- UEFA Champions League 2026/27 msimu mpya umeanza kutimua vumbi rasmi, ambapo timu zinazoanzia hatua ya awali zinapambana kusaka nafasi ya kufuzu.
- Timu hizo zimeingia katika hatua ya tatu ya kufuzu yaani ‘UCL Third qualifying round.’
- Ikumbukwe hii hii itakuwa Makala ya 72 ya UEFA Champions League tangu kuanzishwa kwake,
- Makala hii inakuletea dondoo muhimu za mambo yote, unayohitaji kufahamu kuhusu hatua ya tatu ya kufuzu.
Hatua ya 3 ya kufuzu ya UEFA Champions League 2026/27 yaani ‘Third UCL qualifying round’ imeingia katika hatua za mechi za marudiano. Hii ni kuelekea kuanza rasmi kwa msimu mpya wa soka 2026/27, ambapo ligi mbalimbali zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi mwezi huu Agosti. Kwa mashindano ya Ulaya hii itakuwa Makala ya 72, tangu kuanzishwa kwake. Makala hii inakuletea baadhi ya dondoo muhimu za hatua hii.
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Cheza Aviator na upate nafasi ya kushinda hadi TZS milioni 800 kwa raundi.
Kuhusu matokeo na ratiba hatua ya 3 ya kufuzu UEFA Champions League

Mbio za kuwania nafasi katika hatua ya 3 ya UEFA Champions League 2026/27 zimezidi kupamba moto wiki hii, baada ya mechi za mkondo wa kwanza. Katika raundi hiyo imeshuhudiwa mabao ya dakika za mwisho, timu kurejea mchezoni kwa kishindo na ushindi mkubwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Sasa ni hatua ya play-off pekee ndiyo imebaki kabla ya kufuzu rasmi kwenye hatua ya ligi.
Siku ya Jumanne huko jijini Sofia, mabingwa wa Bulgaria Levski Sofia waliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa Kazakhstan Kairat Almaty. Ushindi huo ulitokana na bao la dakika za majeruhi lililofungwa na Serginho. Levski walitawala mchezo kwa asilimia 71 ya umiliki wa mpira, huku wakiwazuia Kairat kutopiga hata shuti moja lililolenga lango katika dakika zote 90. Matokeo hayo yanawapa Levski faida ndogo kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa Almaty, ambako Kairat watahitaji kutumia vyema uwanja wa nyumbani ili kupindua matokeo.
Katika mchezo mwingine nchini Sweden, mabingwa wa Slovakia Slovan Bratislava walitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mjällby ugenini. Baada ya kuruhusu bao la penalti muda mfupi baada ya dakika ya 60, Slovan waliendelea kushambulia na kufunga mabao mawili. Manasse Kianga akifunga bao la ushindi dakika ya 94, na kuwapa faida muhimu kabla ya mchezo wa marudiano.
Mabingwa wa Croatia GNK Dinamo Zagreb walicheza moja ya mechi bora zaidi ya raundi hii, kwa kuichapa Kauno Žalgiris ya Lithuania mabao 5-0. Dinamo walikuwa makini sana mbele ya lango, wakicheza kwa kasi na usahihi huku wakitumia vyema udhaifu wa safu ya ulinzi ya wageni. Isipokuwa kama kutatokea muujiza mkubwa nchini Lithuania, mabingwa hao wa Croatia tayari wana mguu mmoja kwenye hatua ya play-off.
Ararat-Armenia waliimarisha matumaini yao ya kusonga mbele, baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Celje ya Slovenia. Baada ya kuruhusu bao la kwanza, wenyeji walibaki watulivu wakimiliki mpira kabla ya kufunga mabao mawili. Mabao hayo yaliwapa ushindi mwembamba kuelekea mchezo wa marudiano wiki ijayo.
Kwa upande mwingine, timu ya Israel Hapoel Be’er Sheva ilipata ushindi muhimu wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa Serbia Crvena Zvezda. Licha ya kubaki na wachezaji 10 kwa zaidi ya dakika 30 za mwisho, Hapoel walionyesha nidhamu kubwa ya kujilinda. Sasa watasafiri kwenda Belgrade wakiwa na faida muhimu.
Katika mfumo wa ligi, mechi iliyovutia zaidi ilikuwa kati ya Union Saint-Gilloise na mabingwa wa Norway Bodø/Glimt, waliomaliza kwa sare ya kusisimua ya 3-3 nchini Belgium. Bodø/Glimt waliongoza mara mbili, lakini Union walisawazisha kila mara kupitia Raul Florucz. Mchezaji wa akiba Promise David alionekana kuipa Union ushindi baada ya kufunga dakika ya 88, lakini Bodø/Glimt hawakukata tamaa na wakasawazisha dakika ya 91 kupitia Odin Lurås Bjørtuft, hivyo kuifanya mechi hiyo kubaki wazi kabisa kabla ya marudiano.
Mabingwa wa Czech Sparta Praha walifanya makubwa baada ya kutoka nyuma na kuwafunga vigogo wa Ufaransa Lyon mabao 2-1. Lyon walitangulia kwa bao la kujifunga muda mfupi kabla ya mapumziko, lakini Sparta walijibu kwa mabao mawili ndani ya dakika sita. Mabao hayo yaliwapa ushindi muhimu uliomaliza rekodi yao mbaya dhidi ya klabu hiyo ya Ligue 1.
Katika mchezo uliochezwa Piraeus, Olympiacos na NEC Nijmegen walitoka sare tasa ya 0-0. Pande zote mbili zilipata nafasi kadhaa lakini hakuna iliyofanikiwa kuzitumia. Hii inafanya mchezo wa marudiano nchini Uholanzi, kuwa moja wa mechi zilizo wazi zaidi katika raundi hii.
Mechi za Jumatano zilihitimishwa kwa Aarhus ya Denmark kuifunga Sabah ya Azerbaijan mabao 2-1, na hivyo kupata faida ndogo kabla ya marudiano. Wakati huo huo, vigogo wa Uturuki Fenerbahçe walichukua hatua kubwa kuelekea hatua ya play-off baada ya kuifunga Sturm Graz ya Austria mabao 2-0. Kwa kuwa nafasi ya kucheza hatua ya play-off iko hatarini, mechi za marudiano wiki ijayo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
KUFAHAMU KUHUSU UCL 2026/27, SOMA HII: Uefa Champions League 2026/27: Timu, Ratiba, Droo, Mfumo wa Mashindano mpaka Fainali
Haya hapa matokeo ya Mkondo wa Kwanza – Raundi ya Tatu ya Kufuzu UEFA Champions League 2026/27

