MC Alger yawasili Zanzibar Kuivaa Yanga SC: Maandalizi ya CAF Champions League | Live score

- Rasmi MC Alger yawasali Zanzibar kuivaa Yanga SC mchezo wa CAF Champions League, Novemba 28, 2026 Uwanja wa New Amaan Complex.
- Kwa habari za papohapo za Yanga SC vs MC Alger fuatilia SportPesa Blog, huku SP Score ikikuandalia livescores.
- Msafara wa wachezaji 25 ukiwa chini ya kocha wa muda Karim Delhoum akibeba mikoba ya Khaled Ben Yahia umeanza mazoezi mepesi.
- Tiketi za pambano zimeanza kuuzwa huku joto la mchezo huu wa hatua ya makundi likizidi kupanda.
Klabu ya MC Alger yawasili Zanzibar kuivaa Yanga SC kwenye mchezo wa hatua ya makundi wakiwa ugenini.Waarabu hao wa Algeria wameweka kambi kujiandaa kwa mchezo wao muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya wenyeji wao, Yanga SC. Kikosi kamili kimewasili kikijumuisha wachezaji muhimu akiwemo Ramadane, Gourari na Hammach kwa upande wa makipa.
Safari hii ya MC Alger inathibitisha kuwa maandalizi ya mchezo huo wa Jumamosi, Novemba 28, yameanza rasmi. Yalla Shoot iliripoti kuwa klabu hiyo ilishiriki video ya kuwasili kwao Jumatano, Novemba 25, ikionyesha wachezaji na benchi la ufundi wakishuka kutoka ndege.
SOMA HII PIA:Yanga SC Yaweka Kambi Zanzibar: Fadlu Ajiandaa Kuikabili MC Alger
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Maandalizi ya MC Alger Zanzibar
Baada ya kuwasili, MC Alger inatarajiwa Novemba 26 imeanza mazoezi mepesi na kisha kuingia kwenye ratiba kamili ya maandalizi.Novemba 27 wachezaji wa timu hiyo akiwemo kiungo Mohamed bin Khumasas wanatarajiwa kuutumia Uwanja wa New Amaan kwa mazoezi.Lengo kuu ni kuzoea hali ya hewa na mazingira ya Zanzibar kabla ya kukabiliana na Yanga SC, ambao pia wameweka kambi visiwani humo.
APS (Shirika la Habari la Algeria) limethibitisha safari hii na mechi ya Jumamosi, likisisitiza umuhimu wa mchezo huu kwa klabu hiyo ya Algeria katika mashindano ya CAF Champions League.
SOMA HII PIA:Yanga vs MC Alger Bei ya Tiketi na Namna ya Kununua kwa Mechi ya CAF Champions League
Kikosi cha MC Alger na matarajio
MC Alger wamkuja na kikosi kazi kamili gado kuwakabili Yanga SC kikijumuisha wachezaji 25.Imejumuisha wachezaji wao muhimu ikiwemo washambuliaji 8 wakiongozwa na Nduwumwe, Bayazid, Konate. Klabu hiyo inajulikana kwa kuwa na wachezaji wenye uzoefu na vipaji, ambao watajaribu kupata matokeo chanya ugenini.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, kwani timu zote mbili zina malengo makubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids itatumia faida ya nyumbani na uungwaji mkono wa mashabiki wao.
Hitimisho
Ni wazi MC Alger yawasili Zanzibar kuivaa Yanga SC ikiwa chini ya kocha wa muda Karim Delhoum akibeba mikoba ya Khaled Ben Yahia aliyekuwa kocha mkuu.Kuwasjili kwa wapinzani hawa kunaongeza joto la mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Yanga SC. Mashabiki wa soka wanatarajia kuona pambano la kusisimua Jumamosi, Novemba 28, huku timu zote zikiwa zimejiandaa kikamilifu kwa ajili ya ushindi.

