skip to Main Content

Miaka Mitano ya kibabe SportPesa Tanzania!!

Kampuni ya michezo na burudani Sportpesa leo inaazimisha miaka mitano tangu kuanza shughuli zake za michezo ya kubashiri nchini Tanzania.

Akizungumza ofisini kwake, Oysterbay Dar-Es-Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na mtanzania pekee mwanahisa Tarimba Abbas anasema kampuni ya Sportpesa ilianza biashara miaka mitano iliyopita.

“Kampuni hii ya Sportpesa ilianza rasmi shughuli zake Mei, 2017 ikiwa na ofisi yake Oysterbay, Dar-Es-Salaam.

Tangu kuanza kwa kushughuli zake za michezo ya ubashiri na kubahatisha kampuni ya Sportpesa ndani ya miaka 5 imefanikiwa kuwa namba 1 kati ya kampuni zaidi ya 20 zinazojihusisha na shughuli za ubashiri nchini Tanzania.

‘’Kampuni yetu ilianza na uwekezaji mkubwa wa kimtaji ikiwekeza zaidi ya Bilioni 35 kuanzia wakati ule mpaka wakati huu ambapo tunaadhimisha miaka mitano ndani ya ardhi ya Tanzania’’.

Mwenyekiti waBodi ya wakurugenzi SportPesa , Tarimba Abbas akizungumza na waandishi wa habari kwenye mahojiano maalum ya kuadhimisha miaka mitano ya uendeshaji wa shughuli zake Tanzania.

Akizungumzia uzoefu wake kwenye tasnia ya michezo ya bahati nasibu Mh. Tarimba anasema amehudumu serikalini kwa zaidi ya miongo miwili na nusu ambapo alifanikiwa kupata uzoefu wa kutosha kumudu kuongoza kwa mafanikio taasisi ya bahati nasibu Tanzania, Bodi ya michezo ya Kubahatisha na sasa Sportpesa Tanzania.

‘’Mwaka 2002 niliasisi utafiti uliopelekea kuvunjwa kwa shirika la Bahati Nasibu Ya Taifa na kuanzishwa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha. Mimi niliteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa kwanza wa taasisi hiyo ambayo ipo hadi sasa ikiratibu, na kusimamia sheria, kanuni na matakwa ya kiuwekezaji katika sekta ya michezo ya kubahatisha.

Katika miaka yangu yote ya kufanya kazi serikalini nimebahatika kuhudhuria makongamano na mafunzo mbali mbali ambao umenipa msingi na kunijenga kuwa na uzoefu mkubwa ambao umezinufaisha hata nchi Jirani kama Kenya, Uganda, Msumbiji, Ghana, Ethiopia na Malawi.

Hii ilipelekea mimi baada ya muda mrefu wa kuitumikia serikali, ilipofika muda wa kustaafu nilifikiria namna ya kujiunga na kampuni binafsi ambayo ina mipango na weledi kama niliokuwa nayo mimi. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mimi kujiunga na Sportpesa na kuwa mmoja wa washirika wa kibiashara kama mwanahisa pekee ndani ya kampuni hii.

‘’Moja ya jambo ambalo tunajivunia kwa uhakika kabisa ni namna tulivyoweza kukua kwa kiwango cha kuongoza soko kwa asilimia 30. Toka tumeanza tumekuwa tukikuwa katika maeneo mengi moja wapo ni aina za huduma na viwango vya zawadi tunavyotoa, ikienda sambamba na ujumla wa kodi tunazolipa.

Kwa ufupi kwa miaka hii mitano tu, jumla ya kiwango cha fedha za zawadi kwa wachezaji wetu tumetoa Bilioni 434.4, hii ikienda sambamba na kiwango kikubwa kabisa cha zawadi ya washindi wawili wa Jackpot ambao waligawana Milioni 400 na ushehe ambapo mwajiriwa wa Magereza na Muajiriwa wa Jeshi walishinda kila mmoja.

Pia kuna kodi iliyotokana na zawadi za washindi ambapo jumla yake ni Bilioni 63.3 zimelipwa serikalini, Kiasi cha kodi Bilioni 34 kimelipwa kwenye matumizi mengine ya kawaida na shughuli za operesheni za kibiashara za kampuni.

Anaendelea kusema katika kipindi hicho cha miaka mitano Sportpesa imeweza kusaidia udhamini katika maeneo kadhaa katika sekta ya michezo na burudani. Moja ya eneo hilo ni la mpira wa miguu ambapo wamedhamini kwa muda wa miaka mitano.

‘’Kwa upande wa kurudisha kwa jamii tumewekeza kiasi kikubwa sana kwenye udhamini ambapo tulianza na Simba na Yanga baadae tukaenda kwa Singida United na Namungo. Pia katika muktadha huo tuliweza kuwaleta Everton na Sevilla kwa nyakati mbili tofauti, pamoja na wachezaji kadhaa waliowika wa ligi kuu ya Uingereza kama Sol Campbel na viongozi wa timu kama Southampton, Hull City, Arsenal, Everton na watendaji wa ligi ya La Liga ambao kwa pamoja walifanya kliniki kwa ajili ya wachezaji na viongozi wa kitanzania.

Anaongezea kuwa wakati wa maandalizi ya kuwaleta Everton iligundulika eneo la kuchezea na la kubadilishia nguo katika uwanja wa Mkapa hayakuwa katika viwango na ubora unaostahili hivyo ililazimu kuleta wataalamu wa nyasi wa kimataifa toka nje pamoja na waliofanyia maboresho vyumba vya kubadilishia nguo.

‘’Ilitulazimu kudhamini maboresho na matengenezo ya uwanja wa Mkapa ambao zamani ulikuwa unaitwa uwanja mkuu wa taifa. Tulifanya ukarabati wa eneo la kuchezea katika awamu moja wakati wa kuileta Everton ambapo tulifanya ukarabati wa muda mfupi na baada ya hapo tulidhamini usimamizi na maboresho ya nyasi za uwanja kwa miaka miwili tukileta wataalamu waliobobea katika shughuli hizo toka Ireland na Italia’’.

Tarimba anaendelea kusema katika hatua kubwa za udhamini walizozifanya ni Pamoja na kuanzisha mashindano ya Kombe la Sportpesa ama (Sportpesa Cup) lililofanyika mara mbili Tanzania na mara moja nchini Kenya.

‘’Kwa sasa mashindano haya yalisimama kwa muda kutokana na athari za ugonjwa wa uviko 19, lakini mipango bado ipo jikoni tukifanya tathmini ya namna ya kuyarudisha katika siku za usoni pale ambapo mazingira yatakuwa rafiki.’’.

Kuhusu changangamoto ambazo Sportpesa imepitia anasema kiwango cha kodi inayotozwa na serikali ni kubwa hivyo kupunguza wigo wa wachezaji. Anaendelea kusema angependelea kuwe na ubunifu zaidi wa mfumo wa kodi ambao utachochea wachezaji wangi zaidi ili faida iongezeke si tu kwa wao kama kampuni bali hata kwa Serikali

‘’Hapa natolea mfano wa kodi ambayo ilikuwa inakatwa toka kwa wachezaji na kwa kampuni ambayo ilikuwa asilimia 20 kutoka mwezi julai mpaka Desemba 2020. Baada ya kutolewa asilimia tano ya kodi hiyo kumepatikana faida ya mapato bilioni 14 kwa kipindi cha miezi sita yaani mwezi julai mpaka Desemba 2021 ambayo ni asilimia 37 zaidi ya mwaka 2020. Kwa mwaka wa fedha 2021 Julai mpaka mwaka 2022 Juni Serikali ilipanga kukusanya Bilioni 150 na mpaka sasa umebaki mwezi mmoja wameshakusanya asilimia 90 ya mapato waliyotarajia.

Changamoto nyingine ni anaona Serikali inabidi iweke mizania sawa wakati wa kutunga sheria zinazohusiana na michezo ya kubahatisha ili wadau wakuu nao wapewe nafasi inayostahiki katika kusikilizwa kabla sheria hazijapitishwa ama kutungwa.

‘’Hapa naamini pana changamoto ya uelewa wa mazingira halisi ya biashara hii ambapo ni ngumu kwa mtu ambaye hana taaluma ama uzoefu kama wa kwangu kuingia kwa undani kutunga sheria na kanuni zitakazowezesha mazingira mazuri ya kukuza aina hii ya biashara’’.

Tarimba amegusia uwepo wa utitiri wa vyombo ama taasisi za udhibiti zimekuwa nyingi zote zikilenga kupata mapato kwenye eneo moja. Hii inapelekea kampuni kutumia fedha nyingi katika shughuli ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na uzalishaji wa mapato.

Mwisho anamalizia kwa kusema Mipango ya Sportpesa kwa miaka mitano ijayo ni pamoja na kuhakikisha mafanikio waliyoyapata ndani ya miaka hii mitano wanayadumisha na kuyaboresha.

Pili lengo kuu ni la kuendelea kuongoza sekta hii ya michezo ya kubahatisha kwa kusalia kwenye nafasi ya kwanza kama ilivyosasa.

Jambo la tatu ambalo analiona Sportpesa itafanikiwa nalo ni pamoja na adhma ya kuongeza mapato mpaka kufikia zaidi ya asilimia 40 au 50 ya ukubwa wa soko.

Nne kuongeza ajira kwani kadiri wigo wa wachezaji na mtaji utakavyokuwa ndivyo huduma nyinginezo zitakavyohitaji watendaji wa kuzisimamia na kuzitekeleza.

Tano kuongeza thamani ya zawadi ambapo alitolea mfano wa Jackpot yetu ya sasa ambayo ipo zaidi ya Bilioni 1, itakapopata mshindi basi wataongeza Jackpot nyingine kubwa ambayo itavutia zaidi. Ikumbukwe Jackpot inayochezwa sasa hivi inaanzia Milioni 200 na pia inachezwa kwa mechi 13 tu.

Share this:
Back To Top