Tanzania Prisons vs Transit Camp FCPrisonsPrisons

Tanzania Prisons vs Transit Camp FC
Kikosi cha Prisons

Tanzania Prisons vs Transit Camp FC: Uchambuzi wa Mchezo wa NBC Championship League

  • Mechi ya funga kazi Oktoba ni Tanzania Prisons vs Transit Camp FC Oktoba 23,2026, Ijumaa.
  • Tanzania Prisons kwenye msimamo ipo nafasi ya  6 ikiwa na pointi 10, Transit Camp FC nafasi ya pili na pointi 13.
  • Pambano hilo la NBC Championship League litapigwa Uwanja Sokoine, Mbeya.

Tanzania Prisons vs Transit Camp FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Championship (NBC Championship League).Pambano hili litapigwa Oktoba 23, 2026. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali huku timu zote zikipambana kusaka pointi muhimu katika ligi.Uwanja wa Sokoine,Mbeya saa 10:00 jioni utachezwa.

Hapa tumekuletea uchambuzi wa kina wa mchezo huu, tukichunguza hali ya timu, takwimu za awali, na matarajio ya jumla. Ni muhimu kwa mashabiki na wadau wa soka kuelewa nini cha kutarajia kutoka kwa pambano hili la Championship.

SOMA HII PIA:Stand United 1-1Tanzania Prisons NBC Championship | Msimamo | SportPesa Blog

Shinda mamilioni kwa kupaisha kindege

Rubani kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi ukipaisha kindege. Ni rahisi sana anza safari muda huu uvune mpaka milioni 800. Bofya link hii hapa:-

image

Habari za timu na majeraha

Tanzania Prisons imetoka kupoteza mchezo uliopita Uwanja wa Manungu Oktoba 18,2026 ubao uliposoma Mtibwa Sugar 1-0 Prisons.Inaingia katika mchezo wa mwisho Oktoba kwa hesabu kubwa kusaka pointi tatu muhimu.Inakutana na wenyeji ambao nao wametoka kupoteza wakiwa nyumbani.

Oktoba 17,2026 ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma Transit Camp FC 1-2 KMC FC. Hii ni vita kubwa kwa timu ambazo zimepoteza mechi zilizopita.Uwanja wa Sokoine kutakuwa na mchezo mkali ndani ya dakika 90 huku wachezaji wa timu zote mbili wakiwa kamili kwa kazi.

Takwimu na fomu ya sasa

Wenyeji Tanzania Prisons baada ya mechi 6 kwenye ligi wamepata ushindi mechi 3.Sare 1 huku wakipoteza mchezo mmoja.Pointi 10 kibindoni wakiwa nafasi ya 6 kwenye msimamo.

Transit Camp FC baada ya mechi 6 imepata ushindi kwenye mechi 4, imepoteza mchezo mmoja na kuambulia sare moja.Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 13.Imekuwa kwenye mwendelezo mzuri katika mechi za ligi.

Utabiri na mtazamo wa wahariri

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili. Tanzania Prisons, wakiwa na uzoefu fulani katika ligi, wanaweza kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kujipatia ushindi. Transit Camp FC, kwa upande wao, watahitaji kucheza kwa nidhamu na kutumia fursa zozote watakazopata.

Ushindi mwememba kwa wenyeji kutokana na rekodi za hivi karibuni.Tanzania Prisons 2-1 Transit Camp FC matokeo ya utabiri na sio rasmi.Baada ya mchezo kukamilika matokeo yatakuwa wazi.

SOMA HII PIA:Mbeya Kwanza 2-2 Mbuni NBC Championship | Matokeo yote ya Oktoba 10

Hitimisho

Mchezo kati ya Tanzania Prisons na Transit Camp FC unatoa fursa kwa mashabiki kushuhudia soka la Championship. Timu zote zitajitahidi kupata matokeo chanya, na tunatarajia kuona mchezo wa kusisimua. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa uchambuzi zaidi na habari za michezo.

Share this: