Yanga SC wametua Zanzibar kwa maandalizi ya mechi za CAF na NBC Premier League | Fadlu ameanza kazi

ByLunyamadizo Mlyuka

November 8, 2026
Yanga SC wametua Zanzibar kwa maandalizi ya mechi za CAFDavidsDavids
  • 08/11/2026 Yanga SC wametua Zanzibar kwa maandalizi ya mechi za CAF na NBC Premier League 2026/27.
  • Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini ameanza kazi rasmi kuwanoa wachezaji wa timu hiyo inayotetea taji la NBC Premier League.
  • Wachezaji waliopo kambini ni Aziz Ki, Zimbwe Jr, Sure Boy, Dickson Job, Aboutwalib Mshery.
Yanga SC wametua Zanzibar kwa maandalizi ya mechi za CAF
Fadlu Davids Kocha Mkuu Yanga SC

Mabingwa watetezi wa ligi, Yanga SC wametua Zanzibar kwa maandalizi ya mechi za CAF na NBC Premier League 2026/27.Hii ni kambi maalumu wakati huu wa mapumziko ya kalenda ya FIFA.08/11/2026 msafara uliondoka Dar na kufika salama Zanzibar chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini ambaye ameanza kazi rasmi mrithi wa mikoba ya Manqoba Mngqithi.

SOMA HII PIA:Hizi hapa mechi 3 za kwanza za Kocha Fadlu Davis Yanga SC: 2 ni za Ligi Kuu NBC na moja ni dhidi ya Waarabu MC Alger kutoka Algeria

Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kazi imeanza mara baada ya Yanga SC kutua Zanzibar

Mara baada ya msafara wa Yanga SC kutua Zanzibar kazi imeanza.Kocha mpya Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini mbinu zake zimeanza kutumika.Kwa mara ya kwanza ameanza kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo yenye maskani yake Jangwani, Kariakoo.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Zimbwe Jr, Duke Abuya, Aziz Andambwile, Aboutwalib Mshery.Dickson Job, Sure Boy,Clement Mzize,Kibwana Shomary.Kiungo Aziz Ki,Boka, Yao wapo kambini Zanzibar.

Mechi zijazo za Yanga SC chini ya Fadlu Davids

Kwa mujibu wa Ratiba ya Bodi ya Ligi Kuu ya NBC, baada ya kumalizika kwa ratiba ya mechi za timu za taifa kufuzu AFCON 2027, Yanga SC watashuka uwanjani Novemba 20, 2026. Ratiba inaonyesha mechi ya Polisi Tanzania vs Yanga SC Uwanja wa Ushirika Moshi. Ratiba ya mechi ya 2 ni ya Yanga SC vs MC Alger ya Algeria, mchezo huu ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi ya mwisho itakuwa Fountain Gate vs Yanga SC mechi inayotarajiwa kupigwa Desemba 12, 2026.

SOMA HII PIA:Rasmi Fadlu Davids ni kocha mpya Yanga SC 2026/27 | SportPesa Blog

Hitimisho

Yanga SC imetinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.Mchezo wa kwanza inatarajiwa kuanza nyumbani ni dhidi ya MC Alger ya Algeria.28/11/1016 saa 1:00 usiku.Mechi ya pili inatarajiwa kuwa Desemba 5, 2026 itakuwa dhidi ya Club Africain ikiwa ugenini kwa Kundi B.

Share this: