Mashujaa FC vs Yanga SCBacca Ibrahim
  • Mashujaa FC vs Yanga SC NBC Premier League ni mchezo ujao kwenye ratiba Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
  • Matokeo ya mchezo uliopita Yanga SC 6-0 Yanga SC, Uwanja wa KMC Complex
  • H2H kwenye mechi 5 ushindi ulikuwa kwa Yanga SC

Mashujaa FC imecheza mchezo mmoja dhidi ya Yanga SC kwenye NBC Premier League 2025/26. Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza matokeo yalikuwa Yanga SC 6-0 Mashujaa FC, Uwanja wa KMC Complex. Jumamosi, Juni 13, 2026 wababe hawa wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

SOMA HII: Yanga SC 6-0 Mashujaa FC NBC Premier League/ Highligts, stats, standigs

Je hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Mashujaa FC vs Yanga SC NBC Premier League ni Jumamosi Juni 13, 2026

Mashujaa FC vs Yanga SC
Okello na Mudathir Yahya, viungo wa Yanga SC

SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC NBC Premier League 2025/26 mechi za lala salama | SportPesa Blog

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Mchezo ujao kwenye ratiba ni Mashujaa FC vs Yanga SC NBC Premier League 13:15 UTC. Wananchi wanaongoza ligi na pointi 60 baada ya mechi 25, wenyeji nafasi ya 11 na pointi 27.

Huu ni mzunguko wa pili kwa wababe hawa wawili kusaka pointi 3 uwanjani. Yanga SC wanapambania kutetea taji la ligi huku Mashujaa FC wakipambania kuwa ndani ya 10 bora. Mtanange mkali kwa wababe hawa nani atavuna ushindi? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa za hivi punde na matokeo.

Msimamo wa Mashujaa FC vs Yanga SC

TimuNafasiPointiUshindiSarePotezaMagoli KufungaMechi Zilizochezwa
Yanga SC16018615825
Mashujaa FC112751281225

H2H Mashujaa FC vs Yanga SC

Mashujaa FC vs Yanga SC
Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC

H2H Mashujaa FC vs Yanga SC wamekutana katika mechi 5 NBC Premier League. Mabingwa watetezi wamepata ushindi mechi zote wakipata ushindi nje ndani. Kipigo kikubwa walichotoa dhidi ya Mashujaa FC ni goli 6, mchezo wa mzunguko wa kwanza 2025/26

TareheMechiMatokeo
19 Januari 2026Yanga SC vs Mashujaa FC6-0
23 Februari 2025Mashujaa FC vs Yanga SC0-5
19 Desemba 2024Yanga SC vs Mashujaa FC3-2
5 Mei 2024Mashujaa FC vs Yanga SC0-1
8 Februari 2024Yanga SC vs Mashujaa FC2-1

Yanga SC kwenye mechi 5 safu ya ushambuliaji imefunga magoli 17. Mashujaa FC imefunga magoli 3. Ushindi kwa mabingwa watetezi umekuwa asilimia 100 na magoli mengi katika mechi za NBC Premier League.

SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Matokeo ya mchezo wa mzunguko wa kwanza

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga SC ilipata ushindi wa magoli 6-0. Magoli ya Yanga SC yalifungwa na  Mohamed Damalo dakika ya 8, Duke Abuya dakika ya 28, Pacome Zouzoua dakika ya 35, Prince Dube dakika ya 79, Mudathir Yahya dakika ya 80 na Depu dakika ya 89. Kiungo Mudathir alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Hitimisho

Mashujaa FC vs Yanga SC ni mchezo ambao wageni wanapewa nafasi kubwa kushinda kutokana na rekodi walizonazo. Licha ya ubora walionao bado Mashujaa FC sio timu ya kuikatia tamaa. Matokeo rasmi kwenye mchezo huo yatapatikana baada ya dakika 90. Endelea kufuatilia blog ya SportPesa kwa taarifa za hivi punde.

Share this: