KATI YA SIMBA NA YANGA NANI KUSONGA MBELE KIMATAIFA?
Ikiwa ni masaa machache kabla ya kipenga cha michezo kati ya Simba na Horoya kupulizwa, vuguvugu mtaani limekuwa ni timu gani kati ya Yanga na Simba, itakayoweza kupenya hatua hii ya makundi na kusonga mbele kwenye mechi za robo fainali.
Simba ambayo leo alasiri, itakuwa dimbani katika uwanja wa Benjamini Mkapa, inahitaji ushindi tu ili iweze kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali, ya kombe la klabu bingwa Africa.
Kwa namna hesabu zilivyokaa katika kundi C ambapo Simba yupo, Raja Athletic Club ameshafuzu na anacheza mechi zake kukamilisha ratiba, hivyo, hana presha ya ushindi, wakati timu ya Simba na Horoya, zote kwa pamoja, zinautaka ushindi wa leo kwa udi na uvumba, ili ziwe kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Timu ya Simba ina pointi 6, baada ya kucheza mechi nne akipoteza mechi mbili na kushinda mechi mbili, wakati Horoya wao wana point 4, wakiwa wameshinda mechi moja, kutoa Sare moja, na kufungwa mechi mbili.
Kwa mtazamo wa kimahesabu ili Simba aweze kufuzu ni lazima ashinde mechi zake zote mbili, au ashinde moja, huku akiomba timu ya Horoya itoe sare au kufungwa mechi zake zote mbili, ikianzia hii anayocheza na Simba leo kabla ya kwenda kucheza mechi ya mwisho na timu ya Vipers ya Uganda, ambayo inashika mkia ikiwa na pointi moja tu.
Kwa upande wa Yanga wao watacheza na timu ya US Monastir, ya Tunisia, ambayo tayari imeshatua tangu siku ya Ijumaa, Tarehe 17 Machi 2023, kwa ajili ya mchezo wao wa kombe shirikisho, unaotarajiwa kuchezwa hapo hapo katika uwanja wa Benjamini Mkapa, siku ya Jumapili 2023.
Yanga nayo, kama ilivyokuwa kwa mahasimu wao Simba, wanahitaji alama tatu muhimu kwenye mchezo wake siku ya kesho, ili waweze kuweka rekodi ya kutinga hatua ya Robo Fainaili, ya kombe la shirikisho.
Katika kundi lao, Yanga SC wanashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo, nyuma ya US Monastir wenye alama 10, Yanga SC 6, Mazembe alama 3, Bamako alama 2.
Hata hivyo, Yanga SC wanashikilia rekodi pekee ya kushiriki hatua ya makundi mara nyingi zaidi (3) 2016, 2018, na 2022 kwa vilabu kutoka Tanzania na endapo watafika hatua ya Roba fainali basi watakuwa klabu ya pili kufikia hatua hiyo baada ya watani wao wa jadi kufanya hivyo msimu uliopita.
Raisi wa Klabu ya Yanga SC Eng Hersi Said amesisitiza kuwa klabu yake ina malengo na matarajio makubwa kwenye mtanange wa kesho.
“Nina imani Yanga SC itakuwa timu ya Kwanza kutoka Tanzania kutwaa Kombe la CAF. Nina Imani siku ya kesho, tuna asilimia kubwa za kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya kombe la Shirikisho. Nina hakika tuna timu nzuri na tuna nia thabiti ya kuvuka na kwenda nusu fainali na hata Fainali.
Niwahakikishie Wananchi msiwe na hofu wala wasiwasi, tujitokeze kwa wingi” alisema Eng Hersi
Kwa upande wa nahodha msaidizi Dickson Job amewasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa wachezaji hamasa
“Sisi kama wachezaji tunahitaji mchango mkubwa sana kutoka kwa mashabiki, bila wao ushindi wa michezo iliyopita hautakuwa na maana yoyote kama tutashindwa kushinda mchezo ujao” alisema Job
Fiston Mayele ndiye mchezaji tegemeo kwenye kikosi hiki cha wana jangwani akiwa amefunga magoli 15 kwenye ligi pamoja na magoli 9 kwenye mashindano ya kimataifa. Kikosi cha Yanga kipo tayari kwa ajili ya kukabiliana na US Monastir, ambaye katika raundi ya kwanza alishinda goli 2-0.
Kwa vyovyote itakavyokuwa wapenzi na mashabiki wa timu hizi mbili wote wana imani timu zao zitafanya vizuri na kuwakilisha vyema nchi, kama ambavyo tayari wameshafanya. Nimatumaini yetu kama wadau wa tasnia ya michezo kuona timu hizi zikifika mbali.
Kama kawaida yetu SportPesa tumewawekea mechi zote mbili katika tovuti yetu, pamoja na mechi nyingine za ligi ya klabu bingwa Afrika zinazocheza leo, na timu za kombe la shirkisho zinazocheza kesho, pamoja na Yanga.
Kujisajili na kucheza tembelea hapa au piga *150*87#.

