie A, wameshinda michezo 14, sare 7 na wamefungwa mara 9.
Wakiwa nyumbani vijana wa Kocha Gian piero Gasperini wamekuwa na matokeo mchanganyiko wakiwa nyumbani wameshinda michezo 6 pekee katika michezo 14, wakitoa sare 3 na kupotea mara 5, huku huko ugenini wamecheza jumla ya michezo 16,wameshinda mara 8,sare mara 4 ,wamepoteza mara 4 na kujikusanyia jumla ya alama 49,wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Serie A.
Tukiwamulika AS Roma wanaonolewa na Kocha, Jose Mourinho wapo kwenye kiwango kizuri sana msimu huu na hadi sasa wapo nafasi ya 3 kwenye msimamo wakiwa na alama 56 baada ya ushindi wa mechi 17 kati ya 30 walizocheza,wamepoteza mara 8 na sare 5.
Rekodi ya AS Roma wakiwa nyumbani wamecheza mechi 15, wameshinda mechi 10, sare 1 na kupoteza mara 4 lakini wakiwa ugenini wamecheza mechi 15, wameshinda michezo 7, sare 4 na wamepoteza mara 4.
Tukirejea kwenye mechi walizokutana kati ta 42 kwenye mashindano yote Atalanta imeshinda mara 13 wakati AS Roma imeshinda mara 20 huku michezo 9 ikimalizika kwa sare huku kila mchezo ukiwa na wastani wa kuzalisha wastani wa mabao 3.05.
Katika Serie A timu hizi zimekutana mara 32, AS Roma imeibuka mbabe kwa kushinda mara 15 na Atalanta wameshinda mara 10, sare 7, AS Roma ikifunga mabao 53 wakati Atalanta wamefunga mabao 48.
Kwa mujibu wa takwimu kuelekea mchezo huo AS Roma wana asilimia 46.9 wakati wenyeji Atalanta wana asilimia 31.3 ya ushindi katika mchezo huo hivyo kwa wakali wa kubashiri unaweza kufanya maamuzi sasa kupitia Sportpesa.
Katika mechi 5 za mwisho kwenye Serie A,Atalanta imeshinda mara 2 tu,ikipoteza mara 2 na sare 1 wakati AS Roma imeshinda michezo mitatu mfululizo ya mwisho lakini imepoteza miwili ya mwanzo kati ya mitano iliyopita.
Atalanta iliwahi kucheza takribani michezo 10 bila kupoteza wakati AS Roma walicheza michezo 6 bila ya kupoteza,na katika michezo yote 30,Atalanta ilishindwa kufunga bao hata moja katika michezo 6 tu wakati AS Roma ilishindwa kufunga bao katika michezo 5 tu,tafsiri yake timu hizi zina wastani mzuri wa kufunga bao katika kila mchezo.
As Roma imefunga mabao kuanzia mawili na kuendelea katika michezo 12 wakati Atalanta imefanya hivyo katika michezo 13.
Mfungaji bora wa AS Roma ni Paul Dyabala mwenye mabao 11 akifuatiwa na Tammy Abraham mwenye bao 9 wakati kwa upande wa Atalanta kinara wa mabao ni Ademola Lookman aliyecheka na nyavu mara 13 akifuatiwa na Rasmus Winther mwenye mabao 7.
Ili kubashiri mechi hii kati ya Atalanta VS Roma tembelea tovuti yetu sportpesa.co.tz au piga *150*87#