| Na. | Mchezo | Matokeo |
|---|---|---|
| 1 | Mjällby vs Slovan Bratislava | 1-2 |
| 2 | Ararat-Armenia vs Celje | 2-1 |
| 3 | Levski Sofia vs Kairat Almaty | 1-0 |
| 4 | Hapoel Be’er Sheva vs Crvena Zvezda | 1-0 |
| 5 | GNK Dinamo Zagreb vs Kauno Žalgiris | 5-0 |
| 6 | Aarhus vs Sabah | 2-1 |
| 7 | Olympiacos vs NEC Nijmegen | 0-0 |
| 8 | Union Saint-Gilloise vs Bodø/Glimt | 3-3 |
| 9 | Sparta Praha vs Lyon | 2-1 |
| 10 | Fenerbahçe vs Sturm Graz | 2-0 |
Hii hapa ratiba ya mechi za marudiano (Saa za Afrika Mashariki – EAT)

| Na. | Mchezo | Muda (EAT) |
|---|---|---|
| 1 | Kairat Almaty vs Levski Sofia | Saa 12:00 Jioni |
| 2 | Sabah vs Aarhus | Saa 1:00 Usiku |
| 3 | Kauno Žalgiris vs GNK Dinamo Zagreb | Saa 2:00 Usiku |
| 4 | Crvena Zvezda vs Hapoel Be’er Sheva | Saa 3:00 Usiku |
| 5 | Slovan Bratislava vs Mjällby | Saa 3:15 Usiku |
| 6 | Celje vs Ararat-Armenia | Saa 3:15 Usiku |
| 7 | Bodø/Glimt vs Union Saint-Gilloise | Saa 1:00 Usiku |
| 8 | NEC Nijmegen vs Olympiacos | Saa 2:30 Usiku |
| 9 | Sturm Graz vs Fenerbahçe | Saa 3:30 Usiku |
| 10 | Lyon vs Sparta Praha | Saa 4:00 Asubuhi (Jumatano) |
Kuhusu matokeo na ratiba ya UEFA, soma hii: UEFA Champions League results, fixtures and table
Hitimisho

Katika hatua hii ya kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya 3 ya UCL 2026/27, washindi wa kila pambano la raundi ya tatu ya kufuzu watafuzu kwenda UEFA Champions League Play-off Round. Hii ndiyo hatua ya mwisho, kabla ya kuingia rasmi kwenye hatua ya ligi. Timu zitakazoondolewa katika Champions Path zitaendelea kwenye hatua ya play-off ya UEFA Europa League, huku zile zitakazoshindwa katika League Path zikifuzu moja kwa moja kwenye hatua ya ligi ya UEFA Europa League. Timu 7 zitakazoshinda hatua ya play-off zitaungana na timu 29 ambazo tayari zimefuzu moja kwa moja, kukamilisha timu 36 Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

