Kwa mara nyingine tena SportPesa imetoa mshindi wa Jackpot bonus, Mzee Ally Suleimani Iswizilo, ambaye ni mkazi wa Mwanza wilaya ya Nyamagana, kata Nyegezi. Ally amejishindia bonus ya shilingi 12,209,017 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13.
Akifanya mahojiano katika ofisi za SportPesa,Mzee Ally alisema alianza kucheza na SportPesa kwa takribani miaka miwili.
“Katika kipindi chote hicho nimewahi kufaulu ushindi wa Supa Jackpot bonus ambao leo ni ushindi wangu wa tatu, ushindi wa kwanza nilipata shilingi 680,000, ushindi wa pili nilipata shilingi 500,000, na ushindi wa leo ndio huu wa shilingi 12,209,017” Alisema Ally.
Aliongeza kwa kusema kuwa aliifahamu SportPesa kupitia maagazeti na Luninga, aliweza kushawishika kuanza kucheza baada ya kuona ni mchezo ama burudani inayoendana na rika lake.
“Huwa nateremsha michez0 yangu 13 ninaikopi kisha hukaa na kuanza kuipanga kutokana na fomula yangu ambayo ninaijua mwenyewe hadi ninapofikia hatua ya kuanza kubashiri.
Mzee Ally amekuwa akitumia shillingi 20,000, tokea ameanza kucheza Mid-week jackpot, kwa kuweka mikeka 2, na hii ilitokana na kutokufahamu fomula ambayo ingeweza kumsaidia kushinda
“Katika kila mchezo ambao nilikuwa nina faili ambalo nilikuwa nahifadhi kila michezo ambayo nimekosa na kuifanyia tathimini ni wapi nilikosea, na inapotoka mid-week jackpot nyingine mpya huwa nachukua matokeo na kulinganisha na yaliyopita, kwahiyo ikawa inanichukua muda mrefu sana,hadi nilipoweza kufanikiwa kupata fomula ambayo iliniwezesha kushinda.”
Akizungumzia kuhusu mikeka aliyoshinda, Ally alisema alipanga mikeka ya mechi 12 na mechi 10, na kila timu ilivyokuwa inatiki alikuwa akifwatilia kwa ukaribu huku akiwa na karatasi yake ambao alikuwa ameandika mikeka yake yote, hadi saa nne kamili ambapo gemu ya mwisho ndo iliisha.
” Wakati mikeka inatiki nilikuwa najisikia vizuri na niliweza kupokea meseji yangu ya ushindi ndani ya muda mchache baada ya mechi ya mwisho kuisha kutoka kwa mtoa huduma kwa wateja anayeitwa Jamila.
Wakati ninashinda, nilikuwa na mke wangu na Watoto, ambao wamekuwa wakinicheka na kuniambia baba mechi hizi huwezi kushinda, pia mke wangu amekuwa akiniambia siwezi kushinda hela ya mzungu kwa kutumia hesabu.
Mimi nilikuwa najiamini kwa sababu nilikuwa nimeshaweka fomula ambayo itaweza kunipatia ushindi, baada ya kupokea meseji ya ushindi kutoka SportPesa mke wangu aliomba nimfundishe na yeye jinsi ya kucheza.
Kiasi hiki cha fedha nilichoshinda, nitakitumia kumalizia ujenzi wa nyumba zangu ambazo ziko tabata bunyokwa, kwa kuziwekea umeme,maji na kumalizia jiko kwenye nyumba ambayo haijamalizika jiko, ili wapangaji wangu waweze kukuta mahali pazuri.
Mzee Ally yeye anatumia simu yake aina ya WE+, ambayo ameshajisajili na SportPesa. Kwa mkeka wa wiki hii nimeshadownload mechi zangu 13 na kuziandika pembeni.
Nilichagua kucheza na SportPesa ili nisichukue muda mwingi sana wa kuhangaika sana, ndo maana huwa nacheza mkeka wa mechi 13 na mechi 17, kwa sababu mimi nacheza wakati nikiwa nimepumzika, ndo maana huwa ninadownload mkeka wa mechi 13.

Kwa Mkeka huu, kuanzia saa mbili usiku hadi saa sita nitakuwa nimeshamaliza kuupanga na tayari kwa kubeti, kwa sababu tayari nimeshaweka fomula yangu ambayo itanisaidia kupata ushindi.
Ningependa kuwashauri watu wacheze huu mchezo kama wanavutiwa nao, wasicheze kwa sababu wanamuona Ally ameshinda hawataweza kuufurahia. Kuna Rafiki yangu mmoja yeye alikuwa anatumia kwa wiki shilingi 100,000 na hakuwahi kushinda hadi leo kiasi cha yeye kutofurahia mchezo huu, Mchezo huu ni bora kucheza kama unavutiwa nao.
Akimpongeza mshindi Ally Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimsihi Mzee Ally kuendelea kucheza na SportPesa na kwa maelezo yake anaonyesha ipo siku ataibuka mshindi.
“Kama Mzee Ally anatenga muda ili kufatilia matokeo ya mechi alizopoteza inamaanisha anafatilia jinsi mechi zinavyoenda ikiwemo historia za wachezaje na hii, hii ni ishara kuwa siku tutampigia Mzee Allly kama mxhindi wetu wa Jackpot ama Supa Jackpot”
“Nichukue fursa hii kumpongeza Mzee Ally kwa kufanikiwa kushinda bonasi ya zaidi ya milioni 12, inafurahisha kuona Mzee wa umri kama wake anacheza hizi jackpot akiwa na nia ya kutimiza malengo yake”
Cha mwisho ni kuwakumbusha watanzania kuendelea kucheza na SportPesa kwani kwetu ushindi ni mwingi, unaweza cheza jackpot zote mbili ama unaweza cheza michezo ya kasino kuna Aviator na Virtual Football Pro au multibet ambayo ina bonus ya mpaka 1000% ya ushindi ambao utaupata.
Supa Jackpot yetu wiki hii imesimamia TZS 1,137,260,419.

