Lionel MessiMessi
  • Jordan vs Argentina Kombe la Dunia 2026, mechi nyingine ya kuona balaa la ‘mchawi’ na nahodha wa Argentina, Lionel Messi katika mchezo wa mwisho wa Kundi K.
  • Mechi hii kali itapigwa kwenye Uwanja wa Dallas, USA 28 June 2026 saa 11 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.
  • Jeshi la Argentina likiongozwa na staa wao Messi na Julain Alvarez, watavaana na Jordan wanaoburuza mkia kwenye Kundi hilo.
  • Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo

Argentina itakuwa mgeni wa Jordan katika mchezo huu wa kukamilisha ratiba ndani ya Kundi J la Kombe la Dunia 2026. Argentina tayari wamefuzu hatua ya 32 bora, wataingia katika mchezo huu wakisaka nafasi ya kuongoza Kundi hilo kwa ushindi utakaowapa pointi 9. Staa wa Argentina, Lionel Messi ametuma ujumbe mzito katika mechi zake 2 za kwanza akifunga mabao 5 na kuibeba Argentina. Jordan wao wanaingia katika mchezo huu, kusaka heshima.

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Jordan vs Argentina

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Jordan vs Argentina
Jordan vs Argentina

Maelezo ya Mechi

KipengeleMaelezo
MashindanoMchezo wa tatu na wa mwisho wa hatua ya makundi katika Kundi J la Kombe la Dunia la FIFA 2026, utakaoamua nafasi za mwisho za kundi hilo.
Tarehe na MudaMechi itachezwa Jumapili, 28 Juni 2026, kuanzia saa 11:00 alfajiri (EAT).
UwanjaAT&T Stadium, jijini Dallas, Marekani, ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa pambano hili la mwisho la hatua ya makundi.
Msimamo wa Kundi JArgentina wanaongoza kundi wakiwa na pointi 6 na tayari wamefuzu. Austria wanashika nafasi ya pili kwa pointi 3, wakifuatiwa na Algeria wenye pointi 3, huku Jordan wakibaki mkiani bila pointi baada ya kupoteza michezo yao miwili ya kwanza.
Mchezo Mwingine wa KundiSambamba na mchezo huu, Algeria watamenyana na Austria katika pambano lingine la Kundi J litakaloamua timu itakayoungana na Argentina kufuzu hatua ya 16 bora.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Muhtasari wa Jordan vs Argentina

Messi na Alvarez
Messi na Alvarez

Mabingwa watetezi wa mashindano hayo Argentina, wanatarajia kuendeleza rekodi yao ya ushindi wa asilimia 100 katika Kombe la Dunia 2026. Hii ni katika mchezo wao vs Jordan ambao utapigwa Uwanja wa AT&T Stadium, au Dallas, USA. Huu ni mchezo wa kwanza mataifa haya kukutana.

Messi, ambaye amefikisha miaka 39 siku ya Jumatano, ameandika rekodi kadhaa ikiwemo mfungaji bora wa Kombe la Dunia akiwa na mabao 18.

Chini ya kocha Lionel Scaloni, Argentina imekusanya ushindi mechi tisa mfululizo katika mashindano yote, ikitunza nyavu zao katika mechi nane na kuruhusu bao moja pekee. Argentina inapambana kuwa taifa la kwanza tangu Brazil mwaka 1962 kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia. Pia wanataka kuandika rekodi ya kunyanyua kombe hilo kwa mara ya nne katika historia yao.

Jordan ambao wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, tayari wameondolewa kwenye mashindano. Hii ni baada ya matokeo ya vipigo vya 3-1 dhidi ya Austria na 2-1 dhidi ya Algeria.

Jordan wameandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza tangu Ivory Coast mwaka 2006, kufunga katika mechi zao mbili za kwanza za Kombe la Dunia. Changamoto yao kubwa imekuwa safu ya ulinzi, hasa katika mipira ya kona. Mabao matatu kati ya matano waliyofungwa yametokana na kona.

Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa

Jordan hawana majeruhi wala matatizo ya utimamu wa mwili, hivyo kocha Sellami anaweza kuendelea kuwaamini wachezaji waliocheza vizuri dhidi ya Algeria. Kwa Argentina, beki wa kati wa Tottenham, Cristian Romero huenda akakosa mchezo huu baada ya kuumia goti dhidi ya Austria. Pia inawezekana Lisandro Martinez akapumzishwa.

Vikosi vinavyotarajiwa

Jordan

Kikosi cha Jordan
Kikosi cha Jordan
NafasiWachezaji
KipaAbulaila
WalinziAl-Arab, Nasib, Abu Dahab, Haddad
ViungoAl-Rashdan, Al-Rawabdeh, Abu Taha, Al-Taamari
WashambuliajiAl-Mardi, Olwan

Argentina

NafasiWachezaji
KipaEmiliano Martinez
WalinziMontiel, Otamendi, Lisandro Martinez, Tagliafico
ViungoLo Celso, Paredes, Palacios, Almada
WashambuliajiLionel Messi, Lautaro Martinez

Utabiri (Ushindi kwa Argentina)

Jordan vs Argentina Kombe la Dunia 2026
Lionell Messi

Jordan watapambana kwa moyo mkubwa na kujaribu kuleta ushindani, lakini tofauti kubwa ya kiwango, ubora wa kikosi na uzoefu wa Argentina katika mashindano makubwa inaifanya timu hiyo kuwa na nafasi kubwa ya kushinda. Mchezo huu unakutanisha timu ambazo zina asifu tofauti, ni kati ya timu bora sana hasa kwenye ushambuliaji dhidi ya timu dhaifu zaidi kwenye Kundi. Argentina wanataka kuongoza Kundi, huku Messi akijiandaa kuandika rekodi bora zaidi hivyo kwa kuzingatiauchambuzi wa kitaalamu utabiri wetu na maoni ya kiuhariri, ni ushindi kwa Argentina. Ikumbukwe haya ni maoni ya kiuhariri, sio matokeo halisi hivyo Bashiri kistaarabu.

KUJUA RATIBA NA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA GHANA, SOMA HII: Prediction: Croatia vs Ghana FIFA Kombe la Dunia 2026: H2H, team news, odds

Rekodi ya Jordan vs Argentina (H2H)

Timu hizi hazina kumbukumbu ya kukutana kabla ya mchezo huu, hivyo huu unasalia kuwa mchezo wa kihistoria kwa timu hizo.

Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unayapa nafasi kubwa matokeo ya ushindi kwa Argentina. Mechi hii itatoa taswira ya kinara wa Kundi J la mashindano haya. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Jordan vs Argentina kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Jodan
Jodan

Jordan vs Argentina itaanza saa ngapi?

Mechi itaanza saa 11 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) Jumapili tarehe 28 Juni 2026.

Jordan vs Argentina zipo Kundi gani?

Wapo Kundi J pamoja na Austria na Algeria.

KUJUA UCHAMBUZI NA RATIBA YA MECHI IJAYO YA PORTUGAL, SOMA HII: Colombia vs Portugal Kombe la Dunia 2026 Kundi K: Live score, h2h, odds na habari za timu

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.