Atletico Madrid vs Barcelona 8/11/2026: La Liga 2026/27, Live score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu
- Ligi Kuu nchini Hispania, La Liga itaendelea leo Jumapili 8/11/2026, huku mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu ikiwa ni Atletico Madrid vs Barcelona.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Riyadh Air Metropoitano uliopo jijini Madrid, Hispania majira ya saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
- Atletico wanaingia katika mchezo huu wakiwa katika nafasi ya 3 na pointi zao 28 walizokusanya katika michezo 11, huku Barclona wao wakiwa vinara wa msiamo na pointi zao 30.
- Unaweza kufuatilia matokeo ya mchezo huu live kupitia SportPesascore.
Ligi Kuu nchini Hispania, La Liga itaendelea leo 8/11/2026, huku mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu ikiwa ni Atletico Madrid vs Barcelona. Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Riyadh Air Metropoitano uliopo jijini Madrid, Hispania majira ya saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Atletico wanaingia katika mchezo huu wakiwa katika nafasi ya 3 na pointi zao 28 walizokusanya katika michezo 11, huku Barclona wao wakiwa vinara wa msiamo na pointi zao 30.
Weka mkeka wako wa mechi ya Atletico Madrid vs Barcelona ushinde kupitia odds kubwa zilizoboreshwa za SportPesa kwa kugusa hapa chini.

Atletico Madrid vs Barcelona h2h

Historia ya makutano ya timu hizi mbili inaonyesha Barcelona wamekuwa na rekodi bora zaidi. Katika mechi 5 zilizopita Barcelona wamesginda mechi 3 huku Atletico Madrid wakishinda mechi 2. Utofauti wa pointi 2 kati yao unaufanya mchezo huu kuwa mgumu na usiotabirika.
Fomu za timu
Atletico Madrid haijawahi kutwaa ubingwa wa La Liga tangu msimu wa 2020/21, huku ikimaliza katika nafasi ya nne kwenye ligi msimu uliopita, ikiwa nyuma kwa pointi 25 dhidi ya mabingwa Barcelona. Hata hivyo, kikosi cha Atletico cha sasa kinaonekana kuwa na uwezo wa kupambana vikali kuwania ubingwa wa msimu wa 2026/27. Chini ya kocha Diego Simeone, Atletico imeshinda michezo tisa, kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja kati ya michezo 11 ya ligi iliyocheza. Pia ina rekodi bora zaidi ya ulinzi, ikiwa imeruhusu mabao manane pekee. Atletico imeshinda michezo yake saba ya mwisho ya La Liga, ikiwemo ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid kabla ya mapumziko ya mwisho ya michezo ya kimataifa.
Barcelona nayo haijapoteza mchezo wowote wa ligi dhidi ya Atletico Madrid ikiwa ugenini tangu Oktoba 2021, hivyo itakuwa na dhamira ya kuendeleza rekodi hiyo nzuri. Kikosi cha Hansi Flick kiliona mfululizo wake wa ushindi wa michezo 11 tangu mwanzoni mwa msimu ukikatika Oktoba 20, baada ya kufungwa mabao 4-2 na Paris Saint-Germain katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Siku tano baadaye, Barcelona ilipoteza tena kwa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa La Liga. Hata hivyo, kikosi hicho cha Catalunya kimefanikiwa kurejea kwenye njia ya ushindi kwa kuichapa Alaves kwa mabao 6-1 katika mchezo wake wa mwisho wa ligi.
SOMA HII PIA: Atletico Madrid Fixtures and Latest Scores – Spanish Football
Msimamo

Kikosi cha kocha Diego Simeone, kinaingia katika mchezo huu kikiwa katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi. Atletico Madrid wamevuna pointi 28 katika michezo 11 waliyocheza. Barcelona waowanaongoza msimamo na pointi zao 30. Hii inamaanisha kuna tofauti ya pointi 2 tu kati yao.
Utabiri wa matokeo
Kwa mtazamo wa wahariri, kwa kuangalia rekodi zao Barcelona wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu. Kwa kuwa Atletico wanacheza nyumbani, Barcelona hawapaswi kubweteka kwani Atletico wanaweza kuwashangaza. Ikumbukwe kuwa haya si matokeo halisi na wanaobashiri wanapaswa kuchambua mikeka yao vizuri na kubashiri kistaarabu.
SOMA HII PIA: Atletico Madrid vs Bayern Munich 3/11/2026: UEFA Champions League, Live score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu
Vikosi vinavyotarajiwa

Kunatarajiwa kuwa na maadiliko kadhaa ya vikosi vya timu zote mbili. Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na changamoto za majeraha, vifungo na utimamu wa wachezaji. Vikosi vinavyotarajiwa ni kama ifuatavyo;
Kikosi kinachorajiwa cha Atletico Madrid
Kipa: Oblak
Walinzi: Llorente, Pubill, Hancko, Grimaldo
Viungo: Simeone, Barrios, Hjulmand, Baena, Lee,
Mshambuliaji: Alvarez.
Kikosi kinachotarajiwa cha Barcelona
Kipa: J Garcia
Walinzi: Farinas, Cubarsi, Martin, Cancelo
Viungo: Bernal, Pedri, Yamal, Fermin, Gordon
Mshambuliaji: Raphinha.
SOMA HII PIA: Atletico Madrid 1-1 Inter Milan | Highlights, goals, H2H
Hitimisho
Atletico Madrid vs Barcelona ni ratiba ya mechi kali itakayopigwa leo Jumapili 8/11/2026 majira ya saa 5 usiku. Mechi hii inatarajiwa kutoa taswira mpya ya mbio za ubingwa wa La Liga. Endelea kufuatilia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.

