- Leo Jumanne ya moto kwenye Robo Fainali ya mashindano ya UEFA Champions league.
- Ukiachana na Real Madrid wanaoikaribisha Bayern Munich, pia kuna mechi ya Sporting Lisbon vs Arsenal.
- Mechi hii imepewa jina la utani la ‘Viktor Gyokeres derby’, ikimaanisha ni dabi ya Gyokeres staa wa Arsenal atakayecheza dhidi ya timu yake ya zamani.
Mechi nyingine kali ya UEFA Champions league itapigwa leo Jumanne huko nchini Ureno. Ni Sporting Lisbon vs Arsenal mechi ya mkondo wa kwanza, ya kusaka nafasi ya Nusu Fainali ya mashindano hayo makubwa Ulaya. Mechi hii imepewa jina la utani la ‘Viktor Gyokeres derby’, ikimaanisha ni dabi ya Gyokeres staa wa Arsenal aliyojiunga nayo msimu huu, dhidi ya timu yake ya zamani.
SOMA HII PIA: Sporting Lisbon: Ratiba za Mechi, Kikosi, Matokeo na Utabiri wa Kubashari
Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sporting Lisbon vs Arsenal h2h

Timu hizo zimekutana mara 7 katika historia ya michezo ya mashindano ya Ulaya, ambapo Arsenal wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 3. Sporting Lisbon hawajawahi kushinda mechi yoyote ndani ya muda wa kawaida, dhidi ya Arsenal. Hivyo, mechi nne zilizosalia ziliisha kwa sare na sasa huu unakuwa mkutano wao wa nane je, nani ataibuka mbabe?
Vikosi vinavyotarajia kuanza Sporting Lisbon vs Arsenal
Sporting Lisbon

Kipa: Silva
Walinzi: Vagiannidis, Diomande, Inacio, Mangas
Viungo: Braganca, Morita, Catamo, Trincao,
Washambuliaji: Goncalves, Suarez
Arsenal
Kipa: Raya
Walinzi: White, Gabriel, Saliba, Calafiori
Viungo: Zubimendi, Rice, Odegaard, Martinelli
Washambuliaji: Gyokeres, Madueke
SOMA HII ZAIDI: arsenal vs Chelsea- Ni Dabi ya London.
Habari za timu
Arsenal

Arsenal wataingia katika mchezo huu wa ugenini, wakiwa na lengo la kuepuka kipigo cha tatu mfululizo. The Gunners wamepoteza michezo miwili mfululizo, kwanza walifungwa na Manchester City kwenye fainali ya Kombe la EFL. Halafu wakapoteza 2-1 dhidi ya timu ya Championship, Southampton katika robo fainali ya FA Cup.
Ndoto ya Arsenal ya kushinda makombe manne msimu huu ilionekana kuwa na matumaini kwa muda, lakini matokeo ya hivi karibuni yamepunguza kasi hiyo. Baada ya kuchapwa na Manchester City kwenye fainali ya Carabao, kikosi cha Mikel Arteta kilishindwa kutumia ubora wao dhidi ya Southampton. Bao moja lililofungwa na Viktor Gyokeres, halikutosha kuiepusha Arsenal na kipigo. Hata hivyo, bado wana nafasi kubwa ya ubingwa wa EPL ambapo wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 9.
Arsenal hawajapoteza mchezo wowote kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, wakimaliza hatua ya makundi kileleni na kuiondoa Bayer Leverkusen katika hatua ya 16 bora. Pongezi kwa mabao ya Eberechi Eze na Declan Rice katika mchezo wa marudiano, ulioisha kwa ushindi wa 2-0. Hii inakuwa robo fainali ya 3 mfululizo kwa Arsenal.
Gyokeres, mshambuliaji raia wa Sweden atakuwa anakutana na timu yake ya zamani ya Sporting, ambayo aliwahi kuitumikia na kufunga mabao 97 katika mechi 102. Rekodi hizi ni kabla ya kuhamia Arsenal mwaka 2025. Akiwa kwenye msimu wake wa kwanza na Arsenal, amekuwa muhimili muhimu wa mafanikio ya timu hiyo hasa baada ya kukosekana kwa Straika, Gabriel Jesus.
Sporting Lisbon
Kwa upande mwingine, wenyeji Sporting wataingia katika mchezo wa leo wakiwa na morali kubwa baada ya kushinda mechi tatu mfululizo. Sporting wana rekodi bora ya uwanja wa nyumbani, wameshinda mechi 17 mfululizo mbele ya mashabiki wao. Ushindi wao wa 4-2 dhidi ya Santa Clara, umewafanya wabaki nafasi ya pili kwenye ligi ya Ureno. Mabao yalifungwa na Pedro Goncalves, Daniel Braganca, Francisco Trincao na Rafael Nel.
Katika Ligi ya Mabingwa, Sporting wamekuwa na rekodi bora nyumbani, wakishinda mechi zote tano walizocheza dhidi ya timu kama Paris Saint Germain. Ikumbukwe baada ya kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bodo/Glimt katika hatua ya mtoano, walirejea kwa kishindo na kushinda 5-0 nyumbani na kufuzu robo fainali.
SOMA HII PIA: Tetesi za soka usajili Gyokeres kwenda Arsenal, Man United kufanya ‘ubaya ubwela?’
Taarifa za majeruhi
Arsenal

Kwa upande wa Arsenal, Gabriel Magalhaes anatarajiwa kucheza licha ya kuwa na majeraha madogo. Declan Rice na Leandro Trossard pia wako tayari, lakini Bukayo Saka na Jurrien Timber bado hawajawa fiti. Wachezaji wengine watakaokosekana ni pamoja na Eberechi Eze, Piero Hincapie na Mikel Merino.
Sporting Lisbon
Kwa Sporting, Luis Suarez amekuwa kwenye kiwango kizuri, akifunga katika mechi tatu za nyumbani za Ligi ya Mabingwa. Pigo jingine kwa Wareno hao ni nahodha, Morten Hjulmand ambaye atakosekana kutokana na adhabu.
Utabiri na hitimisho
Sporting Lisbon vs Arsenal ni Robo fainali nyingine ngumu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa leo Jumanne. Timu zote zinaingia zikiwa na hali tofauti, lakini zenye ubora mkubwa. Arsenal wana rekodi nzuri katika hatua hii ya mashindano, huku Sporting wakiwa imara sana nyumbani. Inatarajiwa mechi ya ushindani mkubwa na upo uwezekano wa kuisha kwa sare ya mabao.

