skip to Main Content
Sportpesa Yakabidhi Hundi Ya Shilingi Milioni 50 Kwa Simba SC.  Ni Baada Ya Kufuzu Katika Hatua Ya Robo Fainali, Kombe La Shirikisho Afrika.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Sportpesa Mheshimiwa Tarimba Abbas akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Mil. 50 kwa Afisa Mtendaji Mkuu Simba SC Barbara Gonzalez kama bonasi ya kufuzu robo fainali ya mashindano ya kombe la shirikisho Afrika. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya, Mchezaji Erasto Nyoni akiwakilisha baadhi ya wachezaji wa Simba(wa pili kulia) akifuatiwa na Ahmed Ally Meneja Habari na Mawasiliano Simba.

Sportpesa yakabidhi hundi ya shilingi milioni 50 kwa Simba SC. Ni baada ya kufuzu katika hatua ya robo fainali, Kombe la shirikisho Afrika.

simba

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika kwenye ofisi za SportPesa ambao ni wadhamini wakuu maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Waliohudhuria kutoka SportPesa ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas, Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sabrina Msuya, kutoka Simba ni Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally pamoja na mwakilishi wa wachezaji wa timu ya Simba Erasto Nyoni.

 

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Sportpesa Mheshimiwa Tarimba Abbas akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Mil. 50 kwa Afisa Mtendaji Mkuu Simba SC Barbara Gonzalez kama bonasi ya kufuzu robo fainali ya mashindano ya kombe la shirikisho Afrika. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya, Mchezaji Erasto Nyoni akiwakilisha baadhi ya wachezaji wa Simba(wa pili kulia) akifuatiwa na Ahmed Ally Meneja Habari na Mawasiliano Simba.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Simba kwa hatua waliyofikia hii inaonyesha ni jinsi gani timu Pamoja na uongozi wake wamedhamiria kufika mbali.

“Napenda kuwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba SC kwa hatua na mafanikio ambayo mmeyapata, kwani mmewapa heshima kubwa wana msimbazi kote nchini. Kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi wadhamini wenu wakuu kwa namna mlivyoweza  kuliwakilisha taifa na kupambana mpaka kufikia hatua hii”

“Hii ni ishara nzuri kwani tuna matumaini kwenye mashindano yajayo mtashiriki kwa kujipanga vizuri zaidi na kufika hatua za mbele zaidi ya mlipofikia, ili kutimiza lengo lenu kama timu”.

Aliendelea kwa kufafanua kuhusu kiasi hicho cha pesa ambacho SportPesa imekabidhi kwa Simba kwa kusema;

Simba imeitendea haki nembo yetu SportPesa na kampuni inaamini sisi kama wadhamini wakuu imekuwa ni moja ya chachu iliyosababisha Simba Sports Club kufuzu hatua hii”

“Tunachokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi tuliyotoa wakati tunasaini mkataba wa udhamini mwaka 2017 kuwa tutatoa bonasi ya Shilingi Milioni 50 endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itafuzu katika hatua ya robo fainali kwenye kombe la shirikisho la mabingwa Afrika, alihitimisha.

Akiongea kwa upande wa Simba SC, Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez alianza kwa kusema:

“Nichukue nafasi hii kuipongeza SportPesa kwa kufuata kila makubaliano yaliyopo kwenye mkataba kwa kutoa bonus ya Sh. 50,000,000 baada ya kufanikiwa kufika robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika”

“Sportpesa imekuwa ikitoa bonus kila tunapofanya vizuri katika michuano mbalimbali iwe ya ndani au ya kimataifa na hilo ni kwa mujibu wa mkataba, nawapongeza sana” 

“Tunaamini Sportpesa wamekuwa chachu kubwa kwetu kufanya vizuri katika michuano mbalimbali kutokana na motisha wanayotoa tena kwa wakati.”

“Katika kipindi chote cha mkataba wetu mmekuwa mkitimiza makubaliano ambayo mafanikio tuliyopata tunaamini mna mchango mkubwa”

SportPesa ni wadhamini wakuu wa klabu ya Simba na Yanga kwa kipindi cha miaka mitano sasa.

Mwisho.

Share this:
Back To Top