MpanzuMpanzu
  • Ligi Kuu Bara (NBC Premier League) imerejea rasmi baada ya mapumziko ya kupisha ratiba ya kimataifa ya FIFA.
  • Kesho Aprili 2, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, kutakuwa na mchezo mkali wa Simba SC vs Coastal Union.
  • Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo na rekodi bora ya ushindi, ambapo wameshinda mechi 8 kati ya 10 zilizopita walipokutana.

Moto unazidi kuwaka! Ligi Kuu Bara (NBC Premier League) imerejea rasmi baada ya mapumziko ya kupisha ratiba ya kimataifa ya FIFA. Kesho Aprili 2, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, kutakuwa na mchezo mkali wa Simba SC vs Coastal Union. Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo na rekodi bora ya ushindi, ambapo wameshinda mechi 8 kati ya 10 zilizopita walipokutana.

SOMA HII PIA: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 ni moto | Msimamo, Mzizima Dabi, Kariakoo Dabi

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Simba SC vs Coastal Union h2h

NBC Premier League wiki ya moto
Loemba Inno

Katika miaka ya karibuni timu hizi zimekutana mara 23, ambapo Simba wameshinda mechi 16. Coastal wao wameshinda mechi moja tu, huku mechi 6 zikisha kwa matokeo ya sare. Hivyo hii ni nafasi nyingine kwa kila upande kuandika historia mpya.

Matokeo ya mechi zilizopita kati ya Simba SC vs Coastal Union

Baadhi ya remichezo baina ya timu hizi ni kama ifuatavyo;

01/03/2025, Coastal Union 0-3 Simba SC

04/10/2024, Simba SC 2-2 Coastal Union

09/03/2024, Coastal Union 1-2 Simba SC

21/09/2023, Simba SC 3-0 Coastal Union

09/06/2023, Simba SC 3-1 Coastal Union

03/12/2022, Coastal Union 0-3 Simba SC

07/04/2022, Coastal Union 1-2 Simba SC

31/10/2021, Simba SC 0-0 Coastal Union

11/07/2021, Simba SC 2-0 Coastal Union

21/11/2020, Coastal Union 0-7 Simba SC

SOMA HII ZAIDI: NBC Premier League ratiba 2025/26 Aprili | Azam FC vs Simba SC | Yanga SC vs Prisons | Msimamo

Habari za timu na kauli za makocha

NBC Premier League ratiba 2025/26 Aprili
Kibabage Nickson

Mechi hii muhimu inatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Licha ya utawala wa Simba SC kwenye mbao za matokeo ‘Score board’ baada ya mchezo, lakini kwa kawaida huu ni mchezo ambao unakuwa mgumu siku zote. Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema: “Mara zote mchezo huu unakuwa mgumu na uthibitisho mnakumbuka mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu uliopita tulipata sare, tumeangalia mapungufu yao na tumejipanga kuwazidi kimbinu na kuvuna ushindi.”

Naye Ofisa Habari wa Coastal Union, Hussein Mchomvu ‘Diego’ amesema: “Kwa ujumla kama uongozi tumefanya maandalizi yote ya nje na ndani ya uwanja, kuhakikisha tunapata matokeo licha ya ugumu wa mchezo.”

Simba SC vs Coastal Union, msimamo unasemaje?

Simba SC vs Coastal Union
MSIMAMO wa Ligi Kuu Bara

Mpaka sasa Simba wanakamatia nafasi ya 3 kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi 31 katika mechi zao 14 walizocheza mpaka sasa. Katika msimamo ni Yanga SC na Azam FC Pekee ndizo zimekusanya pointi nyingi dhidi ya Simba, ambapo Yanga SC wana pointi 38 na Azam wana pointi 32 zote zikicheza mechi 16 mbili zaidi ya mechi walizocheza Simba SC. Coastal Union wao wanakamatia nafasi ya 13 kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi 15 tu, katika mechi 16 walizocheza. Kwa nafasi waliyopo Coastal wana kazi kubwa kujiondoa eneo la hatari.

SOMA HII PIA: Ishu ya Chama kurudi Simba SC ukweli huu hapa! Kipa mpya atambulishwa: Tetesi za usajili mpya Ligi Kuu Bara 2025/26

Hii hapa ratiba ya mechi zijazo kwa Simba SC NBC Premier League

Azam FC vs Simba SC, Aprili 5,2026 saa 1:00 usiku

Fountain Gate FC vs Simba SC, Aprili 9, 2026, saa 10:00 jioni

Namungo FC vs Simba SC, Aprili 15,2026 saa 1:00 usiku

Simba SC vs JKT Tanzania, Aprili 19,2026 saa 1:00 usiku

Simba SC vs Tanzania Prisons, Aprili 29, 2026 saa 1:00 usiku

Simba SC vs Yanga SC, Mei 3,2026 saa 11:00 jioni.

Mashujaa FC vs Simba SC, saa 12:15, jioni.

Coastal Union vs Simba SC, Mei 16,2026 saa 10:00 jioni

Simba SC vs Dodoma Jiji FC, Mei 20,2026, saa 1:00 usiku.

Utabiri na hitimisho

Kapombe na Rushine
Kapombe na Rushine

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba SC vs Coastal Union haujawahi kuwa rahisi licha ya utawala wa matokeo kwa Simba SC. Pointi 3 za mchezo huu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo zina maana kubwa kwa kila upande. Kwa Simba SC ni nafasi ya kusogea kileleni mwa msimamo na kuwashusha Azam FC, Lakini kwa kwa Coastal Union ni nafasi yao ya kujiondoa kutoka katika nafasi za hatari. Japokuwa mchezo unatarajiwa kuwa mgumu, alkini Simba wanapewa nafasi kubwa ya ushindi kutokana na fomu yao kulinganisha na wapinzani wao.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.